Bwawa la Mto Nile: Sudan yawa 'mbogo' kwa Ethiopia

Workey Tadele, opereta wa redio, katika Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD), karibu na Guba nchini Ethiopia, mnamo Desemba 26, 2019.

Chanzo cha picha, AFP

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Sudan imejikuta kati kati ya mzozo wa muda mrefu kati ya Ethiopia na Misri kuhusiana na ujenzi wa bwawa katika Mto Nile.

Katika miezi ya hivi karibuni kubadilisha msimamo wake, kama anavyoripoti Zeinab Mohammed Salih kutoka Khartoum.

Linapokuja suala la kujadili bwawa la Renaissance la Ethiopia (Gerd), Msimamo wa Sudan umebadilika mara kwa mara hali ambayo imeifanya kutiliwa shaka.

Mabadiliko haya, kwa sehemu kubawa, yanashiria ongezeko la ushawishi wa jeshi katika serikali ya mpito ambayo inatakiwa kutoa nafasi kwa mfumo wa kidemokrasia baada ya kumng'oa madarakani kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir.

Joto la kidiplomasia limeongezeka wakati kipindi cha mvua kinapokaribia Ethiopia na hifadhi ya maji katika bwawa hilo likipata maji kwa mara ya pili bila ya kufikiwa kwa makubaliano ya jinsi ya kusuluhisha mgogoro uliopo.

The Gerd in construction
Reuters
The Grand Ethiopian Renaissance Dam

Africa's biggest hydropower project

  • Construction beganon the Blue Nile in 2011

  • The $4bn costhas been partly met by citizens buying bonds

  • The power generatedwill transform the lives of millions of Ethiopians

  • Egypt is worriedas it almost entirely relies on the water from the Nile

  • Sudan and Egypt want a guaranteed flow of water

Source: Reuters/BBC
Transparent line

Ethiopia na Misri zimejadili kuhusu mradi huo kwa misingi ya ustawi wao.

Ethiopia inasema bwawa hilo ni muhimu kwa maendeleo kwani itasaidia kuwafikishia nguvu za umeme kwa hadi asilimia 60 ya wananchi wake .

Misri kwa upende wake inasema bwawa hilo linatishia kuathiri mtiririko wa maji wa Mto Nile ambayo inatumia kujikimu.

Sudan, ambayo iko katikati ya nchi hizo mbili, sasa imetoa vitisho vikali.

Mshauri wa baraza kuu la Sudan, Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, alizungumzia vita vya majini "ambavyo vitakuwa vya kutisha kuliko vile mtu angeweza kufikiria" isipokuwa jamii ya kimataifa itasaidia kupata suluhisho

Kubadilika kwa msimamo

Miezi 14 iliyopita mamlaka iliangazia mjadala tofauti,mjini Khartoum.

Mwezi February 2020, Waziri wa rasilimali za maji Yasir Abbas alizungumzia jinsi bwawa hilo kubwa zaidi Afrika litakavyosaidia Sudan.

Picha ya setilaiti iliyopigwa Novemba iliyopita inaonesha sehemu ya hifadhi iliyoundwa na bwawa

Chanzo cha picha, Reuters

Akikubali kwamba kuna masuala madogo yanahitaji kushughulikiwa, alisema bwawa hilo litasaidia mtiririko wa maji katika Mto Nile kuwatabirika zaidi na huenda ikatoa nafasi ya msimu wa tatu wa kilimo

Bwana hilo pia litasaida upatikanaji wa nguvu za umeme kwa gharama nafuu kwa Sudan, ambayo hivi karibuni ilikabiliwa na ukosefu wa umeme kwa saa 12 kwa siku

Lakini mapema mwezi huu, baada ya kugonga mwamba kwa mazungumzo yaliyoongozwa na Muungano wa Afrika kutafuta suluhisho la mzozo kati ya, Misri, Ethiopia na Sudan kuhusiana na suala hilo mjini Kinshasa, Bw. Abbas aliwaambia waandishi wa habari kwamba ni tisho kwa usalama wa kitaifa, ikiwa Ethiopia itajaza maji bwawa hilo kabla ya kusuluhisha masuala yens utata.

Sudan inataka Ethiopia kutia saint mkataba wa maelewano badala ya kufuata muongozo, kuhusu kiwango cha maji katika bwawa hilo na kipindi cha kujaza maji katika hifadhi yake. Pia inataka uwazi katika utakaosaidia kusuluhisha mizozo ya siku zijazo.

Bw. Abbas pia aliambia BBC kwamba Ethiopia inatoa masharti kuhusu maji yanayotumiwa kwa kilimo katika hali ambayo inafanya majadiliano kuwa magumu.

"Bila makubaliano, bwawa hili ni tisho kwa watu wanaoishi upande wa chini wa mto… kwa mazingira na maishaya watu," aliongeza kusema.

Alihoji kuwa Sudan itaathirika zaidi kuliko Misri ikiwa hatua ya kujaza maji bwawa hilo itapunguza kiwango cha maji yanayofika Sudan, kwani Misri ina hifadhi kubwa ya maji katika bwawa lake la Aswan.

'Kuiinulia fimbo Ethiopia'

Hii limejulikana kwa muda mrefu. Kilichobadilika ni ninani aliye na uwezo kati y amajeshi na raia katika utawala wa baada ya kuondolewa -Bashir.

Tishio llolote kwa usalama wa kitaifa kwa sasa litaangaziwa kivyake. Hata hivyo mzozo unaendelea kutokota kati ya Sudan na Ethiopia juu ya suala la mpaka katika eneo linalofahamika kama al-Fashaga umefanya Sudan kutoegemea upande wa Ethiopia.

Mpaka halisi kati ya nchi hizo mbili haujawekwa na licha ya makubaliano ya enzi ya ukoloni kuashiria kwamba al-Fashaga ni sehemu ya Sudan, Waethiopia wamekuwa wakiishi hapo na kulipa kodi kwa mamlaka za Ethiopia.

Mwaka 2008, mwafaka ulifikiwa ambapo Ethiopia ilikubali ni sehemu ya Sudan, lakini Waethiopia waliendelea kuishi hupo.

Sudan, hata hivyo imetumia nafasi ya iliyotolewa na mzozo wa Tigray nchini mwaka jana kuwapeleka wanajeshi wake katika eneo la al-Fashaga.

Wakulima wengi wa Sudan wanategemea Mto Nile kumwagilia mazao yao

Chanzo cha picha, AFP

Serikali ilifanya kampeni kubwa kuwahamasisha watu kuunga mkono hatua ya kijeshi katika eneo hilo. Kampeni hiyo ilijumuisha kuwapeleka watu mashuhuri katika eneo hilo la mpakani na wasanii maarufu kutumbiza watu katika matamasha tofauti mjini Khartoum wakiwa wamevalia sare za kijeshi .

Kaskazini mwa Sudan, vikosi vya ulinzi vimekuwa vikifanya mafunzo ya pamoja na Misri.

"Ni wazi kuwa wanajaribu kuinilia fimbo Ethiopia," Brigedia mstaafu Mahmoud Galender aliiambia BBC.

Kwa upande wake, Ethiopia inaendelea na juhudi za kujaribu kuihakikishia Sudan kwamba bwawa la Gerd halitaathiri nchi hiyo.

Siku ya Jumapili, Waziri Mkuu Abiy Ahmed aliandika kwenye Twitter akisema kwamba Ethiopia " aina nia ya kufanya uharibifu" kwa kuzuia maji ya maji kutofikia nchi hiyo, na kuongeza kwamba maji yaliyoingia katika bwawa hilo mwaka jana ''yalisaidia kuzuia mafuriko katika nchi jirani ya Sudan".

Pia alizungumzia suala la kupokezana taarifa kuhusu kile kinachoendelea kabla ya msimu wa mvua mwaka huu.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Ijapokuwa maneno hayo huenda yasiridhishe Sudan au Misri huku juhudi za kushinikiza mazungumzo zaidi zikiendelea.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry kwa sasa anafanya ziara katika bara hili kwa lengo la kupata uungwaji mkono kutoka kwa washirika wa Mistri kwa lengo la kutafuta suluhisho la kisheria "katika utumizi wa bwawa hilo na kujazwa wake maji katika njia ambayo italinda maslahi ya nchi zote tatu", tarifa ya serikali ya Misri ilisema.

Jenerali wa Burhan wa Sudan pia alitoa ujumbe sawa na huo katika mahojiano ya televisheni wiki iliyopita.