Prince Philip: Raia wa Uingereza ambao hawaungi mkono uwepo wa Ufalme

Iliyochapishwa

Salamu za rambirambi zinatumwa kutoka kila pembe ya dunia kufuatia kifo cha mume wa Malkia wa Uingereza, Mwanamfalme Philip, salamu hizo pia zinaambatana na kuiunga mkono Familia ya Kifalme.

Japo watu wengi wanahuzunika pamoja na familia hiyo,si kila raia wa Uingereza anaunga mkono Ufalme.

Ukiwauliza, watu wengi bado wanasema wanauthamini utamaduni wa ufalme na alama yake kwa Uingereza na watasikitishwa kama Ufalme utaondoshwa. Lakini wapo watu, ambao si wachache pia, wataotaka mabadiliko ya kikatiba ili kuwa na mkuu wa nchi ambaye anapigiwa kura.

Kwa mujibu wa kura ya maoni iliyoendeshwa na taasisi ya YouGov mwezi uliopita, asilimia 63 ya watu nchini Uingereza wanasema Ufalme uendelee. Hata hivyo mtu mmoja kati ya kila watu wanne wangependelea nchi hiyo kuwa na kiongozi mkuu aliyechaguliwa huku mtu mmoja kati ya kila watu 10 wakiwa hawajafanya uamuzi wa kuchagua upande upi baina ya kuendeleza Ufalme ama kuuondosha.

Ikiongozwa na Malkia Elizabeth II, mwenye umri wa miaka 94, Familia ya Kifalme imeitawala Uingereza kwa takribani miaka 1,000 - ukiachana na kipindi cha miaka mitano - katika miaka ya 1600 baada ya Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe (the English Civil War).

Malkia ana majukumu mengi kwa mujibu wa katiba ikiwemo kusaini sheria, kumteua Waziri Mkuu na kufungua mikutano ya bunge, lakini nguvu nyingi za kimajukumu za Ufalme zimekuwa zikipunguzwa kwa miaka kadhaa iliyopita.

Malkia Elizabeth pia ni mtawala wa nchi 54 za Jumuiya ya Madola, ambayo ina mizizi yake na iliyokuwa Dola ya Kikoloni ya Uingereza.

"Binafsi nadhani hatuhitaji tena kuwa na Ufalme. Sina hakika wanafanya kazi gani, na mning'inio wa ukoloni na mambo ya wakati tofauti (na sasa)," anasema Kirsten Johnson, kutoka Derby.

"Ukifikiria muda ambao Malkia Elizabeth alipoingia mamlakani,haikuwa muda mrefu toka kumalizika kwa Vita ya Pili vya Dunia na kipindi hicho Jumuiya ya Madola ilikuwa katika hali tofauti kabisa na ya sasa. Kipindi kiale kilikuwa ni dola hasa, tofauti na sasa.

"Tayari tuna viongozi wa kuchaguliwa, hivyo sioni kwa kweli umuhimu wa kuwa na Ufalme," anaeleza. "Kwa nadharia Malkia inabidi apitishe kila kitu, lakini kiuhalisia, yeye ni nembo tu, tena ni nembo ghali kweli."

Malkia ana majukumu mengi kwa mujibu wa katiba ikiwemo kusaini sheria, kumteua Waziri Mkuu na kufungua mikutano ya bunge, lakini nguvu nyingi za kimajukumu za Ufalme zimekuwa zikipunguzwa kwa miaka kadhaa iliyopita.

Malkia Elizabeth pia ni mtawala wa nchi 54 za Jumuiya ya Madola, ambayo ina mizizi yake na iliyokuwa Dola ya Kikoloni ya Uingereza.

"Binafsi nadhani hatuhitaji tena kuwa na Ufalme. Sina hakika wanafanya kazi gani, na mning'inio wa ukoloni na mambo ya wakati tofaiti (na sasa)," anasema Kirsten Johnson, kutoka Derby.

"Ukifikiria muda ambao Malkia Elizabeth alipoingia mamlakani,haikuwa muda mrefu toka kumalizika kwa Vita ya Pili ya Dunia na kipindi hicho Jumuiya ya Madola ilikuwa katika hali tofauti kabisa na ya sasa. Kipindi kale ilikuwa ni dola hasa, tofauti na sasa.

"Tayari tuna viongozi wa kuchaguliwa, hivyo sioni kwa kweli umuhimu wa kuwa na Ufalme," anaeleza. "Kwa nadharia Malkia inabidi apitishe kila kitu, lakini kiuhalisia, yeye ni nembo tu, tena ni nembo ya ghali kweli."

Mnamo mwaka 2020, garama ya Familia ya Ufalme kutoka kwa walipa kodi wa Uingereza ilikuwa ni pauni milioni 69.4 ($95.3m) kulingana na takwimu zilizotolewa na Makazi ya ufalme -kikiwa ni kiwango cha hali ya juu zaidi kuwahi kurekodiwa.

Pesa hizi huitwa Sovereign Grant na hutumiwa kufadhili mambo kama vile kazi za Malkia na makazi yake, safari rasmi za kifalme, na ukarabati wa kasri za Ufalme , ikiwa ni pamoja na uboreshwaji wa makao makuu ya ufalme na ukarabati wa katika makazi mengine ya ufalme huo ya Frogmore Cottage, ambayo awali yalikuwa nyumba ya Mwanamfalme Prince Harry na mke wake Meghan.

"Pesa za walipa kodi'' huenda kusaidia ndugu wa mbali wa familia ya ufalme ambao, kwasababu ya vyeo vyao hupata kazi fulani, kiasi fulani cha ulinzi, na mengine, lakini ni nini hasa wanachoifanyia nchi? Sisemi wasifanye kitu chochote, lakini ni nini wanachokifanya ambacho ni cha kipekee na kinachohusiana na ufalme ambacho mtu mwingine hawezi kukifanya ?" anasema Kirsten.

"Malikia Elizabeth ametawala kwa muda mrefu sana na amefanya hivyo kwa neema. Anaonekana kama mwanamke mzuri , lakini sioni haja kwa ufalme kwa sasa zaidi ya utalii, na watu wanaotaka kuja na kutazama kasri la Buckingham Palace wanaweza kwenda pale bado hata kama hakuna Ufalme ."

Malkia pamoja na familia yake ya karibu ni watumishi wa umma na hushiriki katika matukio rasmi zaidi ya 2,000 ndani na nje ya Uingereza kwa mwaka. Jukumu lao kuu ni kuboresha umoja na mshikamano wa kitaifa kupitia shughuli za umma na misaada ya kibinaadamu.

"Naiona Familia ya Kifalme kama watumishi waliopendelewa, ambao wamezaliwa kwenye kazi zao na hawawezi kuzibadili," anaeleza Sammy Knight.

Sammy ni mzaliwa wa Canada lakini kwa sasa ni raia wa Uingereza na anaamini Ufalme hauna nafasi kwa nchi hiyo pamoja na Jumuiya ya Madola.

"Namini Ufalme ni taasisi inayokufa na Malkia. Kusema Keli sisal kuhusu haji lake, lakini ni mwanamke shupavu. Nimeskitika kuona Philip amefariki kwa kuwa sasa amebaki peke yake.

"Navutiwa na utumishi wa Malkia na Mtawala wa Edinburgh - wamekuwa na Marsha yasiyo ya kawaida na nafikiri wamejitoa kadri ya uwezo wao kwa kazi za kijamii.

"Sivutiwi na vijana wa familia hiyo na nafikiri wakati umefika sasa kwa Uingereza kuwa na mkuu wa nchi anayepigiwa kura.

Wakati data za maoni zilipoainishwa kulingana na miaka ulionekana utofauti mkubwa baina ya vizazi . Wale wenye umri wa miaka kati ya 18 na 24 wana uwezekano mdogo wa kufikiria kuwa Uingereza inapaswa kuwa na ufalme, huku watu wenye umri wa zaidi ya miaka hiyo wakionekana kupendelea kwa kiasi kikubwa kuendelea kuwa na Familia ya Kifalme.

Pia kuna ukosefu wa uwiano katika matokeo ya kura ya maoni unapotazama katika maeneo tofauti ya Uingereza. Ni nusu tu ya watu wa Uskochi walioelezea mtazamo unaopendela hali ya baadae ya Ufalme , ikiwa ni sehemu ndogo zaidi ya uwiano katika kanda nyingine ya watu.

" Kama mtu wa uskochi binafsi nahisi ufalme ukiwa mbali zaidi na wa kigeni ," anasema Mathew Burton-Webster, muhudumu wa watoto na mkazi kutoka eneo la Kirkaldy lililoko kwenye mwambao wa mashariki wa Uskochi " Kitu kinachotufanya tukumbuke kuwa tunao hapa ni pesa zetu au mmoja wao anapofariki.

"Wanajipatia vyeo vya umiliki wa maeneo na mapumziko katika makazi ya kibinafsi hapa, lakini ni kama hawatoi chochote kurudisha mkono. Ni taasisi isiyo na maana ya Uingereza na utamaduni ambao haumnufaishi yeyote isipokuwa wenyewe ."

Sio kila mmoja anapendelea kukomeshwa kabisa kwa ufalme. Stephen Allison, mshauri mstaafu wa masuala ya kisiasa, badala yake angeangalia uwezekano wa kufanyika kwa baadhi ya mageuzi ya taasisi ya Ufalme.

"Kusema kweli utamaduni na muendelezo unaotolewa na wakuu wa ufalme lakini kuna wanafamilia wadogo wengi sana ," anasema. "Tunahitaji Malikia na Mwanamfalme wa Wales - Pia ningekuwa na Mwanamfalme William na Mwanamfalme George kwasababu ni warithi moja kwa moja wa Ufalme - lakini baada ya hapo hatuhitaji makumi ya Wanamfalme wa kike na wa kiume

"Kwahiyo, nadhani ninasema ninapenda wazo la baadhi ya watu wa Ufalme, lakini sio wote ."

Utawala wa Ufalme huongoza kwa idhidni ya watu nchini Uingereza, na katika miaka ya hivi karibuni ufalme wa Uingereza umekuwa ukijadiliwa.

Lakini kwa sasa, wale wanaotaka kuona mwisho wa Familia ya ufalme bado ni wachache.