Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ramadhan 2021: Kwanini Uganda imeanza kufunga kufunga leo, huku Tanzania ikianza Kesho
Hii leo, Waislamu nchini Uganda wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, huku katika mataifa jirani ya Tanzania na Kenya viongozi wake wa dini hiyo wakitangaza kuwa mwezi huo utaanza Jumatano. Lakini swali kwa wengi, Waislamu na hata wasiokuwa wafuasi wa dini hiyo ni kwa nini hali hiyo hutokea?
Tofauti ya kuanza mwezi wa Ramadhan pia ipo hata ndani ya Kenya na Tanzania. Japokuwa Mufti wa Tanzania Sheikh Zubeir bin Ally na Kadhi Mkuu wa Kenya Sheikh Ahmed Muhdhar kutangazia umma wa Waislamu katika chi hizo kwamba mwezi haukuandama na leo inafaa kuwa Shaaban 30, wapo baadhi ya Waislamu katika mataifa hayo ambao wameanza kufunga.
Wanazuoni kutofautiana
Kalenda ya Kiislamu inafuata muandamo wa mwezi, na hivyo tarere zake huwa baina ya siku 29 na 30. Ikifika tarehe 29 ya mwezi, watu huangalia kama mwezi umeandama, na kama tuko hilo limetokea basi kesho yake huwa ni mwezi mpya. Na endapo mwezi hautaonekana basi siku inayofuata huwa ni tarehe ya mwisho wa mwezi, yaani tarehe 30.
Mafundisho ya dini ya Kiislamu huwataka waumini wake wafunge kwa kuuona mwezi ama kuusikia. Tafsiri ya mafundisho hayo kwa wanazuoni wa kiislamu ndio inayosababisha kutofautiana kwa kuanza mwezi wa Ramadhan na kuumaliza.
Kuna ambao wanaamini katika kuuona wenyewe ama kuusikia katika maeneo ya jirani. Mathalan, nchi za Afrika Mashariki kwa miongo kadhaa zimekuwa zikipeana taarifa ya muandamo wa mwezi.
Hata hivyo kama ilivyo kwa mwaka huu, chi hizo hutofautiana pia. Mwaka 2019 Kenya ilitangaza kuonekana kwa mwezi na siku hiyo hiyo Tanzania ikatangaza mwezi haujaonekana.
Lakini kuna kundi la pili ambalo hufuata mwezi wa kimataifa, hawa hufunga ama kufungua endapo mwezi utathibiti shwa kuonekana popote pale duniani. Watu wanaofuata kundi hili ndio ambao leo wameanza kufunga kwa kuwa kuna nchi kadhaa walitangaza kuonekana kwa mwezi jana jioni.
Ramadhan ni nini?
Ramadhan ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislam, na unaaminiwa kuwa mwezi mtukufu zaidi na waumini wa dini ya Kiislam.
Kwa mujibu wa mafundisho ya Quran, Waislamu wanatakiwa kuanza kufunga kula na kunywa.
- Ramadhan ni moja ya nguzo tano kuu katika dini ya Kiislamu.
- Mwezi huo, Waislamu hujifunga kula na kunywa kuanzia macheo hadi machweo.
- Kufunga wakati huu huwawezesha Waislamu kujitolea zaidi katika dini na kumkaribia Allah.
- Kando na kufunga, ni wakati pia wa kutafakari kiroho, kuswali, kutenda matendo mema na kujumuika na familia na marafiki.
Waislamu hufanya juhudi za kipekee kuungana na wengine katika jamii na kuwasaidia wale wanaohitaji usaidizi katika jamii.
Huwa ni kawaida kwa Waislamu kula chakula asubuhi kabla ya mawio, suhur, na jioni wakati wa kufungua baada ya jua kutua, ambacho hufahamika kama iftar.
Mwisho wa kufunga, baada ya machweo, familia na marafiki hujumuika pamoja kufungua.
Wengi pia huenda Msikitini kuswali.
Ramadhan imekuwa mwezi huu kwa sababu ndio wakati Koran tukufu ilipofichuliwa kwa mara ya kwanza kwa Mtume Muhammad.
Ramadhan huwa ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu, lakini tarehe hiyo hubadilika kila mwaka.
Hii ni kwa sababu dini ya Kiislamu hufuata kalenda inayotumia mzunguko wa mwezi, hivyo hubadilika tofauti na kalenda inayotumiwa na mataifa ya Magharibi inayofuata jua.
Ni kila mtu hufunga?
Si kila Mwislamu hufunga wakati wa Ramadhan.
Watoto, wanawake waja wazito, wazee na wagonjwa au wanaosafiri wameruhusiwa kutofunga wakati wa mwezi huu mtukufu.
Watoto hutakiwa kuanza kufunga punde wanapobalehe, ambapo kawaida huwa ni wakiwa na miaka 14.
Mtu mzima anaweza kufidia siki ambazo hakufungwa wakati wowote katika mwaka au kulipa fidyah, ambapo mtu hutoa msaada wa chakula au pesa kwa kipindi ambacho hakufunga.
Mwisho wa mwezi wa ramadhan, ambao mwaka huu utakuwa 14 Juni, au karibu na hapo, huwa kuna maadhimisho ya siku tatu ya sikukuu ya Eid al-Fitr.