Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya Corona: Fahamu nchi zinazotumia chanjo ya Covid kuzidisha ushawishi kimataifa
Idadi ya watu waliofariki kote duniani kutokana na janga la corona ni kubwa sana: zaidi ya watu milioni 2.5 wamepoteza maisha, mamilioni ya wengine kuwachwa bila kazi, na mamilioni ya dola za utajiri zimeharibiwa.
Na ugonjwa huo haujakamilisha mkondo wake kwa njia yoyote; mamia kwa maelfu zaidi wapo hatarini.
Ugonjwa huo umezifanya nchi nyingi na kampuni mbali mbali kuanza kutafuta chanjo na baadhi ya zilizofaulu kutengeza chanjo hiyo sasa zimetumia hilo kuendeleza maslahi yazo ya kisiasa na kidiplomasia.
Miongoni mwa nchi hizo ni China, Urusi na Israel zinazoshtumiwa kutumia fursa ya kuwa na chanjo ya kutosha kuzidisha ushawishi wao katika ulingo wa kimataifa na kuafikia malengo mbali mbali ya kisiasa.
China na Tawain
Taiwan imeishtumu China kwa kutmia chanjo yake ya Corona ili kufanya Diplomasia kwa ili kuafikia malengo yake ya kisiasa baada ya Uchina kuitaka Paraguay kukatiza uhusiano wake na Tawain ili ipewe chanjo ya Corona kutoka China.
Waziri wa Mambo ya nje Joseph Wu alidai China imeahidi mamilioni ya dozi kwa Paraguay ambayo imeathiriwa sana na janga hilo.
Beijing inaiona Taiwan kuwa sehemu ya China na inasema inapaswa kuungana na China.
China imekanusha kutumia chanjo kujaribu kushawishi Paraguay kubadili msimamo wake kwani Paraguay ni moja tu ya nchi chache ambazo zinatambua eneo linalojitawala la Taiwan kama taifa huru.
Akizungumza Jumatano, Bw Wu aliilaumu China kwa "diplomasia ya chanjo".
"Serikali ya China ilikuwa na bidii kusema ikiwa serikali ya Paraguay iko tayari kukata uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan, wataweza kupata milioni chache za dozi za chanjo kutoka China," ameongeza.
Bwana Wu alisema Rais wa Paraguay Mario Abdo Benítez alikuwa ameshinikizwa na Taiwan ilikuwa imeuliza nchi nyingine kusaidia kupata chanjo kwa Paraguay. India inasema imetuma dozi 100,000.
Nchi hiyo pia imepokea dozi 36,000 kutoka AstraZeneca, dozi 4,000 za chanjo ya Sputnik V ya Urusi na 20,000 ya Sinovac ya Wachina.
Ni nchi 15 tu zinazotambua rasmi Taipei juu ya Beijing. Washirika kadhaa wako chini ya shinikizo kubadili uaminifu wao kwa Taiwan.
Israel na Palestina
Mnamo Desemba 19,2020 Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alipokea chanjo ya Pfizer-BioNTech COVID-19 kwenye hafla iliyopeperushwa kwenye runinga mubashara . Hii ilianzisha kampeni ya kitaifa ya chanjo ya hali ya juu ambayo imeshuhudia Waisraeli wengi wakichanjwa -kiwango cha juu zaidi ulimwenguni.
Sababu nyingi ziliifanya Israeli kuongoza katika mchakato wa utoaji wa chanjo hiyo.Kuwa nchi ndogo - Kwa eneo la ardhi na idadi ya watu - hakika ilisaidia.
Kuwa na mfumo wa kitaifa wa huduma ya afya ambao unahitaji raia wote kusajiliwa pia ulichangia. Kwa kuongezea, tofauti na nchi nyingine , serikali ya Israeli haikusita kuajiri jeshi kusaidia katika usimamizi na usambazaji wa chanjo hiyo.
Lakini kuna upande mbaya kwa "Mafanikio ya chanjo" ya Israeli: Ingawa inawapa chanjo raia wake dhidi ya COVID-19 kwa kiwango cha haraka, serikali ya Israeli haifanyi chochote kuwapa chanjo mamilioni ya Wapalestina wanaoishi chini ya utawala wake wa kijeshi.
Kinaya chenye ukatili ni kwamba mamia ya dozi zilizokaribia kuharibiaka zilitupwa katika kliniki za Israeli wakati fulani hapo nyuma wakati mamilioni ya Wapalestina wananyimwa chanjo hiyo.
Kwa kweli, wakati chanjo ikitolewa nchini Israeli ni pamoja na raia wa Palestina wa Israeli, haijumuishi Wapalestina milioni tano wanaoishi Ukingo wa Magharibi na Gaza.
Tangu mwaka wa 1967, maeneo haya mawili ya Wapalestina yamekuwa chini ya utawala wa jeshi la Israeli, na la mwisho pia limekuwa chini ya vikwazo vya kuingoa na kuomndoka eneo hilo tangu mwaka wa 2007.
Miongoni mwa mambo mengi, utawala wa Israel umekuwa na udhibiti kamili hatua ambayo inaathiri moja kwa moja uwezo wa Wapalestina kupata huduma za afya na hata ubora wa huduma hizo unaowafikia katika Ukingo wa Magharibi na Gaza.
Mamlaka ya Palestina (PA) bado haijapata chanjo ya kutosha kutoa chanjo kwa idadi ya Wapalestina dhidi ya COVID-19. Na kwa sababu ya hali yake mbaya ya kifedha, itahitaji msaada muhimu kutoka nje ili kufanya ununuzi wowote mkubwa.
Urusi
Tangu Urusi ilipolitwa eneo la Crimea mnamo 2014, Moscow imekuwa na shida ya uhusiano mwema nan chi za bara Ulaya.
Vikwazo vya Ulaya dhidi ya Urusi vilifuata na uhusiano kati ya Moscow na Brussels ulizorota wakati Vladimir Putin alipoonyesha ubabe wake Mashariki mwa Ulaya na Magharibi mwa Balkan, akiungana na viongozi kama Aleksander Vucic wa Serbia na Victor Orban wa Hungary.
Kutokana na uhusiano mbaya uliopo sasa , haishangazi kwamba harakati za kasi kuipata kwanza chanjo ya COVID-19 na kisha kuisambaza na kuisimamia imeingia kwenye mchakato mzima wa kila taoifa kutaka kuonyesha ushawishi wake .
Wakati EU ikijitahidi kutoa chanjo zinazotengenezwa na Ulaya, Urusi tayari imetuma chanjo yake ya Sputnik V kwenda Hungary na Slovakia na kujitolea kusambaza dozi milioni 50 zaidi kwa Ulaya na nchi nyingine hasa za Afrika
Mnamo Machi 9, ilitangaza kwamba Sputnik V itazalishwa nchini Italia kutoka Julai katika viwanda vya kampuni ya dawa ya Italia na Uswizi Adienne huko Lombardy. Dozi milioni kumi zitatolewa kati ya Julai 1 na Januari 1, 2022, kampuni hiyo ilithibitisha, pamoja na mamilioni kufanywa na kampuni za Korea Kusini, Brazil na India.
Licha ya hatua hizo , mataifa mengi ya Ulaya hayatanunua chanjo ya Urusi kwani haijakubaliwa na Wakala wa Dawa za Ulaya (EMA).
Hivi maajuzi EMA ilitangaza kwamba itaanza ukaguzi wa Sputnik V lakini siku chache baadaye mkuu wake, Christa Wirthumer-Hoche, aliwaambia waandishi wa habari wa Austria kwamba kuitumia ilikuwa "kulinganishwa na mazungumzo ya Urusi".
EMA haijajibu maswali juu ya maoni ya Wirthumer-Hoche na Euronews.
Wakati huo huo, ripoti katika The Lancet, jarida la matibabu la Uingereza , iligundua kiwango cha ufanisi wa 91% dhidi ya virusi, kitu ambacho kimetumiwa sana na vyombo vya habari vya Urusi ambavyo vinasema wazi kwamba Sputnik V ndio chanjo bora ya COVID-19 ulimwenguni. Kwenye akaunti rasmi ya Twitter ya Sputnik V, Moscow ilidai kuomba msamaha juu ya maoni ya Wirthumer-Hoche.
Sio mara ya kwanza kwa hatua ya Urusi kuhusu janga la COVID-19 kukosolewa huko Ulaya. Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen alisema kuwa Urusi ilikuwa ikitoa mamilioni ya dozi ulimwenguni wakati "haikuendelea vyema katika kuwapa watu wake chanjo."
Kwa kweli, wakati mamilioni ya chanjo ya Sputnik V yakipelekwa nje ya nchi kutoka Laos, Argentina hadi Serbia - na mamilioni mengine zaidi yaliyoahidiwa - matumizi nchini Urusi yamekuwa ya chini sana
Hatua hiyo imewafanya wengi kuchukualia hatua ya Urusi kama mojawapo ya njia zinazotumiwa na Kremlin kuzidisha ushawishi wake kisiasa na kidiplomasia katika nchi nyingine.
Wakosoaji pia wanashikilia kwamba wakati mengi yameahidiwa na Moscow, mengi bado yanapaswa kutolewa au kuidhinishwa. India, Nepali na Brazil - zilizoahidiwa kupokea dozi milioni 125, milioni 10 na milioni 25 mtawaliwa - bado hazina chanjo