Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanga wa matumaini: Picha za watoto walionusurika mzozo DR Congo
Mpiga picha Hugh Kinsella Cunningham amezuru maeneo tofauti ya mkoa wa Ituri kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiwa na shirika Kimataifa la watoto Save the Children, kuangazia taarifa za kibinafsi za watoto waliopatikana kwenye mizozo.
Histori aya hivi karibuni ya DR Congo imekuwa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na ufisadi, hali ambayo imesababisha mamia ya watu kupoteza maisha kutokana na sababu za moja kwa moja zilizotokana na mapigani aumagonjwa na ukosefu wa lishe bora.
Ghasia hizo zimechangia kuibuka kwa makundi kadhaa yaliyojihami ambayo yanakabiliana na mamlaka namara kwa mara yanawalenga raia.
Cunningham anatumia picha hizo kuwasilisha ujumbe wa matumaini kkupitia kazi yake. Kila picha ilipigwa bila kutumia mfumo wa kidijitali kuziboresha. Ametumia maua na vifaa vinavyopatikana ndani ya kambi wa wakimbizi wa ndani kwa ndani wakati wa upigaji picha.
Kila kitu kilibadilika kwa Veronique aliye na umri a miaka 12- wakati alipovamiwa na kundi la watu waliokuwa wamejihami kwa silaha walivamia kijiji chao, na kulazimu familia yake kukimbilia kambi ya wakimbizi wa ndani iliyo karibu.
"Tulipokuwa kijijini kwetu , tuliishi maisha ya kawaida. Wazazi wangu wangelifanya kazi katika mashamba yaliyo karibu na kutununulia nguo," anasema Veronique. "Lakini tangu tulipofika hapa mambo yalibadilika na maisha yamekuwa magumu."
"Nilataka kuendelea na masomo yangu,kwasababu nilikuwa katika mwaka wa nne, lakini sasa hilo haliwezekani, kutokana na ukosefu wa fedha ."
"Njiani niliona washambuliaji wakiua, wakichinja watu, kuwapiga risasi na kuiba nguo," anasema Emilie, 15.
Emilie na familia yake walifukuzwa na maaskari waliokuwa wamejihami lakini walifanikiwa kujificha katik amsitu uliokuwa karibu. Familia hiyo sasa inaishi katika kambi ya wakimbizi inayokaliwa na maelfu ya familia na watoto waliokimbi aghasia.
"Hapa hatuna chakula cha kutosha," anasema. "Nilipokuwa kijijini, tulipata chakula shambani sasa hakuna kitu ."
David, 12,alikuwa katika mwaka wa tano wa shule wakati walilipotoroka nyumbani kwao kufuatia ghasia.
"Tulipokuwa tunatoroka tulipata miili ya watu waliokufa njiani, ikiwa ni pamoja na ya baadhi ya marafiki zangu mbao waliuawa," anakumbuka.
Japo hali ya utulivu imerejea, analala katika mazingira ya baridi wakati wa usiku, na anaomba amani ipatikane iliwarudi nyumbani.
Upatikanaji wa maji, mazingira safi na lishe bora ni baadhi ya changamoto zinazowakabili watu wanaoishi katika kambi ya wakimbizi wa ndani. Huduma za afya pia ni haba.
Mradi wa Save the Children unalenga kuwapa huduma ya afya, lishe bora na ulinzi. Ushauri nasaha kwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono na dhulma za nyumbani na kwa watoto waliotenganishwa na wazazi wao.
Ijapokuwa sasa hakabiliwi na tisho la ukosefu wa usalama, Joseph, 14, anaishi na kumbukumbu ya ukatili alioshuhudia alipokuwa anatoroka makundi ya watu waliojihami.
"Ni kweli washambuliaji walikuja katika kijiji chetu, na kuwaua baadhi ya marafiki zangu na watoto wengine … Nawafikiria marafiki wangu wengine tuliowaacha nyuma."
"Sijatulia vyema hapa, lakini nahitaji kuwa hapa kwa usalama wangu," anasema Jonathan, aliye na umri wa miaka 13.
"Mwalimu [katika kambi] alinisajili kujiunga na shule na kunilletea vitabu vy akuandikia na sare zote. Nafurahia kusomabadala ya kukaa bure nyumbani. Hii ndio kitu ninachotaka.
"Nataka niishi hapa ili maisha yangu yawe mazuri siku za usoni," alisema.
Rachel, 17, alikuwa katika mwaka wake wa nne wa shule wakati makundi watu waliyojihami walipovamia kijiji chao.
Anakumbuka usiku aliotoroka kijijini kwao, anasema: "Niliona silaha za moto, vifaa moto, mapanga na mapanga. Washambuliaji waliwaua watu wote waliokuwa wakiwatafuta na kuchoma chumba zao..
"Kukiwa na vita kinachotokea ni mateso juu ya mateso… Sijui ni lini vita hivi vitaisha. Nataka amani kote Ituri, tumekuwa tukililia amani lakini haijawahi kupatikana."
Picha zote kwa hisani ya Hugh Kinsella Cunningham/Save the Children