Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chanjo ya AstraZeneca inasababisha hatari ya damu kuganda kwenye ubongo ?
Mabonge ya damu yasiyo ya kawaida kwenye ubongo yamegunduliwa kwa watu wachache baada ya kudungwa chanjo ya Oxford-AstraZeneca.
Hali hii ya kuganda kwa damu kwenye ubongo, kitaalamu "cerebral venous sinus thrombosis" au CVSTs zimesababisha nchi nyingine - zikiwemo Ujerumani, Ufaransa na Canada - kuzuia ni nani anaweza kupewa chanjo. Shirika la Afya duniani na Wakala wa Dawa wa Ulaya wanasema faida za chanjo hiyo huzidi hatari zozote.
Wanasayansi na wasimamizi wa usalama wa dawa ulimwenguni wanajaribu kujua ikiwa chanjo inasababisha athari hizi, ni hatari gani kubwa inaweza kuwa na inaweza kuwa na maana gani katika programu za chanjo.
Chanjo husababisha damu kuganda?
Kwa sasa, hatufahamu.
Wakala wa Dawa Ulaya (EMA), ambao wamekuwa wakipitia data za usalama, wanasema "hawajathibitisha, lakini inawezekana".
Shirika linapaswa kufahamu ikiwa kuganda kwa damu kulikokripotiwa ni athari ya baada ya chanjo au bahati mbaya ambayo ingeweza kutokea kawaida. Hii ni ngumu sana wakati wa kushughulika na masuala ambayo ni nadra kutokea . Ikiwa, kwa upande mwingine, mtu mmoja kati ya kila watu 10,000 ataripoti kutokea kwa hali ya kuganda damu basi jibu litakuwa dhahiri.
Nimezungumza na wanasayansi wanaoheshimika ambao wengine wana wasiwasi, wengine wanazidi kushawishika.
Hali isiyo ya kawaida ya kuganda damu huwa kama ishara ya kitu kinachoendelea. Mara nyingi huonekana wakati huo huo kukiwa na viwango vya chini vya chembe chembe za damu, ambazo ni moja wapo ya dalili kubwa na kingamwili zinazohusiana na shida nyingine za kuganda zinazoonekana kwenye damu.
Wengine wanasema hakuna ushahidi wa kutosha na kesi zilizoripotiwa zinaweza kuwa si sababu ya Covid, bali yenyewe inahusishwa na kuganda kusiko kwa kawaida.
Hatari inaweza kuwa kubwa kiasi gani?
Inabaki uwezekano kabisa kuwa hatari haipo kwani chanjo hazijathibitishwa kusababisha kuganda kwa damu kwenye ubongo.
Taasisi ya Paul Ehrlich ya Ujerumani imeripoti visa 31 na vifo tisa kati ya watu milioni 2.7 waliopewa chanjo huko.
Hatahivyo, data za hivi karibuni za Uingereza ziliripoti visa vitano tu, kati ya watu zaidi ya milioni 11 waliopewa chanjo.
Shirika la Dawa la Ulaya, ambalo limetathmini data kutoka kote ulimwenguni, linakadiria kuwa kuna hatari moja kati ya 100,000 ya CVST kwa watu walio chini ya umri wa miaka 60 ambao wamepewa chanjo ya AstraZeneca.
Mkuu wa ufuatiliaji wa usalama wa shirika hilo, Dk Peter Arlett, alisema hiyo ni "zaidi ya tunavyotarajia kuona".
Hatahivyo, haijulikani ni kweli kiasi gani kuhusu kiwango cha hali hii kujitokeza kwenye ubongo hapo kabla. Makadirio yanatofautiana kutoka kwa karibu kesi mbili kwa watu milioni kila mwaka hadi karibu 16 katika kila watu milioni kwa nyakati za janga la corona yenyewe inaweza kuwa inasababisha pia.
Chanjo ya AstraZeneca ni salama?
Hakuna usalama kwa asilimia mia moja katika dawa na hata tiba ambazo ni hatari hutumiwa katika mazingira yanayofaa.
Dawa za tiba ya mionzi zina athari mbaya, lakini zina thamani kubwa; na hata dawa za kutuliza maumivu kama paracetamol na ibuprofen zina athari mbaya, ni nadra sana.
Uamuzi huegemea kwa kutazama faida zinazozidi hatari.
Hii ni changamoto haswa katika janga la corona. Kawaida dawa inategemea "kanuni ya tahadhari" kuthibitisha usalama wa kutosha kabla ya kutoa dawa mpya kwa idadi kubwa ya watu. Lakini katika janga hilo, ucheleweshaji wowote wa chanjo ya watu pia utagharimu maisha.
Kulingana na data ya Ujerumani peke yake, ikiwa chanjo ya watu milioni moja basi unatarajia watu 12 watakuwa na tatizo la damu kuganda na wengine wanne watakufa.
Lakini ikiwa watu milioni wenye umri wa miaka 60 watapata virusibasi karibu 20,000 watakufa na Covid-19. Ikiwa watoto milioni 40 wa miaka wanapata virusi hivyo basi karibu 1,000 hufa. Ingekuwa watu mia chache katika miaka yao ya 30.
Faida za chanjo huongezeka kwa kutegemea umri na nchi kama Ujerumani na Canada zimeruhusu chanjo ya AstraZeneca kutumika katika vikundi vya wazee. Uamuzi huu pia utasababishwa na chanjo mbadala ambazo zinapatikana na ni nani bado anahitaji kupatiwa chanjo.
Ulimwengu unachunguza data kwa nguvu, lakini majibu yatachukua muda.