Wafalme wa kiarabu wanaowinda ndege kuongeza nguvu za kiume

Iliyochapishwa

Mwaka 1983, wanajeshi wawili walisimama eneo fulani wakitaka kukodisha gari katika mji wa Pasni kusini mashariki mwa pwani ya Pakistan.

Mmoja wao akamuuliza mwenyewe: "Una gari ambalo ni salama? Tunaenda kumchukua mwanamume tajiri wa kiarabu tumpeleke Panjpur."

Mwenyewe akasema anayo na akawaunganisha na kijana wake Hanif ili aweze kuwaonesha gari.

Na gari hiyo ikakodishwa kwa ajili ya Mwanamfalme Suroor bin Mohammed al-Nahyan, mmoja wa vijana sita wa nchi ya Flame za Kiarabu (UAE).

Anataka kwenda Panjpur, umbali wa kilomita 100 kuwinda.

Sheikh alipenda gari lile, na kuichukua kutoka kwa Hanif, wakati huo akiwa na umri wa miaka 31.

Na hapo ndipo walipoanza kuwa na uhusiano ambao umedumu kwa muda mrefu, amesema Haji Hanif kama anavyofahamika sasa hivi.

Miaka 37 baadaye, amekuwa mwenyeji anayewatunza watu wa familia ya kifalme wanaosafiri hadi nchini mwake Pakistan kila mwaka kuwinda.

Ndege hao ambao wana ukubwa wa bata mzinga wanaendelea kupungua kwa hiyo kuwaua ni hatua ambayo itakuletea utata lakini bado wanawindwa kwa ajili ya michezo.

Ndege aina ya kulungu wanakaribia kuwindwa.

Hata hivyo watu wa ngazi ya juu wa Pakistan wamekuwa wakiunga mkono uwindaji huo kwa misingi ya kuendeleza uhusiano mwema na wenye ushawishi katika mataifa tajiri ya ghuba.

Wale ambao wanaunga mkono ziara hizo zinazofanywa na familia za kifalme wanasema zinatengeneza ajira na uwekezaji.

Lakini hakuna uhakika hasa wa kile ambacho Pakistan inafaidika kutokana na utamaduni huo. Wengine ambao wamekuwa wakishuhudia utamaduni huo wa uwindaji wanasema familia za Kifalme wanatumia ziara hizo kujipumzisha na kujifurahisha.

Novemba na Februari kila mwaka, Haji Hanif huwa anakuwa mwenyeji wa familia za kifalme wawindaji huko Balochistan, umbali wa saa moja kwa gari kutoka eneo la pwani mji wa Gwadar.

Na kabla ya kukamilika kwa kipindi cha msimu wa baridi wakati wa uwindaji, alialika BBC kuona jinsi yeye na wafanyakazi wake walivyojitayarisha kupokea familia za kifalme.

Mahali anapokuwa na wageni wake ni eneo la Pasni, ambako badio wenyeji kupata mahitaji yao ya msingi ni kama ndoto.

Tunakutana na wanaume wawili ambao walitutembeza katika nyumba ya kifahari ya Hanif, kilomita chache tu kutoka uwanja wa ndege.

Gari ya wanaume hao aina ya Jeep lilikuwa limesajiliwa kwa nambari ya United Arab Emirates, na kufanya tujione kana kwamba tuko katika sehemu ndogo ya Abu Dhabi.

Hisia hizo ziliimarishwa na nembo kubwa ya kifalme ya Abu Dhabi, yenye nembo ya tai tuliyoiona punde baada ya kuingia nyumbani kwake.

Familia za kifalme zzilizokuwa zinatembelea zilitoa ajira kwa raia wengi. Wakati tunawasili, tuliona watu wakiendelea na shughuli zao wengine wakitengeneza jiko, wakirekebisha magari, huku wengine wakiweka magari makubwa aina ya SUVs katika gereji.

Mwanamume aliyevaa nguo za kifalme alituongoza katika chumba cha wageni, ambako tulikaribishwa kwa harufu nzuri inayonukia.

"Eneo letu minalionaje?" Haji Hanif aliyekuwa ameketi katika moja ya sofa akauliza.

Haji Hanif, ambaye sasa hivi ana umri wa miaka 60, wakati anawaonesha maeneo mbalimbali alizungumzia ziara ya Sheikh kwa miaka mingi.

"Baada ya kumtafutia gari, alirejea kwetu tena. Kufikia mwaka 1988, baba yangu na mimi tulikuwa tunasimamia magari 20 ya familia ya kifalme kwasababu walituamini."

Kwa wakazi wa Pasni, ziara za familia za kifalme zimekuwa chanzo cha riziki kwa wenyeji 35 ambao waliajiriwa miezi mitatu kabla ya familia za kifalme kufika.

Pia kuna wanaume ambao hutunza mwewe, vipanda na njiwa kuwasadia kuwapa mafunzo.

Pia kuna wanaume watatu wanaofanyakazi katika mashamba ambako kuna malimau yanayokuzwa kwa ajili ya sheikh, kuna anayetunza simba wanaofugwa huku mwingine kazi yake ikiwa ni kufua.

Wengine walikuwa wanasimamia kupika na kufanya usafi pamoja na pia kuna wanaorekebisha magari yanapokuwa na matatizo.

Mwendeshaji pikipiki analipwa kuja kuangalia ndege wako wapi ili familia ya kifalme isihitajike kusafiri mwendo mrefu wakati wa kuwinda.

Watoto watatu wa Haji Hanif pia wameajiriwa kumsaidia baba yao.

Kijana wake mkubwa anasimamia magari 20 aina ya SUVs yaliyopo kwa ajili ya familia ya Kifalme, kijana wake wa pili mlinzi wake anayesimamia usalama huku wa tatu akihakikisha kuwa ndege hawawindwi kwa njia isio halali kupitia soko haramu.

Kwanza, Pakistan ilikaribisha wawindaji wa familia za kifalme mwaka 1973. Tangu wakati huo makundi ya familia za Kiarabu yamekuwa yakitembelea eneo la houbara kusini mashariki mwa Balochistan wakati wa msimu wa baridi.

Kufikia mwaka 1989 serikali za eneo zikaungwa mkono na serikali kuu ya Islamabad, na kufanya ziara hizo kuwa rasmi kwa kutenga maeneo mbalimbali kwa ajili ya uwindaji wa familia za kifalme tofauti tofauti.

Ufalme wa Abu Dhabi umepewa maeneo ya kuwinda huko Pasni, Panjgur na Gwadar. Huku Ufalme wa Qatar ukipewa eneo lake huko Jhal wilaya ya Awaran mashariki mwa pwani.

Ufalme wa Saudi Arabia ukipewa eneo la Chaghi huko kaskazini. Familia kama ya Haji Hanif, ambao wanaaminiwa na familia ya Kifalme, ndio waliopewa majukumu ya kusimamia ardhi zao tangu enzi na enzi.

Miaka ya 1970, wawindaji kutoka sehemu mbalimbali za Uarabuni duniani waliweka kwenye kambi kila ndege walipokuwa.

Wawindaji wangekaa huko katika kipindi cha wiki moja, na wanafamilia wangepika na kula ndege kabla ya kurejea mjini.

Lakini hofu ya usalama magharibi huko Balochistan, ambapo wapiganaji wa jihadi walianzisha mashambilizi miaka ya hivi karibuni, ikafanya kambi hizo za misituni kuwa hatari kufikiwa.

Na siku hizi wasimamizi wengi wanaishi katika mahoteli ya kifahari, majumba ya kifahari kama vile Haji Hanif.

Na hakuna tena zile safari za muda mrefu hadi msituni kuwinda.

Kiutamaduni, uwindaji wa ndege wenye manyoya ambayo thamani yake ni juu mno - shingo ya ndege inakatwa kwa kisu punde tu anaposhikwa.

Ndege pia wanawindwa. Lakini wakati huo huo, walanguzi na watunzaji huachia ndege kwasababu mwewe huwakamata pale tu wawindaji wanapokuwa karibu.

Alikuwa na furaha kupita kiasi sio tu kwasababu ya ajira zinazopatikana lakini pia familia za kifalme zinajenga visima, mashule na hospitali. Tatizo kwa shule ni ukosefu wa walimu na wahudumu wa afya kwa mahospitali.

Hata hivyo, Haji Hanif hataki mtoto wake hata mmoja rithi kazi yake.

"Mimi ni mtumwa wa familia za kifalme, lakini sitarajii watoto wangu warithi kazi yangu. Wao watafanya wanachotaka, biashara zao na kutafuta suluhu zao kwa changamoto watakazokumbana nazo maishani.