Virusi vya Corona : Viongozi wa dunia wataka pawepo mkataba wa kimataifa wa kukabiliana na majanga

Iliyochapishwa

Waziri Mkuu Boris Johnson amejiunga na zaidi ya viongozi 20 wa ulimwengu wanaotoa wito wa kuwepo makubaliano ya kusaidia ulimwengu kujiandaa kwa milipuko ya magonjwa siku za baadaye

Katika nakala ya gazeti viongozi hao, pamoja na kansela wa Ujerumani na rais wa Ufaransa, walisema Covid ni changamoto kubwa zaidi tangu Vita vya pili vya dunia

Janga hilo limeonyesha "hakuna mtu aliye salama hadi kila mtu awe salama", walisema.

Katibu wa Biashara Kwasi Kwarteng alisema Uingereza inahitaji kuwa na chanjo ya ziada kabla ya kusafirisha nyingine kuzisaidia nchi zinazohitaji chanjo hiyo .

Wakiandika katika Daily Telegraph na majarida mengine kama Le Monde huko Ufaransa na El Pais huko Uhispania, viongozi hao 24 wanasema kwamba mkataba sawa na ule uliofikiwa baada ya Vita vya pili vya dunia unahitajika ili kujenga ushirikiano baina ya nchi mbali mbali .

Waliotia saini, ambao ni pamoja na mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, alisema: "Wakati huo, kufuatia uharibifu wa vita viwili vya ulimwengu, viongozi wa kisiasa walikusanyika kuunda mfumo wa pande nyingi.

"Malengo yalikuwa wazi: Kuleta nchi pamoja, kuondoa vishawishi vya kujitenga na utaifa, na kushughulikia changamoto ambazo zinaweza kupatikana tu pamoja kwa roho ya mshikamano na ushirikiano - ambayo ni amani, ustawi, afya na usalama. "

Viongozi walisema kwamba kwa roho hiyo hiyo, nchi lazima sasa "ziwe tayari zaidi kutabiri, kuzuia, kugundua, kutathmini na kukabiliana vyema na milipuko ya magonjwa kwa mtindo ulioratibiwa sana".

Mkataba mpya utasaidia kuanzisha mifumo bora ya kuwatahadharisha watu juu ya milipuko ya magonjwa walisema, na pia kuboresha ushirikiano katika kutoa data na usambazaji wa chanjo na vifaa vya kinga binafsi.

"Kutakuwa na magonjwa mengine ya kuambukiza na dharura zingine kuu za kiafya. Hakuna serikali moja au wakala anayeweza kushughulikia tishio hili peke yake. Swali sio ikiwa, lakini lini.

"Janga la Covid-19 limekuwa ukumbusho mkali na mchungu kwamba hakuna mtu aliye salama mpaka kila mtu awe salama."

Barua hiyo iliongeza: "Wakati ambapo Covid-19 imetumia udhaifu wetu na mgawanyiko, lazima tuchukue fursa hii na tuje pamoja kama jamii ya ulimwengu kwa ushirikiano wa amani ambao utadumu hata baada ya mgogoro huu."

Dr David Nabarro, mjumbe maalum wa Covid-19 kwa WHO, aliambia kipindi Today cha BBC Radio 4 kwamba bila "aina ya hatua maalum, ulimwengu kwa jumla hautapewa chanjo hadi 2022".

"Wakati huo kila aina ya shida na na changamoto zitatokea, na kwa hivyo viongozi wote wanasema ni" shida hii ni kubwa sana lazima tushirikiane kukabiliana nayo ", ameongeza.

Bw Kwarteng alikimbia kipindi hicho kwamba kufanya chanjo kupatikana kwa nchi nyingine "kunaweza kutokea mara tu tutakapokuwa na chanjo ya ziada hapa Uingereza".

"Bado kuna njia nyingine. Lazima tuhakikishe tunafanya kila kitu tunachoweza kukabiliana na janga na virusi vya korona katika nchi hii," alisema.

"Lakini ni wazi tunataka kufanya kazi katika roho ya ushirikiano pia, na wakati tunayo ziada tutakuwa tukitafuta kusafirisha hizo, nina hakika."

Nakala hiyo ya pamoja inakuja baada ya tofauti kati ya Uingereza na EU juu ya chanjo, baada ya muungano huo kuanzisha udhibiti mkali zaidi wa usafirishaji wa nje juu ya juu ya chanjo zinazozalishwa katika muungano wenyewe.

Uingereza na Shirika la Afya Ulimwenguni walionya juu ya vizuizi, wakati EU ililaumu kampuni za dawa - haswa AstraZeneca - kwa kutotoa dozi zilizoahidiwa.

AstraZeneca imekanusha kuwa inashindwa kuheshimu mkataba wake.

Kwenye mkutano wa Downing Street Jumatatu, Bwana Johnson alitangaza kwamba makumi ya mamilioni ya dozi za chanjo ya Novavax sasa yatazalishwa na kupakiwa kaskazini mashariki mwa England.

Waziri mkuu alisema makubaliano yameafikiwa na GlaxoSmithKline kuweka chupa za dozi milioni 60 katika kituo chake huko Barnard Castle.

Mpango wa awali ulikuwa wa mchakato wa "kujaza na kumaliza" - ambayo chanjo huwekwa kwenye vichupa maalum huko Ulaya.

Novavax inachunguzwa sasa na Mamlaka ya Udhibiti wa bidhaa za dawa na Afya.

Pia katika mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Uingereza haikujua "haswa nguvu" za ulinzi wake dhidi ya wimbi lingine la Covid itakuaje licha ya chanjo yake "yenye ufanisi".

Alikuwa akiongea wakati kanuni ya kukaa nyumbani ikimalizika England, ikiruhusu vikundi kukutana nje. Sehemu za michezo ya nje, pamoja na mabwawa ya kuogelea, korti za tenisi na kozi za gofu, zimefunguliwa tena, wakati harusi pia zikiruhisiwa.

Bwana Johnson alionya vifo zaidi, maambukizo na kulazwa hospitalini ni jambo ambalo halitaepukika wakati Uingereza inapotoka kwenye zuio la kutotoka nje