Meli iliyokuwa imekwama katika mfereji wa Suez yaanza tena kuelea

Iliyochapishwa

Meli kubwa iliyokuwa imekwamba katika mfereji wa Suez tangu Jumanne wiki iliyopita imefanikiwa kuelea tena majini.

Video iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii Jumatatu. Meli hiyo imeonekana ikielekea kwenye kingo za mfereji na kufungua njia. Kampuni ya huduma za majini ya Inchcape pia imeripoti kuwa meli hiyo imefanikiwa kuanza kuelea tena.

Kufanikiwa kuelea tena kwa meli hiyo kumetokana na juhudi nyingi zilizojumuisha meli zingine na mashine za kuchina bandari.

Mfereji wa Suez ambao unapita Misri ni moja ya njia yenye shughuli nyingi za kibiashara.

Kukwama kwa meli hiyo - kulisababisha meli zingine kufuata njia nyingine ndefu Afrika.

Baada ya siku kadhaa za juhudi za kuondoa meli hiyo kukwamba, Jumapili maafisa walianza kuondoa kontena karibu 20,000 zilizokuwa ndani ya meli hiyo ili kuipunguzia mzigo.

Awali, Wataalam walizungumza na BBC na kusema operesheni ya kuhakikisha meli inaelea tena ingejumuisha vifaa maalum ikiwemo kreni ambayo ingehitajika kujinyoosha zaidi ya mita 60 na hilo lingechukua wiki kadhaa.

Meli hiyo yenye urefu wa mita 400, iliyokuwa na uzito wa tani 200,000 ilikwamba Jumanne asubuhi kwasababu ya mawimbi makali na thoruba iliyoathiri uonekanaji.

Kampuni zenye utaalamu wa kushughulikia hilo zilitafutwa ili kusadia meli hiyo kuelea tena.

Takriban asilimia 12 ya biashara duniani zinazotumia njia ya meli hutumia mfereji wa Suez ambao unaunganisha Bahari ya Mediteranea hadi Bahari ya Shamu na ndio yenye njia fupi zaidi kati ya Asia na Ulaya.

Njia nyingine inayopita Afrika inaweza kuchukua wiki mbili zaidi.

Awali, boti za kuvuta na wachimbaji wanafanya kazi ya kuisaidia meli kubwa ya kontena kuelea tena majini baada ya meli hiyo kuziba mfereji wa maji wa Suez nchini Misri, moja wapo ya njia zenye shughuli za biashara ulimwenguni.

Misri ilisema kuwa imefungua njia ya zamani kugeuza mkondo wa meli zingine ili kuzuia msongamano wa majini huku baadhi ya meli zikikosa njia ya kupita.

Meli ya Ever Given ni ya aina gani?

Meli ya Ever Given iliyokwama katika mfereji wa Suez inazuia bidhaa za thamani ya karibu dola bilioni 9.6 kila siku (£7bn), kwa mujibu takwimu za uafirishaji.

Hii inachangia dola milioni 400 kwa saa katika biashara ya majini ambayo ni njia muhimu ya usafirishaji kati ya mashariki na magharibi.

Licha ya kuendelea kwa juhudi za kuivuta meli hiyo, huenda ikachukua wiki kadhaa kuirudisha kwenye mkondo, wataalamu wanasema

Meli ya Ever Given, iliendeshwa na kampuni ya Taiwan ya Evergreen Marine ina urefu wa ukubwa wa viwanja vinne vya soka, ni moja ya meli kubwa ya mizigo duniani.

Meli hiyo pia inauzani wa tani 200,000- na ina uwezo wa kubeba makonteni 20,000.

Kukwama kwa meli hiyo kulisababisha msongamano wa meli zingine zinazojaribu kupitia mfereji wa Suez.

Mfereji huo, ambao unatenganisha Afrika, mashariki ya kati na Asia, ni moja ya njia ya biashara iliyo na shughuli nyingi duniani, ikiwa na asilimia 12 ya biashara inayopitia hapo.

Kulingana na data ya Lloyd ya usafiri wa meli 160 zinasubiri kupitia njia hiyo au kukamilisha safari.

Hii ikiwa ni pamoja na meli zingine pamoja na meli 41 zingine za mizigo na 24 za mafuta.

Bidhaa zilizokwama baharini kufuatia tukio hilo ni mafuta na bidhaa za nyumbani kama vile, samani, na vipuri vya magari.