Kufungwa kwa mfereji wa Suez kunazuia mizigo yenye thamani ya dola bilioni 9.6 kwa siku

Chanzo cha picha, Getty Images
Meli ya Ever Given iliyokwama katika mfereji wa Suez inazuia bidhaa za thamani ya karibu dola bilioni 9.6 kila siku (£7bn), kwa mujibu takwimu za uafirishaji.
Hii inachangia dola milioni 400 kwa saa katika biashara ya majini ambayo ni njia muhimu ya usafirishaji kati ya mashariki na magharibi.
Licha ya kuendelea kwa juhudi za kuivuta meli hiyo, huenda ikachukua wiki kadhaa kuirudisha kwenye mkondo, wataalamu wanasema
Meli ya Ever Given, iliendeshwa na kampuni ya Taiwan ya Evergreen Marine ina urefu wa ukubwa wa viwanja vinne vya soka, ni moja ya meli kubwa ya mizigo duniani.
Meli hiyo pia inauzani wa tani 200,000- na ina uwezo wa kubeba makonteni 20,000.
Kukwama kwa meli hiyo imesababisha msongamano wa meli zingine zinazojaribu kupitia mfereji wa Suez.
Mfereji huo, ambao unatenganisha Afrika, mashariki ya kati na Asia,ni moja ya njia ya biashara iliyo na shughuli nyingi duniani, ikiwa na asilimia 12 ya biashara inayopitia hapo.
Kulingana na data ya Lloyd ya usafiri wa meli 160 zinasubiri kupitia njia hiyo au kukamilisha safari.
Hii ikiwa ni pamoja na meli zingine pamoja na meli 41 zingine za mizigo na 24 za mafuta.
Bidhaa zilizokwama baharini kufuatia tukio hilo ni mafuta na bidhaa za nyumbani kama vile, samani, na vipuri vya magari.

Chanzo cha picha, © Cnes2021, Distribution Airbus DS
"Sasa tunasikia ripoti kwamba kampuni za usafirishaji zinaanza kugeuza meli zao kuzunguka ncha ya kusini mwa Afrika, Cape of Good Hope,ambayo inaongeza karibu maili 3,500 kwa safari na hadi siku 12," Guy Platten, katibu mkuu wa Jumuiya ya Usafirishaji ya Kimataifa, aliiambia kipindi cha BBC cha Leo.

Chanzo cha picha, Suez Canal Authority
Alisema meli hiyo inaonekana "imekwama katika eneo gumu", akiongeza kuwa shughuli ya kuiondoa meli khiyo katika kongozi na mfereji huo huenda ikachukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa awali.
Bw. Platten aid amesema "kutashuhudiwa athari kubwa za usambazaji wa bidhaa duniani", akiongezea kuwa watumiaji wa bidhaa hizo huenda wasiwe na budi kugharamia hasara.
Meli za mizigo zimeongezeka kwa karibu mara mbili katika miongo kadhaa iliyopita baada ya kuongezeka kwa biashara ya kimataifa, hali ambayo imekuwa vigumu kuziondoa zinapokwama.
"Tunafikiria nini? Je meli zimekuwa kubwa zaidi? Mizigo ndani ya meli hiyo ni mikubwa na imekuwa vigumu kuirudisha kwa mkondo, hali iliyosababisha msongamano ikiwa ni pamoja foleni kubwa katika bandari tofauti," alisema Jon Monroe, ambaye anaendesha kampuni inayotoa huduma za usafirishaji .
Chama cha kimataifa cha usafirishaji wa majini BIMCO, kinasema shughuli za usafiri wa meli zitaendelea kuchelewa na kuathiri usabazaji wa bidhaa.
"Kwa kila siku ambayo safari zinacheleweshwa itachukua siku mbili kurejelea hali ya kawaida," alisema Alan Baer, rais wa shirk la Marekani la OL linaloshughulikia masuala ya miundo mbinu ya usafiri.













