Kifo cha mflame wa Wazulu Goodwill Zwelithin: Malkia achaguliwa kushikilia wadhifa kwa muda

Queen Mantfombi MaDlamini Zulu pictured in about 1973 when she was a princess of Swaziland, now known as Eswatini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malkia alipopigwa picha miaka ya 1970 kabla ya kuolewa
Iliyochapishwa

Familia ya kiflame ya Zulu nchini Afrika Kusini imemteua mke wa tatu wa Mfalme Goodwill Zwelithini kushikilia nafasi yake hadi pale mfalme mpya atakapotawazwa.

Malkia Mantfombi MaDlamini Zulu ameshikilia wadhifa wa "Mke Mkuu" tangu alipoolewa na mfalme mwaka 1977.

Uteuzi wake umeibua mjadala kwamba mmoja wa wanawe wa kiume atakuwa mfalme wa Wazulu milioni 11.

Zwelithini, 72, alikuwa akiugua maradhi ya kisukari na alifariki hospitalini kutokana na changamoto za kiafya zilizochochewa na ugonjwa wa corona tarehe 12 mwezi Machi.

Alikuwa mfalme wa Wazulu aliyehudumu kwa karibu miaka 50.

Alikuwa na wake sita na watoto 26.

Uteuzi wa Malkia MaDlamini katika uongozi wa Wazulu ulitangazwa kufuatia mkutano kati ya mawakili wa Zwelithini na wanachama karibu 200 kutoka familia ya kifalme kujadili wasia wake.

The King"s wives grieve during the memorial for the late Zulu monarch, King Goodwill Zwelithini at the KwaKhethomthandayo Royal Palace in Nongoma, South Africa, 18 March 2021.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wake watatu wa Malkia walivyoonekana katika ibada maalum wiki jana

Waziri Mkuu wa kitamaduni wa marehemu Mfalme Mangosuthu Buthelezi, amesema uteuzi wake uliendana na matamanio ya Zwelithini.

Familia ya kifalme itaomboleza kwa kipindi cha miezi mitatu na uamuzi zaidi kuhusu mrithi wa mfalme utafikiwa baadae, Mkuu Buthelezi alisema.

"Kifo cha Mfalme wetu mpendwa, ni pigo kubwa, na familia lazima ipewe muda wa kuomboleza," aliongeza kusema.

Zulu King Goodwill Zwelithini ka Bhekuzulu (L) and senior Prince of the Zulu Nation and former leader of the Inkatha Freedom Party ( IFP ) Prince Mangosuthu Buthelezi (R) join thousands of people to commemorate King Shaka's Day Celebration near the grave of the great Zulu King Shaka at Kwadukuza, some 98 kilometres north of Durban, on September 24, 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mfalme Buthelezi (kulia) alikuwa mjomba wa Mfalme Zwelithini (kushoto).

Zwelithini alizikwa - au kupandwa kama wanavyosema Wazulu - siku ya Alhamisi katika hafla ya mazishi ya faragha iliyohuduhuriwa na wanaume wachache walioteuliwa kutoka familia ya kifalme.

Tunafahamu nine zaidi kuhusu kiongozi wa sasa?

Malkia MaDlamini Zulu anashikilia hadhi ya juu miongoni mwa wake wa mfalme kwa sababu anatoka familia ya kifalme.

Ni dada yake Mfamle wa Eswatini Mswati wa III - Mfalme pekee wa Afrika.

Malkia MaDlamini Zulu alikuwa na watoto wanane -miongoni mwao wavulana watano- aliozaa na marehemu mfalme, kulingana na vyombo vya habari vya Afrika Kusini.

Mwana wao mkubwa wa kiume, aliye na umri wa miaka 47- Mwanamfalme Misuzulu, anapigiwa upatu kumrithi baba yake, ripoti zinasema.