Mlipuko mpya wa virusi vya Corona waripotiwa katika mji wa kusini magharibi mwa China

Dkt. Lisa Federle alianza kupima watu katika nyumba za kutunza wazee mji wa Tübingen, Ujerumani, Aprili

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dkt. Lisa Federle alianza kupima watu katika nyumba za kutunza wazee mji wa Tübingen, Ujerumani, Aprili
Iliyochapishwa

Kwa mara ya kwanza kwa karibu miezi miwili, China imeripoti visa vingi vya maambukizi mapya ya Covid-19 - wakati huu kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Watu tisa wamepatikana kuwa na Covid-19 katika jiji la Ruili, mkoa wa Yunnan. Sita wana dalili na watatu hawana dalili.Wagonjwa wanne ni raia wa Burma na watano ni Wachina. Wagonjwa wote wana umri wa miaka 22 hadi 42 na wana dalili chache .Kampeini ya kuwapima watu wengi imezinduliwa, na watu 317 waliokaribiana na walioathiriwa wamewekwa katika karantini. Raia wa Ruili wanaambiwa wabaki nyumbani, na biashara zote isipokuwa maduka makubwa, masoko ya wakulima na maduka ya dawa yamefungwa.Huduma za usafiri zimeanza kudhibitiwa na watu hawaruhusiwi kuondoka jijini bila kuonyesha cheti cha kuonyesha kwamba wamepimwa na kupatikana bila virusi hivyo .Uchina imebaki bila visa vya Covid tangu mapema Februari. Mlipuko wake mkubwa wa mwisho ulitokea kaskazini mashariki mwa nchi mwanzoni mwa mwaka.Hii si mara ya kwanza kwa Ruili, jiji lenye wakazi wapatao 210,000 kupata mlipuko. Mnamo Septemba, mlipuko katika jiji hilo ulihusishwa na mwanamke wa Burma ambaye alikuwa amevuka mpaka muda mfupi kabla .

Serikali ya mtaa imesema leo "itakabiliana vikali na vivuko vya mipaka visivyo halali" wakati wa mlipuko mpya. Raia wa eneo hilo wameliambia gazeti la Global Times kumekuwa na uvumi hivi karibuni katika jiji hilo kwamba watu walikuwa wakisafirishwa kutoka Myanmar, na kuleta virusi hivyo.

Ramani

Tangu kuanza kwa janga la Corona mwishoni mwa mwaka wa 2019 nchi nyingi zimekuwa zikitumia mikakati mbali mbali kupambana na virusi hivyo. Baadhi ya mikakati hiyo imesaidia kupunguza visa vya maambukizi na hata maafa ilhali kuna mingine ambayo haijafanya kazi.

Línea

Hata hivyo kuna baadhi ya hatua zilizochukulia na mataifa ambayo yamefaulu kuzuia usambaaji na maambukizi ya virusi hivyo na sasa hatua hizo zinaunda msingi wa kufaulu katika vita dhidi ya Covid-19.

Hatua hizo za kuzuia maambukizi na maafa kutokana na virusi hivyo ni pamoja na;

  • Kuchukua hatua za haraka na za mapema kudhibiti kuingia kwa wageni mipakani na katika viwanja vya ndege.
  • Kuwapima kuwafuatilia na kuchunguza hali za kiafya za wanaoshukiwa kuwa na virusi hivyo.
  • Usaidizi wa kijamii kwa waliowekwa karantini ili kudhibiti virusi hivyo.
  • Uongozi mwafaka na utoaji wa habari muhimu kwa wakati ufaao kwa umma.

Hakuna mtu anayeweza kudai kuwa amefanya kila kitu sawa. Lakini hatua zilizoorodheshwa hapa chini zinaonyesha sera kote ulimwenguni ambazo zimethibitishwa kuwa nzuri.

Kuziweka pamoja, tuna muhtasari wa "kijitabu chenye kanuni za kukabiliana na majanga" - mwongozo wa kudhibiti milipuko ya magonjwa ya kuambukiza hata katika siku za baadaye.

Hatua ya 1: Matayarisho

Stanley Park anaishi Seoul, Korea Kusini. Alipokwenda uwanja wa ndege kumchukua binti yake, Joo Yeon, hakumsalimia kwa kumkumbatia bali alikuwa amevalia maski na chupa ya sanitaiza mkononi.

Kwa Stanley, hii sio mara yake ya kwanza kujipata katika hali kama hii. Kumbuka uharibifu na hofu ambayo mlipuko wa Mers ulileta Kusini Mashariki mwa Asia mnamo 2015.

Ni matayarisho ambayo nchi inajifunza. Serikali ilifanya mageuzi 48 ili kuimarisha kujitayarisha kwake na jinsi ya kukabiliana na hali ya dharura za kiafya ya umma. Na juhudi hizo zimefua dafu.

Wakati janga la virusi vya corona lilipoibuka, maafisa waliweza kupunguza idadi ya maambukizi haraka, bila kutekeleza vizuizi vikali kote nchini.

Baada ya kuwasili kutoka Atlanta, Joo Yeon alikamilisha karantini ya wiki mbili nyumbani kwa wazazi wake, akapakua programu inayofuatilia hali yake ya kiafya na alipokea simu sita za kujua hali yake kutoka kwa mamlaka. Alichukua karantini yake kwa umakini sana kwamba "hata hakuenda bustani'

"Tangu mwanzo, tulitekeleza hatua kamili za kuzuia kitu hicho kutokea tena - historia inajirudia," Waziri Mkuu Chung Sye-kyun alisema.

Hatua ya 2: Kupima, Kusaka na kujua waliko

"Ni changamoto kubwa kwa sasa, sijui kama wagonjwa ninaowaona wana virusi vya corona au la," David Hodges, daktari kutoka Kaskazini Mashariki mwa England, aliiambia Panorama mnamo Machi 2020. "Tunaweza kuwa na mamia ya kesi ambazo hazijasajiliwa."

Nchi nyingi za Asia Mashariki zilianza kufuatilia visa hivi mnamo Januari 2020.

Korea Kusini, vibanda vya kupima corona viliwekwa nje ya hospitali.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Korea Kusini, vibanda vya kupima corona viliwekwa nje ya hospitali.

Huko Korea Kusini, hospitali kama Yangji, katika wilaya ya Sewan's Gwan-Ak, ziliundwa kushughulikia ugonjwa wa covid -19 kutoka upimaji hadi matibabu.

Hapa, watu hawahitaji hata kuingia kwenye jengo: wanapimwa wakiwa mbali katika kibanda maalum, kilichofungwa kabisa.

Hospitali inashughulikia vipimo vyake vyote hapa na matokeo kawaida hupatikana ndani ya masaa manne hadi matano.

Barabara moja kutoka hospitali, timu ya kufuatilia na kutathmini hali za watu hufuatilia kila kesi inayoshukiwa.

Timu hiyo inafanya uchambuzi wa kina, wa kisayansi na ina inafuatilia maelezo kama vile kadi za mkopo na data ya simu ya rununu.

Yeye hufuatilia kamera kote wilayani, akituma kundi lake kwenda kwa jamii kukagua mitaa anapoona kitu kinachowatia wasiwasi.

Waziri Mkuu Chung Sye-kyun alichukua udhibiti wa hali hiyo kabla hata nchi haijapata kesi iliyothibitishwa ya covid, akiyapa kipaumbele mambo matatu muhimu: upimaji, ufuatiliaji na ufahamu wa waliko watu.

"Kwa kutumia mkakati huo, tumepata matokeo mazuri na muhimu," alisema Sye-kyun.

Idadi ya vifo nchini Korea Kusini, nchi ya watu milioni 52, ni 1,693.

Hatua ya 3: Msaada katika Karantini

"Kuwaweka watu nyumbani ndio sababu kuu ambayo tumeweza kudhibiti COVID," anasema Usha Kumari, mfanyikazi wa afya wa jamii huko Kerala, India.

Usha ni mmoja wa wanaharakati 30,000 walioidhinishwa wa afya ya jamii, wanaojulikana kama wafanyikazi wa Asha.

Jukumu la Usha limekuwa kuhakikisha kuwa kila mtu ambaye anahitaji kujitenga katika eneo lake anafanya hivyo.

Yeye huwafanyia ununuzi wa bidhaa, hukusanya dawa zao na kila kitu wanachohitaji, ili wasiondoke nyumbani.

Msaada kwa wale wanaojitenga hauishii hapo tu. Jamii zimekuwa zikitoa hadi chakula cha bure kwa watu 600 kila siku kwa wale wanaojitenga nyumbani au hospitalini na huduma za afya ya akili zimetolewa tangu kuanza kwa janga hilo.

Uingereza, wanaowasili nchini humo kutoka nchi zilizo katika hatari ya kupata corona ni lazima wawe kwenye karantini.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Uingereza, wanaowasili nchini humo kutoka nchi zilizo katika hatari ya kupata corona ni lazima wawe kwenye karantini.

Mpango huo pia umetoa msaada wa kifedha na wakati mwingine, hulipa akaunti zilizosalia zilizohifadhiwa kwa muda.

Waziri wa Afya wa Kerala KK Shailaja alijifunza mengi muhimu miaka mitatu iliyopita kutokana na kushughulikia virusi hatari vya Nipah na ameyatumia kukabiliana na COVID.

Anasisitiza kuwa kwa kuhakikisha msaada kwa wale wanaojitenga, maafisa waliweza kudhibiti kuenea na kuzuia hospitali kuzidiwa.

Na idadi ya watu milioni 35, Kerala ilifaulu kujitoa kuwa na idadi kubwa zaidi ya kesi nchini India mnamo Machi 2020 na kuwa na moja ya kiwango cha chini kabisa cha vifo vya COVID-19 ulimwenguni.

Hatua ya 4: Kuwalinda wazee/Watu walio na umri wa juu

Mwanzoni mwa Aprili, Daktari Lisa Federle alianza kufanya majaribio katika nyumba za wauguzi katika jiji la Tübingen, katika jimbo la Baden Württemberg, nchini Ujerumani, kuzuia maambukizi ya virusi na kuruhusu wageni kuingia.

Meya wa jiji hilo, Boris Palmer, alifikiria: "Tunapaswa kujenga sehemu maalum za ulinzi kwa watu walio katika hatari zaidi."

Alikuwa ameona athari za virusi huko Italia na Uhispania kwa watu wenye umri wa juu. "Hawa ndio watu wa zamani zaidi, kwa hivyo tunahitaji ulinzi maalum kwao."

Kuna maeneo manne muhimu ambayo yamekuwa muhimu katika kukabiliana na usambaaji wa virusi vya corona.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuna maeneo manne muhimu ambayo yamekuwa muhimu katika kukabiliana na usambaaji wa virusi vya corona.

Palmer alitumia bajeti yake ya mitaa kutanguliza utunzaji na msaada kwa idadi ya wazee wa jiji pamoja na huduma ya teksi inayofadhiliwa, maski za bure zilizopelekwa majumbani, na masaa maalum ya ununuzi.

Hiyo ilimaanisha kwamba hospitali ya chuo kikuu cha jiji hilo ilipokea wagonjwa wachache wa Covid-19 na haikulazimishwa kufuta taratibu zingine za matibabu.

Wazee wamekuwa wahanga wakubwa wa janga hilo na haswa Ulaya pamoja na wale ambao wanaishi katika makazi.

Hatua ya 5: Mkakati wa Chanjo

Zaidi ya watu milioni 26 nchini Uingereza wamepokea angalau dozi moja ya chanjo ya virusi vya corona kama sehemu ya programu kubwa zaidi ya chanjo ambayo nchi imewahi kuzindua.

Ingawa iko nyuma sana ya Israeli, nchi ambayo inaongoza kwa chanjo ulimwenguni ambayo hadi sasa imewachanja zaidi ya nusu ya idadi ya watu, Uingereza imefanikiwa sana na mpango wake wa chanjo.

Zaidi ya watu milioni 24 wamepokea chanjo ya corona kote Uingereza

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Zaidi ya watu milioni 24 wamepokea chanjo ya corona kote Uingereza

Mafanikio ya Uingereza yanatokana kwa sehemu kubwa na juhudi kubwa ya kupanga.

Idara ya Afya na Huduma ya Jamii ilianza kupanga mpango wa chanjo ya ya umma hata kabla ya kesi ya kwanza ya covid-19 kuthibitishwa nchini Uingereza.

Katika msimu wa joto, serikali ilisaini mkataba wa dozi milioni 100 za chanjo ya Oxford-AstraZeneca na dozi milioni 30 za chanjo ya Pfizer-BioNTech.

Mambo ni tofauti huko Uropa: mipango ilianza baadaye na utekelezaji umekuwa polepole.

Ni asilimia 8 tu ya watu huko Uropa ambao wamepokea chanjo hadi sasa, ikilinganishwa na asilimia 36 nchini Uingereza.

Mikataba ya chanjo ya Uingereza ilifungwa miezi mitatu mapema kuliko Umoja wa Ulaya.

Hali ni mbaya zaidi katika nchi zinazoendelea. Wakati karibu Ulaya na Marekani zimeanza kampeni za chanjo, ni nchi chache tu za Kiafrika zilizoanzisha.

Nchi nyingi zinasubiri chanjo ya Covax

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Nchi nyingi zinasubiri chanjo ya Covax

Huko Cape Town, Afrika Kusini, Michael Kuta ni mmoja kati ya watu wengi katika manispaa ambao walijitolea kushiriki katika jaribio lililofanywa na Daktari Linda Gail-Bekker kwa chanjo ya Johnson & Johnson.

Michael hajui ikiwa amepata chanjo au placebo, lakini anasema ilimfaa.

Nchi nyingi masikini zinategemea chanjo kutoka kwa Covax, mpango unaoendeshwa na Alliance for Vaccines (GAVI) na WHO, ambao unakusudia kuhakikisha upatikanaji wa chanjo kwa kila mtu.

Uingereza ndiye mchangiaji mkubwa zaidi na mchango wa karibu $ 700,000,000. Afrika Kusini imejiunga na mpango huo.

Walakini, mkakati wa chanjo lazima uwe juhudi ya kimataifa. Katika nchi ambazo upatikanaji wa chanjo ni mdogo, virusi vina nafasi ya kubadilika, kama ilivyofanyika huko Afrika Kusini na Brazil, na kuunda aina mpya ya virusi ambazo zinaambukiza kwa haraka zaidi na ambazo zinaweza kuenea nje ya nchi.

Wanasayansi wanaogopa kwamba aina hizi zinaweza kuwa sugu zaidi kwa chanjo zilizopo na kwa hivyo zinatishia nchi ambazo zimefanikiwa kutolewa kwa chanjo.

Línea