Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kathleen Folbigg: Je sayansi inaweza kumwachia huru mwanamke aliyefungwa jela kwa mauaji ya watoto wake?
Hebu fikiria kidogo tu kile unachoweza kuhisi, ikiwa wewe ni mama, umezaa watoto wanne na mmoja baada ya mwingine, wakiwa watoto wakaanza kufariki dunia ndani ya kipindi cha miaka 10.
Tena fikiria, wakati ambapo wewe kama mama umeshutumiwa kimakosa kuua watoto wako kwa kuwakosesha hewa safi na kukahukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa makosa manne ya uhalifu mbaya ambao haukuutenda.
Sasa hivi inajitokeza kuwa kweli simulizi ya Kathleen Folbigg, mama mmoja nchini Australia aliyekumiwa kifungo cha miaka 30 kwa mauaji ya watoto wake wanne.
Wakati wa kesi yake mwaka 2003 alibandikwa jina la "Muuaji sugu wa kike hatari sana Australia", Folbigg tayari amehudumia kifungo chake kwa miaka 18 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia kwa mtoto wake wa kwanza Caleb, na mauaji ya watoto wake watatu, Patrick, Sarah na Laura.
Lakini sasa hivi, kuna ushahidi mpya wa kisayansi ambao unaonekana kubadilisha kesi hiyo.
Wiki jana, wanasayansi maarufu 90 walitia saini ombi linalounga mkono matokeo ya utafiti wa kisayansi na wataalam wa tiba ambalo liliwasilishwa kwa gavana wa eneo likitaka Bi. Folbigg aachiwe huru mara moja.
Ikiwa Folbigg ataachiwa huru na mashitaka dhidi yake kufutiliwa mbali, basi hukumu yake itaonekana kuwa ya ukosefu mkubwa wa haki katika historia ya Australia.
"Katika kesi yake iliamuliwa kuwa bila shaka yoyote mtu aliyekuwa amekusudia alidhuru watoto na ikaamuliwa kwamba kilichofanyika ni kuwakosesha hewa safi," alisema Reginald Blanch, aliyekuwa jaji aliyeongoza jopo lililosikiliza kesi yake. "Ushahidi huo ulimwelekezea kidole cha lawama Bi. Folbigg."
Miaka miwili iliyopita serikali ya eneo iliahidi wananchi wake kwamba imejitahidi kwa kila namna "kupata ushahidi sahihi" dhidi ya kesi hiyo.
Hata hivyo kila kukicha sayansi imeendelea kuonesha kutilia mashaka hukumu iliyotolewa dhidi ya mwanamke huyo.
"Sayansi iliyojitokeza katika kesi hi haiwezi kupuuzwa," amesema mwanasayansi anayehusika na masuala ya vinasaba ambaye pia ni Profesa mtafiti Jozef Gecz.
Mtafiti wa masuala ya watoto na afya ya umma Profesa Fiona Stanley amesema: "Inasikitisha kuona kuwa ushahidi wa kitiba na kisayansi umepuuzwa. Sasa tuna maelezo ya kina kuhusiana na vifo vya watoto wa Folbigg."
Maelezo ya sasa hivi ya kilichotokea yanahusisha mabadiliko ya chembe za urithi kwa Kathleen Folbigg na mabinti zake wawili ambapo wanasayansi wanasema kuna uwezekano mkubwa ni "visababishi vya magonjwa" ambavyo wanaamini ndio chanzo cha vifo vya watoto wake wa kike, Sarah na Laura.
Pia kumebainika mabadiliko ya chembe zingine za urithi kwa watoto wake wa kiume, Caleb na Patrick ingawa wanasayansi wanakubali kwamba hilo linahitaji utafiti zaidi.
Pia unaweza kusoma:
Utafiti wa awali ulibaini kwamba wasichana wake walikuwa na mabadiliko ya chembe za urithi.
"Tulibaini chembe ambazo hazijawahi kuonekana kabla kwa Sarah na Laura ambazo walikuwa wamezirithi kutoka kwa Kathleen Folbigg," Profesa Vinuesa wa masuala ya chembe za urithi chuo kikuu cha Taifa cha Australia amezungumza na BBC.
"Chembe tulizoziona zinaweza kusababisha kifo ghafla kutokana na mshtuko wa moyo."
Kundi la wanasayansi kutoka nchi mbalimbali lilibaini kwamba chembe za Folbigg zinaweza kusababisha mshtuko wa moyo na kifo cha ghafla hata kwa watoto wadogo wakiwa wamela
Wanasayansi walisema: "Tunachukulia kuwa chembe hizo ndio zilisababisha vifo kwa watoto wawili wa kike."
Wanasayansi pia waliripoti kwamba Caleb na Patrick kila mmoja wao alikuwa na chembe za ajabu ambazo zilisababisha kifafa kwa panya.
Na kutokana na hitimisho hilo, wanasayansi wanasema watoto wote wanne walikufa wenyewe kwasababu ya chembe walizorithi wala hawakuuliwa na mama yao.