Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mahojiano ya Oprah kwa Harry na Meghan: Je ni kwanini familia ya Kifalme Uingereza inaitwa 'Kampuni'?
Bado yaliyozungumzwa katika mahojiano ya Mwanamfalme Harry na mke wake Meghan katika mahojiano na Oprah Winfrey yanaendelea kuwa gumzo nchini Uingereza.
Katika taarifa fupi iliyotolea Jumanne na kasri la Buckingham ambapo familia ya Kifalme ilionesha kusikitishwa na madai ya Mwanamfalme Harry na mke wake Meghan haikutuliza majadaliano makali yaliyoibuka baada ya mahojiano yao.
Meghan Markel alirejelea mara kadhaa neno 'The Firm'{ kampuni} alipokuwa akizungumzia maisha yake na matatizo aliyokumbana nayo Windsor.
Lakini je nini chimbuko la neno hilo?
Kilichotawala katika fikra za watu
Kuna dhana tofauti kuhusiana na chimbuko lake. Neno "The signature" kuashiria Familia ya Kifalme.
Baadhi ya waandishi wanasema wanalihusisha na Mwanamfalme Phillip aliyeanzisha jina hilo kumaanisha Familia ya Kifalme.
Inasemekana kuwa jina hilo la utani lilibuniwa mwaka 1947 na Mwanamfalme Philip, Duke wa Edinburgh, baada ya kumuoa ambaye wakati huo alikuwa binti mfalme na Malkia wa sasa wa England, Elizabeth II.
"Alilinganisha ndoa hiyo na kuoa biashara ya familia au kampuni," ameelezea mwandishi Marlene Koenig.
Hata hivyo kulingana na baadhi ya waandishi na wanahabari kama Penny Junor au mwanahistoria Ed Owens, waandishi wa vitabu viwili kuhusu suala hilo, chimbuko la jina hilo lilianza kabla hata ya harusi.
"Wanasema kuwa Jorge alipokuwa mwanamfalme na mwanafunzi katika chuo kikuu cha Cambridge, walimuona akivuta sigara akiwa amevaa sare ya chuo. Mkurugenzi wakati huo akamwambia anafaa kuwa mfano mwema: 'Wewe unatoka familia ya kifalme, na wakati huohuo mwanamfalme mdogo ambaye alikuwa Mfalme wa baadaye akajibu: 'Sisi sio familia, ni kampuni'", Owens anasema.
Mwanahistoria huyo anaeleza kuwa msemo huo unamaanisha majukumu na huduma kwa umma ndio kipaembele na familia na starehe za maisha ya kibinafsi ndio yanafuata.
"Kile ambacho kitabu cha Beverley Baxter kinaonesha ni kuwa familia ya kifalme haiwezi kufurahia maisha yao binafsi, muda na familia kwasababu wamejitolea zaidi katika utekelezaji wa majukumu ya umma. Na hapo ndipo kulipotokea wazo la utekelezaji wa majukumu, huduma na kujinyima.
"Lakini hili lilikuwa tofauti kabisa kwa Edward VIII, kaka yake mkubwa, ambaye alijiuzulu ili kufurahia maisha yake na kutimiza ndoto zake binafsi mbali na jukumu lake kama Mfalme," ameongeza Owens.
Nani ni sehemu ya "Kampuni"
Maana liojitokeza kutoka kwa maneno ya George VI inatofautiana na dhana ya Mwanamfalme Phillip aliyetoa maoni yake kwa kumuoa Elizabeth na maana hiyo ndio inaonekana kujitokeza hii leo.
"Duke wa Edinburgh alikuwa anarejelea wafanyakazi wote katika familia ya kifalme kama: Watumishi, wataalamu, watendaji, wataalamu wa mahusiano ya umma," Owens amesema.
Na hivyo ndivyo ilivyo, Familia ya Kifalme ni kampuni ambayo ni zaidi ya wahusika wake, ikijumuisha wanajeshi ambao ni makatibu wa kibinafsi, washauri wa mawasiliano, wakuu wa idara, madereva, wasaidizi, watunza bustani na wengne wote wanaoendesha shughuli za makazi ya Kifalme na maisha ya wanaoishi nao.
Familia ya Kifalme ina nguvu kubwa kifedha. Mwaka 2019, jarida la Forbes lilikadiria kwamba utajiri wa malkia ni takriban dola milioni 500.
"Familia ya Kifalme ni biashara kubwa. Na watendaji wote wakuu katika kampuni hiyo wanatarajiwa kujitahidi kwa kila namna kutojihusisha na sakata yoyote ile ambayo inaweza ikatia doa sifa ya kampuni, biashara ya kifamilia, "kulingana na kitabu cha Penny.
Makazi ya Kifalme pekee ya Buckingham yana wafanyakazi zaidi ya 400 ambao wanaendesha kila kitu kuanzia utoaji huduma ya upishi kwa karamu zinazoandaliwa na Malkia, tafrija na hafla za vyakula vya jioni hadi mfumo wa uendeshaji kampuni kwa mtindo wa uhusiano wa umma ulioundwa na watu kutoka dunia ya uandishi hadi siasa.
Maana iliyotolewa na Meghan
Wakati wa mahojiano ya Mwanamfalme Harry na mke wake Meghan na Oprah Winfrey, wawili hao waliamua kurejelea kampuni nzima badala ya watu binafsi.
"Nafikiri alitumia neno hilo kama ilivyomaanishwa na mwanamfalme Philip. Alikuwa anaelezea kundi hili la watu ambao wanahudumia familia ya kifalme. Wataalamu wa masuala ya uhusiano mwema, makatibu wa kibinafsi, watu ambao kila wakati wanafuatilia vyombo vya habari kuangalia nini kimeandikwa kuhusu familia hiyo, ambao hurejesha taarifa hizo kwa familia ya kifalme na kufanya maamuzi kwa niaba yao, "Owens ameelezea.
"Ikiwa alizungumzia familia ya kifalme, moja kwa moja angetaja watu binafsi, Cambridge, Cornwall, Malkia mwenyewe au Phillip, lakini hakumaanisha hao, " mwanahistoria amerejelea.
Kinachochanganya zaidi, Malkia Elizabeth alianzisha "kampuni yake mwenyewe ya watu 8" Desemba 2020, kundi la watu wanane wa kifalme ambao wanawakilisha familia hiyo kwa umma na kuendeleza utawala wake binafsi wa "mtu lazima aonekane, ili aaminiwe".
Kundi hilo linajumuisha Mwanamfalme Charles na mke wake Camilla, Duchess of Cornwall; Mwanamfalme William na mke wake Kate Middleton, Duchess wa Cambridge; Mwanamfalme Edward na mke wake Sophie, Countess wa Wessex; Binti Mfalme Anne na Malkia mwenyewe.
Licha ya mazungumzo makali yaliyojitokeza katika majadiliano yao, Meghan na Harry walionesha upendo kwa familia ya kifalme.
"Licha ya kilichosemwa mwanzoni katika mahojiano, kila kitu alichosema Meghan kilikuwa kimepangwa vizuri na yeye mwenyewe na timu yake," Owens amesema.
"Nafikiri ingekuwa makosa makubwa kwa Harry na Meghan kwa kuzingatia namna ambavyo raia Uingereza na kote duniani wangewachukulia ikiwa wangemkosoa Malkia moja kwa moja kwasababu hadi kufikia sasa ndiyo mtu maarufu na anayeheshimiwa sana".