Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Thamani ya Jay Z: Utajiri wa Shawn Corey Carter umeongezeka pakubwa baada ya kuuza huduma ya muziki wa mtandaoni Tidal
Thamani ya Rapa wa Marekani Shawn Corey Carter maarufu Jay Z imeongezeka baada ya kuingia katika mkataba wa kuuza kampuni ya muziki inayotoa huduma mtandaoni Tidal kwa kampuni ya malipo ya simu ya Jack Dorsey kwa dau la $297 million.
Makubaliano hayo yalifanyika wiki moja baada ya rapa huyo kuuza nusu ya kampuni ya mvinyo ya Brignac Champagne kwa LVMH kwa makubaliano ya thamani ya $640 m.
Kulingana na Jarida la Forbes , utajiri wa Jay Z ulipanda kwa asilimia 40 baada ya mauzo ya kampuni hizo mbili kumfanya kuongeza thamani yake kutoka $1 b hadi $1.4 b.
Kulingna na mauzo ya huduma ya Tidal , Forbes inasema kwamba rapa huyo alijipatia faida ya $149 mbali na kuwa mwanachama wa bodi ya Square.
Chini ya mkataba huo wa Tidal, hisa za wasanii zitaendelea kumiliki kampuni hiyo huku Jay Z akimiliki kiwango kidogo.
Afisa mkuu mtendaji wa Square Jack Dorsey alingia katika mtandao wake wa twitter na kutangaza hatua hiyo.
Mali nyengine ya Jay Z
Licha ya kukosa kufanya tamasha lolote au kutoa albamu mwaka uliopita, Jay Z alijipatia mamilioni ya fedha kutoka kwa kampuni ya mivinyo ya Armand de Brignac Champagne na D'Usse cognac.
Rapa huyo anashikilia taji la bilionea wa kwanza wa muziki wa hip hop alilopata 2019.
Mali ya Jay Z ni pamoja na kampuni ya burudani ya Roc Nation, Jean - Michel Basquiat,
Kmapuni ya E Marcy venture ilimpatia $85m mwaka 2019.