Malindi: Jinsi mji wa pwani ya Kenya ulivyobadilika na kuwa 'Italia ndogo'

Ufukwe wa bahari mjini malindi Kenya

Chanzo cha picha, I Einashe

Maelezo ya picha, Ufukwe wa bahari mjini malindi Kenya
Iliyochapishwa

Katika msururu wa barua kutoka kwa waandishi wa Afrika , Ismail Einashe anachukua likizo katika pwani ya Kenya , lakini baadaye anashangaa iwapo amesafiri katika taifa jingine.

Short presentational grey line

Malindi, mji wa pwani uliopo kando ya bahari Hindi uliogunduliwa katika karne ya 13 , ukiwa kilomita 120 kaskazini mashariki mwa Mombasa na umejulikana kama Itali ndogo tangu miaka ya 60.

Mji huo wa kitalii ulio na migahawa ya Kitaliano , chakula na maduka - mabango hutoa matangazo yao kwa lugha ya Kitaliano, menu za migahawa zinatoa vinywaji vya baada ya chakula kama vile Limenoncelllo na Amaro.

Wakaazi wengi wanazungumza Kitaliano - kutoka mwenye duka katika eneo mahali ambapo nilikuwa nikiishi hadi watoa huduma katika migahawa , madereva wa boda boda ambao walinibeba hadi wauza samaki waliokuwa katika fukwe za bahari.

Ndio Lugha inayozungumzwa katika mji huo.

Duka hili la jumla lina jibini na nyama baridi kutoka Itali

Chanzo cha picha, I Einashe

Maelezo ya picha, Duka hili la jumla lina jibini na nyama baridi kutoka Itali

Unapozunguka katika barabara za zamani za Waswahili unasikia sauti ya Kitaliano .

Duka la jumla katikati ya mji wa Malindi linaendeshwa na raia wa Kitaliano na limejaa bidhaa kutoka nje , ikiwemo mivinyo , na pasta, na duka hilo lina eneo lenye vinywaji baridi kama vile Parmigiano-Jibini ya Reggiano, salami na nyama za Kitaliano . Na cha kufurahisha zaidi ni biskuti zilizojazwa krimu.

Siasa za kiubaguzi

Nilipoelekea katika ufukwe wa bahari , nilifuatwa na wazee wa Kitaliano katika hoteli ya Osteria.

Duka la gelato mjini Malindi, Kenya

Chanzo cha picha, I Einashe

Maelezo ya picha, Unaweza kupata krimu ya Kitaliano mjini Malindi na menu katika migahawa zimeandikwa lugha ya Kitaliano na Kiingereza

Wanawake wawili waliovalia bikini na miwani ya kuzuia jua walipita mbele yangu wakisema Ciao, Ali, Ciao, Ali huku muhudumu mmoja akiwakaribia. "Buongiorno signora," alisema huku akiandaa vitanda vilivyopo katika ufukwe wa bahari.

Kando yao ni wanandoa wawili wa Kitaliano wakiwa wamejipaka mafuta ya kuzuia ngozi kuchomeka katika vitanda vya ufukweni.

Nililazimika kununua kinyawaji ili kuhakikisha kuwa nilikuwa Malindi na siao Palermo au Naples.

Nilihisi kana kwamba ulikuwa ufukwe wa bahari ambao nilikuwa nimetembelea nchini Itali - tofauti ya pekee ilikuwa joto , minazi na chumvi ya bahari Hindi.

Nilipojaribu kujiliwaza katika kitanda kimoja cha ufukweni kilichokuwa karibu na mnazi , muhudumu wa mgahawa huo alikuja na kuniambia kwamba kitanda hicho kilikuwa kimehifadhiwa wanandoa wa Kitaliano.

Nilihisi tofauti kuwepo pale kama mtalii mweusi

1px transparent line

Katika mgahawa mmoja uliopo mjini humo nililazimika kuinua mkono wangu mara kadhaa ili kuonekana na hata kwa Wataliano ambao huwa marafiki sana wakiwa nyumbani sikupata makaribisho mema.

Na siasa za kibaguzi zimejiingiza Malindi , huku baadhi ya watu wa jamii ya Mijikenda wakihisi kwamba raia wa Kitaliano wanaruhusiwa kufanya lolote kutokana na uwekezaji wao katika mji huo.

Kumekuwa na hasira wakati mwengine kutokana na kile ambacho raia hao wa Kitaliano wanafanyiwa , huku wakazi wengi wakiamini kwamba baadhi ya raia hao wa Kitaliano hawachunguzwi kutokana na uhalifu wanaotekeleza.

Nafasi na Utalii

Historia ya wataliano mjini Malindi inatokana na kituo cha Broglio kilichokuwa kikkendeshwa na Wataliano katika pwani ya kenya.

Map
1px transparent line

Wataliano wa kwanza kuwasili katika mji huo walikuwa wahandisi na wanasayansi waliopenda kile walichopata.

Habari baadaye zilisambaa kuhusu fukwe za bahari za Malindi na chakula chake pamoja na wakaazi wake wakarimu.

Kufikia 1970 jamii hiyo ilianza kuishi katika eneo hilo na kutafuta nafasi katika sekta ya Utalii.

Walifungua hoteli , migahawa, kujenga nyumba za kitalii na kuwa wawekezaji wakubwa wa sekta ya Utalii mjini humo.

line

Kituo cha anga za juu cha Nasa

Kituo cha anga za juu cha Nasa

Chanzo cha picha, NASA

line