Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Je tunafahamu nini kuhusu chanjo ya AstraZeneca itakayowasili Kenya Jumanne?
Shehena ya kwanza ya chango ya corona ya AstraZeneca kupitia mpango wa Covax inatarajiwa kuwasili nchini Kenya Jumanne.
Hii ni baada ya nchi hiyo kutangaza kwamba itaendelea na mipango ya kutumia chanjo ya Astrazeneca na kupuuza wasiwasi wa ufanisi wa chanjo hiyo katika kutoa kinga dhidi ya viruis vya corona.
Lakini je unafahamu nini kuhusu chanjo hii?
Chanjo ya AstraZeneca inakadiriwa kugharimu dola mbili kwa dozi moja na dola nne kwa dozi kamili. Kupitia mpango wa Covax Kenya itapata chanjo ya kiwapa asilimia 20 ya wanachi ambayo ni takrikban watu milioni 10.
Ufanisi wake ukoje?
Kampuni ya AstraZeneca imesema chanjo yao inaweza pia kusafirishwa na kuhifadhiwa kwenye friji ya kawaida, ambayo watetezi wake wanasema ingeifanya iwe rahisi kusambaza, haswa katika nchi masikini, kuliko Pfizer, ambayo inahitaji kusafirishwa na kuhifadhiwa kwa kiwango cha joto nyuzi 70 kipomo cha Celsius.
Chanjo inapaswa kutolewa kwa muda gani?
Chanjo hii inapaswa kutolewa kwa dozi mbili kwa watu wote alio na umri wa zaidi ya miaka 18 bila kuwepo na umri wa wa juu.
Utafiti umebaini muda bora kati ya chanjo ya kwanza na ya pili ilikuwa ni wiki 8 hadi 12 ili kuhakikisha kinga ya maili imeongezeka.
Unaweza pia kusoma:
Watakaopewa kipaumbele ni wahudumu wa afya, wazee, wale ambao wana matatizo ya afya na waalimu.
Je wanawake wanawazito wanastahili kuchanjwa?
Japo wanawake wajawazito wako katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya corona, kuna maelezo kidogo kuhusu usalama wa chanjo hii kwa ujauzito.Wanawake wajawazito wanaweza tu kuchanjwa ikiwa manufaa ya chanjo inazidi hofu ya hatari inayohusiana na hatua hiyo.
Kutokana na sababu hii, wanawake wajawazito walio katika hatari ya kupata virusi vya SARS-CoV-2 (kwa mfano wahudumu wa afya) au wale walio na matatizo ya kiafya ambayo yanawaweka katika hatari ya kupata magonjwa hatari, wanaweza kuchanjwa kwa kupitia ushauri wa wataaamu wa afya.
Je chanjo itazuia kugeuka kwa umbo jipya la kirusi na aina nyingine za virusi za corona?
Virusi hivi vimekuwa vikigeuka umbo na wakati mwingine hufanya hivyo kwa kiasi kwamba vinakua sugu kwa chanjo, kwahiyo vinahitaji kufanyiwa mabadiliko.
Aina ya virusi vya corona iliyobainika Afrika Kusini na Uingereza tayari imesambaa katika nchi nyingine na imesambaa kwa viwango vya hali ya juu.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kikosi kinachosimamia chanjo ya Covid-19 nchini Kenya, Willis Akhawale amewaambia wanahabari kwamba wataalamu wanaendelea kufanya utafiti kubaini ni virus via aina gani vilivyopo na ni change aina gani inaweza kupambana nato na kuthibiti visisambae.
Unaweza pia kutazama: