Donald Trump: Sera ya Marekani imetoka katika Amerika kwanza na kuwa America mwisho

Bw Trump alirudia madai yake ya uongo kwamba alishinda uchaguzi wa mwezi Novema na akadokeza kuhusu kugombea uchaguzi wa 2024
Maelezo ya picha, Bw Trump alirudia madai yake ya uongo kwamba alishinda uchaguzi wa mwezi Novema na akadokeza kuhusu kugombea uchaguzi wa 2024
Iliyochapishwa

Donald Trump anasema hana mipango ya kuanzisha chaka kipya cha kisiasa, akiuambia mkutano wa wahafidhina mjini Florida kuwa hilo litagawanya kura za Warepublican.

Katika hotuba yake ya kwanza tangu Mdemocrat Joe Biden awe rais, Bw Trump pia alidokeza kuwa anaweza kugombea tena urais mwaka 2024.

Alimkosoa vikali mrithi wake, akisema kuwa sera ya Marekani imetoka kuwa " Marekani kwanza na kuwa Marekani mwisho ".

Hotuba hiyo inakuja wiki mbili baada ya Bw Trump kuondolewa kesi ya mashitaka dhidi yake.

Conservative Political Action Conference (CPAC) ni mkutango mkubwa zaidi wa wahafidhina wenye itikadi kali na wanasiasa, na kwa kawaida hutoa mwanagaza kuhusu mwelekeo wa chama cha Republican.

Kuonekana kwa Bw Trump katika mkutano huo Jumapili kunaonesha kuwa bado anaendelea kuwa na ushawishi kaytika chama chama chake licha ya maafisa wa ngazi ya juu wa chama hicho kujitenga na rais huyo wa amani.

Supporters hear Donald Trump speak at the Conservative Political Action Conference in Orlando, February 28, 2021

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waconservatives wenye shauku wakimshangilia Bw Trump katika mkutano wa CPAC

Hali katika mkutano huo uliofanyika Orlando -ambao ulianza Alhamisi- imeonesha hali ya juu ya uungaji mkono na ufuasi wa Bw Trump, ikiwa ni pamoja na seneta wa Texas Ted Cruz na mwana wa kiume wa Trump, Donald Trump Jr miongoni mwa wazungumzaji katika kikao hicho.

Rais huyo wa zamani bado amepigwa marufuku na mitandao ya kijamii , ikiwa ni pamoja na Facebook na Twitter kufuatia kauli zake wakati wa ghasia za maandamano ziliosababisha vifo katika Baraza la seneti la Marekani- Us capitol mwezi wa Januari.

Bw Trump amekuwa akiishi katika makazi yake ya Mar-a-Lago Florida tangu alipoondoka Ikulu ya White House mwezi Januari.

Donald Trump alisema nini Trump ?

Trump mwenye umri wa miaka 74- alishangiliwa na wafuasi wake katika Hoteli ya Hyatt Regency Hbaada ya kuwasili akiwa amechelewa kwa takriban saa moja. Wat wengi katika umati hawakuwa wamevaa barakoa.

"Ninasimama mbele yenu leo kutangaza kwamba safari yetu nzuri tuliyoianza miaka minne iliyopita haijamalizika ,"alisema.

"Tumekusanyika hapa mchana huu kuzungumzia kuhusu hali ya baadae-hali ya baadae ya vuguvugu letu, hali ya baadae ya chama chetu, na hali ya baadae ya nchi yetu tunayoipenda ."

Donald Trump Jr. waves to the crowd after speaking at the Conservative Political Action Conference (CPAC) in

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mtoto wa kiume wa Trump Donald Trump Jr pia alishangiliwa alipokuwa akizungumza katika kikao cha Conservatives

Bw Trump alipuuzilia mbali wazo lolote la kwamba ataanzisha chama kipya cha kisiasa- akielezea tetesi kwamba angefanya hivyo kama "taarifa za uzushi".

"Hilo si litakua ni jambo zuri? Ngoja tuanzishe chama kipya ili tugawe kura zetu na tusishinde kabisa ," alitania.

"Tuna chama cha Republican . Kitaungana kuliko ilivyowahi kutokea awali na kuwa imara zaidi kuliko kilivyokuwa."

Licha ya kupoteza ushindi katika uchaguzi wa mwezi wa Novemba na kukosolewa vikali kuhusu ghasia za mwezi wa Januari , ripoti zinasema kuwa bado Trump ni maarufu sana miongoni mwa wapiga kura wafuasi wake mashinani.

A golden statue of Donald Trump is seen being moved into CPAC conference

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kumbukumbu za ufuasi wa Trump ni pamoja na sanamu hii ya dhahabu P, ambayo imekuwa ikioneshwa

Wiki iliyopita kura ya maoni ya Marekani kuhusu wapigakura wa Trump ilionesha kuwa 46% wangemchagua Trump iwapo angehama Republican na kuanzisha chama chake mwenyewe.

Unaweza pia kusoma:

Katika hotuba yake katika mkutano wa CPAC, Bw Trump alirudia tena madai yake ya uongo kwamba alipoteza uhindi katika uchaguzi wa mwezi wa Novemba kwasbabu ya wizi wa kura na akadokeza kuhusu uchaguzi ujao wa mwaka 2024, akisema : "Ukweli unafahamu kuwa walipoteza ushindi wa White House. Lakini nani -anajua? inaweza hata kuamua kuwashinda kwa mara ya tatu, SAWA?"

Supporters of Donald Trump outside the Hyatt Regency Hotel in Orlando

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Many conservatives remain staunch supporters of Donald Trump

Aliukosoa utaala mpya, huku akimkosoa Bw Biden kwa kurudisha nyuma msimamo mkali kuhusu uhamiaji na usalama wa mipaka.

"Sote tulifahamu kuwa utawala wa Biden utakuwa mbaya , lakini hakuna hata mmoja wetu aliyefikiria kamwe kuwa ni kwa kiwango gani ubaya huo utakavyokuwa na ni kwa kiwango gani watakwenda kushoto ," aliuambia umati ulioshangilia.