Daktari Scott Green ajiunga na kesi kupitia Zoom huku akimfanyia mgonjwa upasuaji

Chanzo cha picha, SACRAMENTO SUPERIOR COURT
Daktari mmoja, katika jimbo la California alijiunga na kesi ya uvunjifu wa sheria barabarani kupitia mtandao wa Zoom huku akimfanyia mgonjwa upasuaji.
Scott Green aliyekuwa amevalia mavazi ya kufanya upasuaji, tayari alikuwa katika chumba cha upasuaji wakati alipojiunga na mahakama kusikiliza kesi dhidi yake mtandaoni siku ya Alhamisi, Sacramento Bee iliripoti.
Alipoulizwa na jaji, Bw. Green alisema anaweza kuendelea na kesi, na kuongeza yuko na "mpasuaji mwingine ambaye anashirikiana naye".
Jaji alisema haitakuwa "sawa" na kuahirisha kesi.
Bodi ya Matibabu ya California imesema katika taarifa kwamba inachunguza kisa hicho, ikiongeza kuwa "anatarajia madaktari kufuata kanuni ya huduma wakati wa kutibu wagonjwa wao".
Kabla ya kusikizwa kwa kesi mbele ya Mahakama ya Juu zaidi ya Sacramento, ambayo ilioneshwa mubashara katika mtandao wa YouTube, karani wa mahakama alimuuliza daktari huyo: "Hujambo, Bw Green? Salama. Unapatikana kushiriki kesi hii? Inaonekana kana kwamba upo katika chumba cha upasuaji."
Green alimjibu: "Naam ni mimi, mkuu. Ndio, Niko katika chumba cha upasuaji muda huu. Naam, naweza kushiriki kwenye kesi. Endelea mbele."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Karani alimwambia Bw. Green kwamba kesi itaendeshwa mubashara mtandaoni, kwa sababu mashtaka ya uvunjifu wa sheria za barabarani kisheria hutakiwa kuendeshwa wazi kwa umma. Wakati huo , afisa aliyeitwa kufika mahakamani aliinua macho yake.
Wakati wanamsubiri jaji, Kamishena wa Mahakama Gary Link, kujiunga kwa njia ya Zoom, Bw. Green alionekana akiendelea kumfanyia mgonjwa upasuaji.
Baada ya Link kujiunga, aliifahamisha mahakama: "Kama sijakosea, Ninaona mtuhumiwa aliye katikati ya chumba cha upasuaji akionekana kushiriki kikamilifu katika kutoa huduma kwa mgonjwa. Je! Hiyo ni kweli, Bwana Green? Ama niseme Dkt Green?"
Baada ya daktari kuthibitisha alikuwa katikati ya upasuaji wa mgonjwa na kwamba angelipendelea kuendelea, Bw. Link alisema: "Sijiskii huru kuendelea mbele na kesi kwa maslahi ya mgonjwa ikiwa uko katika mchakato wa upasuaji hata kama afisa yuko hapa leo."
Bw. Green akasisitiza anaweza kuendelea na kesi, akiongeza: " niko na mpasuaji mwingine kando yangu ambaye tunashirikiana naye, kwa hivyo naweza kusimama hapa na kuwaruhusu waendelee na upasuaji."
Bw. Link alimjibu: " Sikubaliani na hilo, Sidhani hiyo. Ni sawa. Nitatoa tarehe nyingine tofauti - wakati hutakuwa unamshughulikia mgonjwa."
BBC imewasiliana na ofisi ya Bw. Green kupata kauli yake.
Mpasuaji huyo ameripotiwa kukiambia kituo cha habari cha NBC: " Hiyo si kweli na sina la kusema. Asante."
Hii sio mara ya kwanza kikao cha mahakama kupitia mtandao wa Zoom kuzua gumzo.












