Jamal Khashoggi: Marekani inasema Mwanamfalme wa Saudia aliidhinisha mauaji ya Khashoggi

Chanzo cha picha, Reuters
Ripoti ya kijasusi ya Marekani imebaini kuwa Mwnamfalme wa Saudia Arabia Mohammed bin Salman aliidhinisha mauaji ya mwandishi wa habari wa nchi hiyo aliyekuwa ukimbizini Jamal mwaka 2018.
Ripoti iliyotolewa na utawala wa Bw Biden inasema mwanamfalme aliidhinisha mpango wa "kumkamata au kumuua" Khashoggi.
Marekani ilitangaza vikwazo kwa makumi kadhaa ya Wasaudia lakini sio dhidi ya mwanamfalme mwenyewe.
Saudi Arabia ilipinga ripoti hiyo ikiitaja kuwa "hasi, uongo na isiyokubalika ".
Mwanamfalme Mohammed, ambaye anatambuliwa kama mtawala wa ufalme, amekanusha kuhusika kwa namna yoyote ile katika mauaji hayo.
Khashoggi aliuawa alipokuwa akiutembelea ubalozi mdogo mjini Instanbul , Uturuki , na mwili wake ulikatwa katwa.
Mwandishi huyo wa habari aliyekuwa na umri wa miaka 59 wakati mmoja aliwahi kuwa mshauri wa serikali ya Saudi Arabia na alikuwa karibu sana na utawala wa Ufalme , lakini alikosana nao na kwenda nchini Marekani mwaka 2017.
Akiwa nchini Marekani, aliandika waraka wa kila mwezi katika gazeti la Washington Post ambapo alikosoa sera za Mwanamfalme Prince Mohammed.
Ripoti ilibaini nini?
"Tunatathmini kwamba Mwanmfalme wa Saudi Arabia Muhammad bin Salman aliidhinisha operesheni katika ubalozi wa Instanbul ya kumkamata au kumuua mwandi wa habari wa Saudia Jamal Khashoggi," repoti ya mkurugenzi wa ujasusi wa taifa la Marekani inasema.
Ni mwana wa Mfalme wa Saudia Salman bin Abdulaziz al-Saud na anaaaminiwa kuwa mtawala wa ufalme,
Orodha ya ripoti za ujasusi inaonesha sababu tatu za kuamini kwamba mwanamfalme lazima aliidhinisha operesheni ya mauaji hayo,
- Udhibiti wa uchukuzi wa maamuzi katika ufalme tangu mwaka 2017
- Uhusika wa moja kwa moja katika operesheni ya mmopja wa washauri wake pamoja na wajumbe wa kikosi cha ulinzi wa usalama wake.
- "uungaji mkono wake wa matumizi ya hatua za ghasia s kunyamazisha wapinzani walioko nje ya nchi "
Ripoti hiyo inayataja majina ya watu binafsi wanaodaiwa kushirikiana ,na kuhusika, katika mauaji ya Khashoggi. Lakini inasema "hatukufahamu mapema "wale waliohusika kupanga kumdhuru.
Mamlaka za Saudia zimelaumu mauaji hayo kufanywa na "operesheni " iliyotekelezwa na maafisa wa ujasusi waliotiumwa kumrudisha mwandishi huyo katika ufalme wa Saudia, na mahakama ya Saudia iliwashitaki na kuwafunga watu binafsi watano kifungo cha miaka 20 jela mwezi Septemba mwaka jana, baada ya kuwahukumu kifo awali.
Mwaka 2019, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2019, Agnes Callamard alilishutumu taifa la Saudi Arabia kwa "mauaji ya makusudi , yaliyopangwa na kutekelezwa" ya Khashoggi na akapuuzilia mbali kesi ya Saudia aliyosema inaendesha "bila misingi ya haki ".
Hii inamaanisha nini kwa uhusiano wa Marekani na Saudi Arabia?
Muda mfupi baada ya ripoti hiyo kutangazwa, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alitangaza vikwazo vya kusafiri vilivyoitwa "marufuku ya Khashoggi ".
Wale waliolengwa "wanaaminiwa kuhusika moja kwa moja na shuhghuli za mauaji ", alisema.
"Wahusika wanaaminiwa kuwalenga waliotoroka nchi kwa niaba ya serikali ya nchi yoyote ile ya kigeni hawaruhusiwi kufika katika ardhi ya Marekani ," alionya.
Zaidi ya hayo, Wizara ya fedha inawawekea vikwazo baadhi ya wale waliopo karibu na mwanamfalme: mmoja wa washirika wake wa karibu, naibu mkuu wa ujasusi wa zamani Ahmad Asiri,pamoja na mlinzi wake binafsi, ambaye alihusika katika mauaji.
Tangu mwaka 2018, CIA iliripotiwa kuwa inaamini mwanamgalme aliamrisha mauaji ya Khashoggi , lakini madai kwamba alihusika hayakuwahi kutolewa wazi na maafisa wa Marekani hadi sasa.Saudi Arabia, tni muuzaji mkuu wa mafuta dunaini, na mshirika mkuuu wa Marekani katika Mashariki ya Kati.

Chanzo cha picha, Getty Images
Joe Biden alizungumza na Mfalme Salman baada ya kusoma ripoti kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi.
Katika mazungumzo ya simu yaliyofanyika siku ya Alhamisi Salman, na rais Biden "waliafikiana juu ya umuhimu wa nafasi ya Marekani katika kuhakikisha haki za binadamu na utawala wa sheria vinatekelezwa ",ilisema Ikulu ya White House.
Unaweza pia kusoma:
Kulingana na vyanzo vilivyonukuliwa na shirika la habari la Reuters, utawala wa Biden pia unaangalia uwezekano wa kufuta mikataba ya silaha na Saudi Arabia ambayo inasababisha hofu ya ukiukwaji wa haki za binadamupamoja na kupunguza mauzo ya siku zijazo ya silaha kwa ajili ya "kujilinda"
" Inasikitisha kusema kweli kwamba ripoti hii , ambayo haina ushahidi na ambayo sio sahihi, inatolewa wakati ufalme ulikuwa umepinga wazi uhalifu huu mkubwa, na uongozi wa Ufalme ulichukua hatua muhimu kuhakikisha kuwa mauaji ya aina hiyo hayafanyki tena ,"iliongeza.
Ikulu ya Marekani pia ilipinga "hatua yoyote ambayo inaingilia uhusiano wake, hadhi ya taifa na uhuru wa mfumo wa mahakama".
Khashoggi aliuliwa vipi?
Khashoggi alikwenda kwenye ubalozi mdogo wa Instanbul mwaka 2018 ili kupata makaratasi yanayomruhusu kumuoa mchumba wake Mturuki.

Alidaiwa kuhakikishiwa na kaka yake mwanamfalme Prince Khalid bin Salman,ambaye alikuwa balozi wa Saiudia nchini Marekani wakati ule, kwamba atakuwa salama kutembelea ubalozi wa Instanbul. Mwanamfalme Khalid alikanusha kufanya mawasiliano yoyote na Khashoggi.
Kulingana na waendesha mashitaka wa Saudia, Khashoggi alikufa baada ya kulazimishwa kuchomwa madawa mengi kupita kiasi cha dozi ambayo yalimuua .
Baadae mwili wake ulikatwa katwa na kukabidhiwa kwa ''mshirika'' wa mpango wa mauaji hayo wa Uturuki nje ya ubalozi mdogo, alisema mwendesha mashitaka. Mabaki ya mwili wake hayajawahi kupatikana.
Maelezo yalifichuliwa katika maandishi yanayodaiwa kunukuliwa kutoka kwa sauti iliyorekodiwa ambay maafisa wa ujasusi wa uturuki wanadaiwa kuipata.












