Biden achukua hatua ya kwanza ya kijeshi ya shambulio la anga eneo linaloungwa mkono na waasi wa Iran

Iliyochapishwa

Jeshi la Marekani limefanya shambulizi la kwanza la anga kulenga wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran nchini Syria, ikiwa ni hatua ya kwanza ya kijeshi kuchukuliwa chini ya utawala wa Rais Joe Biden.

Ikulu imesema shambulio hilo liliagizwa kama hatua ya kulipiza kisasi mashambulizi dhidi ya Marekani na muungano wafanyakazi lililofanyika Iraq.

Hatua hiyo imefanya uharibifu katika "maeneo kadhaa" yaliyokuwa yanatumiwa na makundi ya wanamgambo yanayoungwa mkono na Iraq, taarifa kutoka Ikulu imesema.

Maafisa wa waasi hao wamesema mtu mmoja ameuawa lakini kuna taarifa kwamba idadi ya waliouawa sio chini ya 22.

Unaweza pia kusoma:

Ikulu imesema shambulio lake karibu na mpaka wa Iraqi mashariki mwa Syria ilikuwa hatua ya "kulipiza kisasi" ambayo ilichukuliwa kwa pamoja na "hatua ya kidiplomasia", ikiwemo kushauriana na washirika wa muungano.

Shambulio hilo limewadia baada ya mwanakandarasi raia wa kawaida kuuawa kwa shambulio la roketi katika maeneo ya Marekani mapema mwezi huu.

Mhudumu wa Marekani na wanakandarasi wengine watano pia waliejruhiwa wakati roketi ziliporushwa eneo la Irbil, ikiwemo kambi zinazotumiwa na muungano unaoungwa mkono na Marekani.

image captionAmericans were injured when rockets hit Irbil on 15 February

Mashambulizi ya roketi pia yamefanyika dhidi ya kambi za Marekani zilizopo Baghdad ikiwemo kwenye makazi ya ubalozi wa Marekani na wajumbe wengine wa kidiplomasia.

Kuna wanajeshi takriban 2,500 wa Marekani nchini Iraq kusaidia vikosi vya Iraqi katika mapigano dhidi ya kundi la Islamic State.

Tunajua nini kuhusu shambulizi hilo?

Ikulu imesema kuwa shambulio la Alhamisi lilifanyika kutokana na agizo la rais.

Lililenga maeneo ya mpakani yanayotumiwa na makundi kadhaa ya waasi wanaoungwa mkono na Iran ikiwemo kundi la Kataib Hezbollah na Kataib Sayyid al-Shuhada, Ikulu imesema.

Makundi ya Kataib Hezbollah na Kataib Sayyid al-Shuhada awali yalitekeleza mashambulizi ya anga au ya roketi dhidi ya vituo vya Marekani nchini humo.

"Rais Biden atachukua hatua kulinda raia wa Marekani na muungano wa maafisa wake. Na wakati huo huo, tumechukua hatua kwa kudhamiria inayolenga kumaliza hali ilivyo kwa ujumla mashariki mwa Syria na Iraq," taarifa hiyo imesema.

Hata hivyo Marekani haikuthibitisha kama kuna waliojeruhiwa lakini waasi wa Iraq wameliambia shirika la AP kwamba mtu mmoja ameuawa huku wengine wakijeruhiwa.

Maafisa wamesema mashambulizi ya anga yamekumba eneo la mpaka kati ya mji wa Syria wa Boukamal na mji wa Iraqi wa Qaim.

Msemaji wa Ikulu John Kirby amesema shambulizi hilo limelenga kuadhibu waasi wala sio kuzorotesha uhusiano na Iran zaidi ambayo Marekani inatafuta kuanza mazungumzo mapya nayo juu ya mpango wake wa nyuklia uliofutiliwa mbali na aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump , taarifa za New York zimesema.