Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Iran yavunja mkataba wa nyuklia kwa kurutubisha Uranium licha ya kuonywa
Iran imeanza kutengeneza madini ya uranium, licha ya kuonywa na mataifa yenye nguvu duniani kwamba ni uvunjaji mwingine wa mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015.
Wakaguzi wa Shirika la kimataifa la udhibiti wa nguvu za atomi wamethibitisha uwepo wa gramu 3.6 (0.1oz) za madini hayo katika kiwanda cha Isfahan wiki iliyopita.
Iran inasema inafanya utafiti na kutengeneza madini hayo kwa lengo la kutengeneza mafuta kwa ajili ya utafiti wa mitambo.
Lakini chuma cha uranium kinaweza pia kutumika kutengenezea bomu la nyuklia.
Iran inasisistiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani, lakini imekiuka makubaliano kadhaa katika mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 katika kipindi cha miaka miwli iliyopita.
Inasema inakiuka mkataba huo kujibu hatua ya Marekani kuiwekea vikwazo vya kiuchumi ambavyo vilirejeshwa tena mwaka 2018 na aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo Donald Trump wakati alipovunja mkataba huo kwa kujiondoa.
Mrithi wake, Joe Biden, anasema Iran lazima irejee katika kuheshimu kikamilifu mkata wa nyuklia kabla ya kuondolewa vikwazo. Lakini kiongozi wa ngazi ya juu zaidi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei anasema Marekani lazima iondoe vikwazo kwanza.
China ya mkataba huo Iran ilikubali kutotengeneza uranium au kufanya utafiti na kutengeneza madini hayo kwa muda wa miaka 15.
Siku ya Jumatano jioni Shirika la Umoja wa Mataifa la udhibiti nishati ya nyuklia (IAEA) lilisema kuwa mkurugenzi wake mkuu aliwafahamisha wajumbe wa mataifa "kuhusu shughuli za hivi karibuni za Iran za kutengeneza chuma cha uranium kama sehemu ya kile ilichosema, yanatumiwa katika kutengeneza mafuta kwa ajili ya utafiti wa mitambo ya Iran ".
"Shirika hilo Februari 8 lilisema kuwa lilithibitisha utengenezaji uranium kwa kiwango cha gramu 3.6 katika kituo cha utengenezaji wa mafuta cha Iran (FPFP) kilichopo katika eneo la Isfahan," liliongeza.
Unaweza pia kusoma:
Chini ya makubaliano ya mkataba wa mwaka 2015 - mapatatano yaliyofikiwa baina ya Iran, Marekani, Uchina, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Uingereza - Serikali ya Tehran ilikubali kupunguza urutubishaji wa madini yake ya uranium na kuwaruhusu wakaguzi wa kimataifa kuyafikia maeneo na viwanda vya urutubishaji wa madini hayo.
Na kwa kutekeleza hilo, vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Tehran viliondolewa,
Lakini Trump aliiondoa Marekani kwenye mkataba huo unaofahamika kama -Mpango wa pamoja wa kina wa utendaji- (JCPOA), katika jitihada za kuishurutisha Iran kufanya mazungumzo ya mkataba mpya, na akarejesha tena vikwazo vya kiuchumi dhidi yake.
Bw Trump alitaka kuzuia kabisa mpango wa nyuklia wa Tehran na pia kuzuia utengenezaji wake wa makombora ya masafa marefu ya ballistic.
Iran ilikataa. Mwezi Julai 2019, ilikiuka 3.67% ya kiwango cha urutubishaji wa madini ya uranium kilichokuwa kimekubaliwa na Januari mwaka huu ilitangaza kuwa imefufua tena urutubishaji wa uranium kwa 20%- kiwango cha uranium kinachotengeneza silaha ni 90%.
katika mahojiano na kituo cha Marekani hivi karibuni , Bw Biden aliulizwa iwapo ataondoa vikwazo vya kiuchumi ili kuieta Iran tena kwenye meza ya mazungumzo, na jibu lake lilikuwa ni ''Hapana''
Wakati huohuo, Ali Khamenei alisema kwamba kwa Iran kurejea katika utekelezaji wa ahadi zake chini ya mkataba, Marekani sharti kwamba "Ifute vikwazo vyote ", iliripoti televisheni ya taifa la Iran siku ya Jumapili.
"Tuta tathmini, na kama tutaona kwamba wamechukua hatua za uaminifu katika suala hili, tutarejea tena kutekeleza ahadi zetu," alisema na kuongeza kuwa: " Hatuwezi kujbadilisha msimamo huu na ni uamuzi wa mwisho na maafisa wote wa Iran wamekubaliana kuuhusu"
Alipoulizwa kuhusu hatua ya hivi karibuni ya Iran kuvunja makubaliano ya nyuklia, msemaji wa wizra ya mambo ya nje wa Marekani Ned Price aliwaambia waandishi wa habari kuwa : "Tunaendelea kuiomba Tehran kufufua utekelezaji wake mkataba wa nyuklia kwa ukamilifu.
"Tunaendela kufanya hivyo kwasababu hilo, kwetu ndio litakalofungua njia ya diplomasia. Na tuna matumaini kuweza kuchukua njia ya diplomasia ili kutatua kile ambacho tunakiangalia kama changamoto ya dharura."
Wazri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Mohammad javad Zarif awali alionya kupitia video kwamba'utawala mpya wa Washington kuna fursa ya kujaribu mbinu mpya, lakini muda uliopoi sasa unakaribia ukingoni".
" Karibuni serikali yangu italazimika kuchukua hatua kali katika kujibu hatua ya Wamarekani na Ulaya kushindwa kutekeleza majukumu yao waliyoyaahidi katika mkataba wa nyuklia ."