Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Watu wenye silaha wavamia shule ya Kagara na kuwateka wanafunzi wavulana
Watu wenye silaha wamemuua mwanafunzi mmoja na kuwateka nyara wengine 27 katika uvamizi dhidi ya shule yao ya kulala katika eneo la kati, kaskazini mwa Nigeria, amesema gavana Abubakar Sani Bello.
Wafanyakazi wa shule watatu na ndugu zao 12 na wawili pia walitekwa nyara katika tukio hilo lililotokea usiku, aliongeza.
Vikosi vya usalama vimepelekwa kusaidia katika shughuli za uokozi.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameamrisha vikosi vya nchi hiyo kufanya kila liwezekanalo kuwanusuru waliotekwa na jenge hilo
Jumatatu watu wapatao 20 waliokuwa njiani wakitoka katika sherehe za harusi walitekwa nyara wakati basi lao liliposhambuliwa katika jimbo la Niger.
Mwezi Disemba zaidi ya wanafunzi 300 wavulana walitekwa katika mji wa Kankara uliopo katika jimbo la kaskazini-magharibi la Katsina. Baadae waliachiliwa huru baada ya mazungumzo na watekaji wao.
Katika shambulio la hivi karibuni, watekaji nyara walikuwa wamevaa magwanda ya jeshi na kuvamia shule ya kulala ya wavulana wengi inayoendeshwa na serikali ya jimbo, kabla ya kuwachukua wanafunzi hao katika msitu uliopo karibu, Shirika la habari la AFP limekinukuu chanzo cha usalama ambacho hakikutajwa jina na afisa mmoja wakisema.
Bw Ubaidu ameiambia BBC kwamba baadhi ya watoto waliweza kutorokea katika misitu iliyopo karibu wakati shule yao ilipovamiwa, na sasa wanarejea.