Jinsi mzaha wa ulemavu ulivyoishia katika mahakama ya juu ya Canada

Iliyochapishwa

Muongo mmoja uliopita, kama sehemu ya kazi yake, mchekeshaji wa Canada alianza kuelezea tukio moja la uchekeshaji kumhusu muimbaji mmoja mwenye ulemevu. Hata hivyo mzaha wake huo uliishia mbele ya mahakama ya juu zaidi nchini Canada.

Jeremy Gabriel alizaliwa na ulemavu wa urithi unaofahamika kwa lugha ya kitaalamu kama Treacher Collins syndrome

Ulemavu huu ulimsababishia pia tatizo kubwa la kutoweza kusikia.

Licha ya haya, aliweza kutimiza ndoto yake ya kuwa muimbaji, na alikwenda kuwaimbia watu maarufu, kuanzia muimbaji Céline Dion hadi Papa Benedict wa XVI.

Amekuwa mtu maarufu katika alikozaliwa la Quebec.

Mwaka 2010, mchekeshaji maarufu kutoka jimbo hilo la Canada, Mike Ward, anayefahamika kwa ucheshaji wake ambao wakati mwingine huvuka mipaka na kuwashangaza wengi ,alitunga kichekesho cha dakika 90.

Zaidi ya kuzungumzia suala tata na zito la ubaguzi wa rangi alizungumzia kuhusu "ng'ombe watakatifu," alizungumzia mfumo wa watu maarufu katika jimbo-watu ambao, kwa maoni yake, ni matajiri sana na wenye nguvu sana, ambao hawawezi hata kucheka anapotoa vichekesho.

Athari za uchekeshaji wake zimedumu kwa takriban muongo. Hatahivyo vita vya kisheria kuhusu kisa cha kichekesho ambacho Ward alikielezea kumuhusu Gabriel ilisikilizwa katika mahakama ya juu zaidi ya Canada.

Kama sehemu ya uchekeshaji wake, Ward aliwalenga watu kama Céline Dion na marehemu mume wake, René Angélil, miongoni mwa watu wengine.

Pia alizungumzia kumuhusu Gabriel, ambaye wakati huo alikuwa anafahamika kama "Petit Jeremy" ambaye pia alikuwa ametoa albamu ya nyimbo.

Ward alisema kuwa aliamini kimakosa kwamba hali ya Gabriel ulikuwa ni ugonjwa unaoua. Alitoa mzaha kuhusu muonekana wa sura yake Gabriel na ulemavu wake.

Katika nyaraka za mahakama, bila sauti ya Ward, inaweza kuwa vigumu kuona ni kwanini hadhira inacheka, lakini walicheka, kusema kweli.

"Sikujua ningeweza kufika hapa na mzaha ule. Wakati mmoja nilijiambia mwenyewe umefika mbali na mzaha huu, wataacha kucheka. ' Lakini hapana, hawataacha kiucheka," anasema Ward.

Onyesho hilo la vichekesho lilichezwa moja kwa moja zaidi ya mara 200 kati ya mwaka 2010 na 2013 na likawekwa kwenye intaneti.

Gabriel kwa mara ya kwanza alikabiliwa na athari za uchekeshaji wa Ward 2010, alipokuwa na umri wa miaka 13 alipokuwa akianzashule ya sekondari . Alinyanyaswa na uchekeshaji wa Ward ulichochea zaidi kunyanyaswa kwake .

"Nisingeweza kumaliza siku bila kuambiwa mojawapo ya mzaha wake," anasema Gabriel mwenye umri wa miaka 24.

Alijihisi kuhusishwa na utani wa Ward kutokana na ulemavu wake na akaanza kujitenga kijamii na kuanza kufikiria hata kuhusu kujiua. Familia ya Gabriel haikuwahi kuwasiliana na familia ya mchekeshaji mara moja.

"Kwasababu ya aina ya vichekesho, kwasababu ya kile kilichokuwa kikisemwa, tulifikiria kuwa wangetupuunza ," anasema Gabriel.

Halafu katika mwaka 2012, walimsikia Ward akizungumzia kuhusu kichekesho katika kipindi maarufu cha televisheni.

"Akijilinganisha binafsi na mraibu wa mihadarati aina ya cocaine, alisema kuwa anahitaji kufanya vichekesho ambavyo vinafika mbali ," zilieleza nyaraka za mahakama.

Wakati huo ndipo familia yake iliwasilisha malalamiko kuhusu uvunjaji wa haki za binadamu dhdii ya mtoto wao.

Wakati kesi ya Ward ilipofikishwa mbele ya mahakama ya Haki za binadamu ya Quebec, mahakama inayoshugulikia kesi zinazohusiana na ubaguzi au unyanyasaji chini ya muswada wa kijimbo wa haki, mchekeshaji huyo alishindwa katika kesi hiyo.

Zaidi ya uhuru wa kujieleza

Mahakama ilibaini kuwa alikwa "amevuka ukomo wa uhuru wa kujieleza " na kwamba vichekesho vyake vilikuwa ni vya kibaguzi kwasbabu ya ulemavu aliokuwa nao.

Alikata rufaa na, akakata rufaa, lakini mwaka 2019 mahakama ya rufaa ikapitisha uamuzi wa awali pamoja na kutozwa faini ya dola 27,500 ambazo alipewa Gabriel kwa kumdhalilisha utu wake.

Nia ya mahakama "si kuzuia ubunifu au kuzuia uhuru wa kujieleza kwa wasanii ," , ilisema mahakama, bali " wachekeshaji, sawa na mwananchi yeyote mwingine, wanawajibika kwa athari za maneno yao wakati wanapovuka mistari fulani ."

Ward alikua tayari ameamua kuwa kama angeshindwa katika kesi hiyo, angeendelea na mapambano yake ya kudai haki katika Mahakama Kuu ya Canada.

"Uchekeshaji sio uhalifu," alisema katika taarifa iliyotolewa baada ya umamuzi wa mahakama ya rufaa kutangazwa. "Katika nchi ''huru'', haipaswi kuwa jukumu la jaji kuamua ni aina gani ya mzaha inayopaswa kutolewa katika jukwaani ."

Alisema kuwa kicheko cha umati "kilijibu swali hilo."

Ward amesema kuwa anakataa kulipa gharama alizoamrishwa na mahakama : "sio mimi, lakini kwa ajili ya wachekeshaji wachanga, wachekeshaji wa kesho."Alidai kwamba ni suala la kimsingi kwa biashara kuwa mchekeshaji anaweza kutoa mzaha unaoweza kuwa wa hatari.

Na ameshikilia msimamo wake kuwa Gabriel alikuwa ni mtu anayefahamika kwa umma kwa hiyo ni mtu ambaye anaweza kufanyiwa mzaha.

Gabriel, harahivyo, alijibu kuwa : "Kuwa mtu maarufu kwa umma haimaanishi kuwa hauna haki tena."

"Mstari umefungwa, Ninaamini katika hilo,"aliongeza.