Mashitaka dhidi ya Trump Trump: Shitaka la uasi ni 'uongo wa ukatili '

Chanzo cha picha, Reuters
Shitaka la uchochezi dhidi ya Trump ' uongo wa ukatili ' ", walisema mawakili wa Trump walipokuwa wakitoa ushahidi katika bunge la Seneti la Marekani.
Wakili Michael van der Veen alitaja vikao vya mashitaka dhidi ya rais wa zamani "vyenye uchochezi wa kisiasa na vilivyojaa hila" vya Wademocrats.
Bw Trump anashutumiwa kwa kusababisha ghasia katika jengo la Seneti ,Capitol mnamo tarehe 6 Januari ambazo ziliwauwa watu watano. Anakanusha mashitaka hayo.
Warepublican wengi wameashiria kuwa hawatapiga kura ya kumtia hatiani Bw Trump.
Timu ya mawakili wa utetezi walitumia chini ya saa nne kati ya saa 16 walizopewa, wakijaribu kuhakikisha kesi ya kumshitaki mteja wao inamalizika haraka.
Baada ya hayo, m,aesenta walipewa saa nne za kuuliza maswali kwa pande zote mbili.
Awali, walikaa kwa muda wa siku mbili kusikiliza ushahidi wa dakika kwa dakika wakisikiliza video na sauti zilizorekodiwa , Wademocrat wakijaribu kuonesha kuwa Donald Trump alichochea ghasia, hakufanya lolote siku hiyo kuzuia maandamano ya ghasia na hakuonesha kujuta.
Walidai kuwa kumuachilia huru kunaweza kusababisha kutokea kwa shambulio sawa na hilo dhidi ya Congress.
Trump anajitetea vipi ?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ijumaa, wakili wake Bw van der Veen alitumia hotuba yake ya ufunguzi akipinga tuhuma za Wademocrat kwamba Bw Trump alichochea ghasia wakati wa hotuba yake kwa wafuasi wake tarehe 6 Januari mjini Washington DC kujaribu kuzuia kuidhinishwa kwa ushindi wa Joe Biden.
Bw Trump alikuwa ametoa madai ya kuwepo kwa udanganyifu wa kura na akawataka wafuasi wake kukusanyika katika jengo la Capitol muda mfupi kabla ya kuibuka kwa ghasia.
Hatahivyo, ukweli ni kwamba ushahidi miongoni mwa makundi kwamba ghasia zilikua zimeopangwa mapema uliodhihirika ni "ni madai ya upuuzi kwamba dhidi ya rais wa zamanikwamba alichochea ghasia", Bw van der Veen alisema na kuongeza kuwa : "Huwezi kuchochea kile ambacho tayari kingetokea."
" Kudai kwamba rais kwa namna yoyote ile alitamani, alikuwa na nia au alichochea mwenendo wa ghasia ni ujinga na uongo wa ukatili. Ukweli ni kwamba, jumbe mbli alizozituma rais kupitia Twitter wakati ghasia zipoanza katika Capitol zilizkua ' Kaa kwa amani' na "Hakuna ghasiakwasababu sisi ni chama chenye sheria ,'" alisema wakili wa Trump.
Kuambia umati kuwa walitakiwa "kupigana kadri ya uwezo wao" ilikuwa ni hotuba tu ya kisiasa , Bw van der Veen alisema
Msifanye makosa , aliwaambia maseneta, "juhudi hizi za kutaka kupaka matope, kudhibiti na kufuta si tu Rais Trump, bali Wamarekani milioni 75waliompigia kura".

Wakili pia alidai kuwa Bw Trump alikuwa na haki ya kisheria ya kupinga matokeo ya uchaguzi.
"Katika miaka iliyopita matais wengine kadhaa walitumia mchaka unaofanana nahuu ku[pinga matokeo yao ya uchaguzi ," Bw van der Veen alisema, kabla ya kuonyesha sauti zilizorekodiwa na kuhaririwa kutoka mwaka 2017 wakati Wademocrat walipopinga matokeo ya uchaguzi yaliyompatia ushindi Bw Trump.

Mameneja wa mashitaka walikua na matumaini kuwa picha za maandamano na ghasia, za kutoroka kwa wabunge na makabiliano kati ya polisi na waandamanaji vitainua hoja yao kwamba Bw Trump alichochea ghasia.
Mwendesha mshitaka wa seneti Joe Neguse alitoa hoja kwamba Bw Trump hakuwa "tu mtu fulani wakawaida " alipotoa hotuba yenye tata -alikuwa ni rais aliyekuwa anawahutubia wafuasi wake ambao "walifanya ghasia na kuwatazama ".
Seneta Jamie Raskin alisema "Wenzangu, kuna kiongozi yeyote wa kisiasa katika chumba hiki anayeamini kwamba kuwa aliwahi wakati wowote kuruhusiwa na Seneti kurejea katikaofisi ya rais- Oval, Donald Trump angezuia uchochezi wa ghasia kiasi kile?"
Mbunge wa Congress Ted Lieu alisema: "mashitaka, kupatikana na hatia , na kuzuiawa kurejea mamlakani tena ni sio jambo tu la wakati uliopita .Linahusu siku zijazo. Ni kuhakiksha kuwa hakuna afisa mwingine wa siku za usoni, hakuna rais ajaye anayefanya sawa na kitu hiki ."
Nini kitakachotokea?
Republicans wanaweza kumuokoa Trump kutoondolewa madarakani kwa sababu wana idadi ya kutosha ya kuweza kumkingia kifua.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mbili ya Tatu ya viti vya bunge la seneti ni upande wa rais , hivyo kati ya viti 100- maseneti, 67 wanahitaji kupiga kura ili Trump aweze kupata ushindi.
Lakini kuna viti 45 vya Democrats, wawili hawana chama na Republican 53, rais ana nafasi kubwa ya kushinda.
Hatua hii haimuweki Trump katika hatari ya kuondolewa madarakani, lakini akiondolewa madarakani basi makamu Mike Pence ndio ataapishwa kuwa rais.












