Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Polisi nchini Nigeria wanatafuta genge la vijana walioonekana kwenye video wakiwapiga wasichana
Polisi katika jimbo la Nigeria la Bauchi imesema kuwa imeanza uchunguzi juu ya video iliyosambaa na kuibua hisia kali kwenye mitandao ya kijamii iliyoonesha jenge la vijana waliokua wakiwatesa wasichana.
Video hiyo ilionesha genge la vijana lililoonekana kuwateka wasichana katibu 10 katika jingo moja ambalo halijamalizwa kujengwa huku wakiwapiga kwa ukatili kwa viboko vingi mfulurizo na kuwachapa mateke.
Wasichana hao ambao wanakadiriwa kuwa na miaka kati ya kumi na minane na zaidi ya 20, walionekana wakipiga mayowe na kulia kwa huzuni kubwa, huku wakiwaomba watesaji wao wawahurumie.
Waathiriwa wameombwa na polisi kufika kwenye kituo cha polisi kutoa taarifa ambazo zitasaidia kuwakamata na kuwashitaki wahusika.
Polisi imelaani ukatili huo na kuapa kuwasaka wahusika na kuwafikisha mbele ya sheria.
Video ilionesha nini?
Video ilionesha kikundi cha vijana wadogo wakiwachapa kikundi cha wasichana
Katika vido hiyo iliyoangaliwa na BBC, vijana hao wanaonekana wakiwapiga wasichana huku wakipiga kelele.
Wakati mwingime wasichana walionekana wakiomba msamaha huku wakilia kwa uchungu, lakini vijana hao waliendelea kuwapiga viboko na hakuna aliyejaribu kuwazuia.
Baadhi ya watazamani wa video hiyo walihesabu idadi ya viboko alivyopigwa kila msichana na kufikia hadi viboko 10 na kugeuzwa tena upande wa pili na kutandikwa vingine zaidi.
Msichana mmoja aliyejaribu kutoroka alipigwa viboko katikati ya miguu yake, huku mwingine akisiskika akipiga mayowe "Toka kwenye masikio yangu, usinishike hapa".
Polis waliongeza kuwa baada ya genge la vijana hao kuwachapa wasichana, walinyoa nywele zao kwa wembe, kuwatukana matusi makubwa na kuwadhalilisha.
"Watu wetu tayari wameanza uchunguzi, na vijana hawa watakamatwa hivi karibuni na kupelekwa mbele ya sheria .
"Ukiukaji wa aina hiyo wa haki za binadamu ni jambo la kusikitisha, ni jambo la ubaguzi wa jinsia ," ilisema taarifa ya polisi.
Iliongeza kuwa : "Kila mwanamke anayo haki ya kuishi kwa heshima-na kuhisi kuwa hana uoga, kutukanwa au kuteswa, na tutahakikisha kwamba kikosi cha jimbo la Bauchi kinahakikisha mambo kama haya yanashugulikiwa kulingana kisheria . "
Wasichana walifanya nini?
Taarifa zinasema kuwa genge la vijana hao liliwafanyia ukatili wasichana kwa kuwashuku kuwa walikua wazururaji katika kile kinachofahamika jimboni humo kama "jioni njema," katika eneo la Dumi Gate .
Hata katika video hiyo wanasikika wakiwaonya wasichana kwamba wanaadhibiwa kwa makossa waliyoyafanya.
Baadhi ya wakazi wa jimbo la Bauchi waliozungumza na BBC wanasema eneo hilo ni maarufu sana kwa vitendoi vya ukatili.
Wameithibitisha kuwa kamati sasa imeundwa kwa ajili ya kutatua tatizo la usalama wa raia katika eneo hilo.
Lakini watu wanahoji juu ya ikiwa vijana wana haki ya kuwahukumu vijana wenzao wa kike kwa makossa wanayowatuhumu?.
Chini ya sheria ya Nigeria, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kujichukuli sheria mkononi kwa uhalifu wowote ule aliofanya mtu.
Nchini Nigeria, tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi mara nyingi husababisha hata watu kupoteza maisha yao. Mwaka jana pia Wanageri waligadhabishwa na mauaji ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka 22, Uwavera Omozuwa aliyeuawa kanisani.
Kampeni ya hashtag #JusticeForUwa au # HakiKwaUwa ilienea kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria, huku familia yake ikiomba msaada wa kumtafuta aliemuua.
Uwavera alikua anajisomea katika kanisa "tulivu" karibu na nyumbani Benin City wakati alipouawa, dada yake, Judith, aliiambia BBC idhaa ya Pidgin.
Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa muuguzi alikufa hospitalini, siku tatu baada kushambuliwa.