Navalny: Maelfu waandamana kupinga kufungwa kwa mpinzani wa Putin

Chanzo cha picha, Reuters
Maelfu ya raia wa Urusi wameshiriki maandamano ambayo hayakuidhinishwa na mamlaka nchini Urusi kudai kuachiliwa huru kwa kiongozi wa upinzani aliyefungwa jela Alexei Navalny.
Zaidi ya watu 5,000 wamezuiliwa, kikundi kimoja kinachofuatilia matukio nchini humo kimesema.
Bwana Navalny alifungwa jela aliporejea nchini Urusi baada ya kupona jaribio la kuuliwa kwa sumu kwa kutumia kemikali inayoathiri neva.
Bwana Navalny amelaumu huduma za usalama kwa shambulio hilo lakini Kremlin imekanusha madai hayo.
Mpinzani huyo wa serikali ya Urusi alitakamtwa baada ya kuwasili kutoka Ujerumani alipokuwa akipata matibabu kwa miezi kadhaa mara baada ya tukio hilo ambalo nusra limsababishie kifo.

Chanzo cha picha, Reuters
Unaweza pia kusoma:
Mamlaka ya nchini Urusi inasema kuwa alipaswa kuripoti polisi kila wakati kwasababu ya kesi yake ya ubadhilifu wa mali ya umma iliyoahirishwa.
Bw Navalny amepinga kukamatwa kwake jambo ambalo anasema "ni ukiukaji wa sheria ", na kuongeza kuwa mamlaka zimruhusu kusafiri hadi Ujerumani kupata matibabu kutokana na sumu ya Novichok, ambayo alipewa Urusi mnamo mwezi Agosti mwaka jana.

Chanzo cha picha, Reuters
Bwana Navalny amelaumu maajenti wa vikosi vya usalama chini ya maagizo ya Rais Putin kwa jaribio la kumuua na waandishi wa habari za uchunguzi, wametaja maafisa wa kijasusi wa Urusi kama washukiwa wa utekelezaji wa tukio hilo la sumu.
Hata hivyo, Kremlin imekanusha kuhusika na kutupilia mbali hitimisho la wataalamu wa nchi za magharibi kuwa sumu ya Novichok ilitumika katika jaribio la kumuua.
Wakati huohuo, Rais wa Urusi Vladimir Putin amekanusha taarifa kuwa yeye ndio mmiliki wa mgahawa uliopo katika eneo la Bahari nyeusi, kama inavyodaiwa na Bwana Navalny katika video ambayo imesambaa katika mitandao ya kijamii nchini Urusi na imetazamwa zaidi ya mara 100.
Nini kinachoendelea kwa sasa?
Mjini Moscow mwandishi wa BBC Sarah Rainsford anasema waandamanaji wamekuwa wakicheza mchezo wa paka na panya na polisi, wakiandamana hadi karibu na maafisa wa polisi kabla ya kurudi nyuma wakihofia usalama wao.
Wakati mmoja polisi waliwavuta waandamanaji kupitia ukuta wao walioujenga kama njia ya kukabiliana na ghasia.
Picha za video zilionesha watu kadhaa wakisindikizwa kwenye vituo vya mabasi na polisi.
Hata hivyo, waandamanaji walijaribu kufikia gereza la Matrosskaya Tishina ambako Bwana Navalny anashikiliwa.
Mke wake Navalny Yulia Navalnaya ni miongoni mwa wale waliokamatwa katika maandamano ya Jumapili lakini baadaye akaachiwa huru.
Kabla ya maandamano hayo alituma ujumbe katika mtandao wa Instagram na kusema: "ikiwa tutanyamaza, wanaweza kutufuata na sisi kesho."
Polisi inasema maandamano hayo ni kinyume cha sheria, huku mamlaka za Urusi zikionya kuwa maandamano yanaweza kusambaza virusi vya corona.
Muandamanaji mwenye umri wa miaka 40 mjini Moscow ameliambia Shirika la habari la Reuters kuwa amehudhuria maandamano licha ya kuwa alifahamu anawezaka kushambuliwa kwa kushiriki maandamano.
"Ninaelewa fika kwamba ninaishi katika taifa ambalo halina sheria. Katika taifa la kipolisi, ambalo halina mahakama huru. Katika nchi inayotawaliwa na ufisadi. Ningependa kuishi tofauti ," alisema.
Maandamano yanayomuunga mkono Bwana Navalny pia yalifanyika mashariki mwa Urusi. Katika mji wa Siberian wa Novosibirsk, watu karibu 2,000 waliandamana katika mji huo huku wakipaza sauti na kusema "Uhuru" na "Putin ni mwizi".
Huko Yakutsk ambako nyuzi joto ilishuka hadi -40, mwandamanaji kwa jina Ivan alisema ni mara yake ya kwanza kushiriki maandamano.

Chanzo cha picha, Reuters
Katika mji wa Vladivostok, mashariki mwa Urusi, washirika wa Bw Navalny wanasema hakujawahi kufanyika maandamano kama yaliyotokea Jumamosi kwa kipindi cha mwongo mmoja.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Bw. Navalny anawalaumu maafisa wa usalama wa taifa kwa kutekeleza maagizo ya Bw Putin kwa kumshambulia n kwa sumu ya Novichok ambayo ilikaribia kumuua. Waandishi wa habari wa taarifa za uchunguzi kutoka Bellingcat waliwataja maafisa wa Shirika la upelelezi la Urusi wanaoshukiwa kumpa sumu Bw Navanly.
Utawala wa Kremlin unakanusha kuhusika shambulio hilo la sunu na unapinga matokeo ya uchunguzi ya wataalamu wa silaha kutoka nchi za Magharibi, waliosema kwamba sumu ya Novichok ilitumika dhidi ya Navanly.












