Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini mwaka wa 2021 utakuwa na siku chache kwa miongo kadhaa?
Haukutambua , lakini baadhi ya siku katika mwaka wa 2020 dunia ilikuwa ikizunguka kwa kasi zaidi ya ilivyo kawaida na kuna hesabu zinazoonesha kwamba mwaka 2021 sayari hii itafuata mkondo huohuo wa kasi.
Huwezi kugundua kwasababu kasi hiyo ni ndogo ya kiwango cha milisekunde. Lakini mashirika ya kimataifa kama vile IERS inayohusika na upimaji wa mzunguko wa dunia husajili tofauti hiyo ya mzunguko .
Jumla ya mizunguko ya siku fupi ikilinganishwa na siku nyingine katika kipindi chote cha mwaka 2020, ilichukua milisekunde 1.28 chini ya ilivyotarajiwa. Kulingana na Date and Time , tovuti ya vyanzo vinavyopima wakati na wakati wa maeneo, mwaka 2021 pia utakuwa na siku fupi na utakuwa mfupi zaidi ya 2020.
Utazunguka kwa kasi ya jumla ya milisekunde 35.40 chini.
Je mzunguko huo wa kasi husababishwa na nini? Na je unamaanisha kwamba kuanzia sasa dunia itazunguka kwa haraka zaidi?
Ni nini kilichotokea mwaka 2020 na ni nini kitakachokuwa mwaka 2021
Urefu wa siku duniani ni sawa na muda wa mzunguko wake ama jinsi dunia inavyopinduka katika mhimili wake.
Kwa siku dunia hutakiwa kuchukua sekunde 86,400 ikiwa ni idadi ya sekunde katika dakika 14440 ama saa 24.
Dunia hukamilisha mzunguko wake katika saa 24. Kuna siku ambapo dunia huzunguka kwa muda wa saa 24 kwa siku , anasema Graham Jones katika Time and Date akizungumza na BBCMundo.
"Lakini vipimo hivi hutofautiana na sekunde chache .
Kwamba mara nyingine mzunguko huo huongezeka kwa milisekunde chache au zaidi.
Hadi kufikia mwaka 2020, siku fupi zaidi iliorekodiwa ilikuwa tarehe 5 Julai 2005 ambayo ilikuwa na mzunguko wa milisekunde 1.0516 zikiwa ni chache zaidi.
Lakini mwaka 2020, kulikuwa na siku 28 ambazo zilikuwa fupi zaidi ya siku fupi ya mwaka 2005.
Siku fupi zaidi iliorekodiwa mwaka 2020 ilikuwa Julai tarehe 19 na ilichukua muda wa milisekunde 1.46,02 chini ya sekunde 86.400 kulingana na shirika la Time and Date ambazo zilikusanywa na vipimo vya IERS.
Kutokana na hilo , mwaka wote 2020 ulizunguka milisekunde 1.28 chache ya inavyotarajiwa.
Kwa wastani siku hizo zitakuwa milisekunde 0.10 fupi zaidi ya milisekunde 86,400 zilizotarajiwa na kwamba mwaka mzima, dunia itakua imezunguka milisekunde 35.40 chache zaidi.
Mwaka 2021 unatarajiwa kuwa mfupi zaidi katika muongo huu.
Mara ya mwisho wastani na urefu wa siku zote katika mwaka mmoja ulipokuwa mfupi kwa sekunde 86,400 ilikuwa mwaka 1937 kulingana na tovuti ya Time and Date.
Inapaswa kufahamika kwamba matokeo hayo kuhusu urefu wa mwaka hupatikana kwa kujumlisha muda wa mzunguko wa dunia wa siku 365 au siku 366.
Lakini muda unaochukuliwa na mzunguko wa dunia kwa mwaka hautegemei mzunguko lakini muhimili wake katika jua.
Mzunguko huo una udhabiti zaidi ya ule mzunguko wa kawaida, kulingana na Christian Bozourd wa shirika linalochunguza mizunguko ya dunia kutoka mjini Paris.
Lakini ni kwa muda gani dunia itaendelea kuzunguka kwa kiwango hiki?
Je kasi hiyo itachukua muda gani?
Tunapotazama nyuma kuna muda ambapo dunia huzunguka kwa kasi na wakati ambapo huzunguka polepole.
Tunaamini kwamba hili limekuwa likitokea kwa mamilioni ya miaka , lakini kwa tofauti ndogo sana ,Jones aliambia BBC Mundo.
Kila mara mzunguko wa dunia huongeza sekunde chache.
Kasi hiyo ilianza 1990, kulingana na Bizourd wa shirika la IERS.
Amesema kwamba kasi hiyo itaendelea kuwepo kwa mwaka mmoja zaidi kwasababu mzunguko wa mwendo pole umechukua takriban miaka 7 , kulingana na watalaamu wa IERS"
Jones wa Time and Date anakubali kwamba kasi hiyo itaendelea mwaka 2021 , ijapokuwa pia yeye hajui itachukua muda gani.
''Katika kipindi fulani mzunguko huo utapunguza kasi tena'' , anasema.
Lakini ni nini haswa kinachosabisha dunia kuongeza kasi ?
"Kwa mizani ya muda wa miongo (kati ya miaka 10 na 100), urefu wa siku unaonyesha tofauti zisizo za kawaida", anasema Christian Bizouard akizunguma na BBCMundo.
Wanasayansi wanakubali kwamba mabadiliko haya yanatokana na mwingiliano wa sababu kama vile shughuli ya kiini cha sayari iliyoyeyuka au mwendo wa bahari na anga, kulingana na Jones na Bizouard akizunguma na BBC Mundo.
Lakini ukweli ni kwamba vyanzo vya tofauti hiyo havieleweki anasema Bizouard
Jones pia anatambua kwamba wataalamu hawajui haswa kwanini dunia huongeza kasi inapozunguka ama hata kupunguza kasi hiyo kwa kipindi cha muda mrefu.
Lakini kwa jumla , kwa upande wa Jones , Inashangaza jinsi dunia ilivyo sawa katika saa zinazotumika duniani kwasababu hupoteza milisekunde chache tu.
Kipi kitafanyika iwapo dunia itapunguza kasi zaidi ama kuongeza zaidi?
Ijapokuwa muda unaoongezeka ama kupungua ni mchache zaidi , mabadiliko ya mzunguko wa dunia huenda yakaongezeka kwa miaka kadhaa na kusababisha muda wetu kwenda mbele ama kurudi nyuma kwa sekunde.
Sababu kama vile shughuli ya msingi ya Dunia, bahari na anga huathiri urefu wa siku Duniani.
Kusuluhisha kutokulingana, wanasayansi wametumia kile kinachoitwa "leap" tangu 1973, ambayo inaweza kuwa chanya au hasi.
Sekunde hii inaweza kuongezwa kwa saa zetu wakati Dunia iko nyuma, au inaweza kuondolewa wakati sayari hii itamaliza mizunguko yake kwa muda mfupi kuliko kawaida.
Tangu 1973, IERS imeongeza sekunde 27 za kuruka kwa wakati rasmi wa saa za Dunia.
"Ikiwa siku fupi zinaendelea, wakati fulani tunaweza kuhitaji kuruka hasi kwa pili, ambayo ni kusema, kuchukua sekunde ya saa zetu kuzoea mzunguko wa kasi wa Dunia," anasema Jones.
"Lakini tunaweza kuhitaji au tusiihitaji. Hatujui ikiwa itatokea kwa sababu hatujui mwenendo huu utadumu kwa muda gani ," anaongeza.