Virusi vya corona: Jinsi maradhi hayo yalivyovuruga sherehe za mwaka mpya duniani

Chanzo cha picha, EPA
Vizuizi vimewekwa dhidi ya sherehe za mwaka mpya katika maeneo tofauti duniana wakati nchi nyingi zinajizatiti kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya coronaona.
Onyesho la fataki na mikusanyiko ya watu ilipigwa marufuku kuanzia Sydney hadi New York.
Sherehe pia zimezimwa hususan barani Ulaya baada ya aina mpya ya ugonjwa ambao maambukizi yake yanasambaa kwa kasi kugunduliwa
Ufaransa iliweka zaidi ya polisi 100,000 kushika doria katika barabara za mji mkuu mkesha wa mwaka mpya ili kuhakikisha amri ya kutotoka nje nyakati za usiku zinazingatiwa.
Zaidi ya watu milioni 1.8 wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona tangu janga hilo lilipoanza mwaka mmoja uliopita.
Zaidi ya watu milioni 81 wameripotiwa kuambukizwa virusi vya corona
Ni nini kilifanyika Ulaya?
Nchini Ufaransa, serikali iliamuru uwepo wa usalama katika maeneo ya mijini kutoka 20:00 (19:00 GMT) Alhamisi, wakati amri ya kutotoka nje ilipoanza.
Katika mji wa Paris nusu ya usafiri wa metro ilifungwa.
Ufaransa ilikuwa imeweka amri ya kutotoka nje huku mabaa, migahawa na maeneo ya vivutio vya watu yakisalia kufungwa walipokaribisha mwaka mpya
Katika hotuba yake ya mwaka mpya, Rais Emmanuel Macron aliwaangazia wakosoaji wanaolalamikia kujikokota kwa mpango wa kutoa chanjo, na kuapa kushughulikia suala hilo katika "muda unaostahili".
Nchini Uingereza - ambako virusi vipya vya corona vinavyosambaa kwa kasi vimegunduliwa huku watu milioni 20 wakiathiriwa zaidi katika eneo hilo watu wamelazimika kusalia majumbani mwao - Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa wito wa watu kuzingatia masharti yaliyowekwa.
Barabara za mji wa London zilikuwa kimya mkesha wa mwaka mpya baada ya polisi kuomba watu washerehekee majumbani mwao.
Badala ya sherehe za kawaida zinazojumuisha mikusanyiko ya watu jijini London, onyesho la fataki lilifanywa katika maeneo tofauti jijini humo.
Ireland iliongeza vikwazo zaidi siku ya Alhamisi, kwa kupiga marufuku watu kutembeleana majumbani na kufunga maduka ambayo hayauzi bidhaa muhimu na kudhibiti usafiri wa hadi kilomita 5.
Ujerumani kwanza sasa imeweka amri ya kutotoka nje hadi Januari 10. Serikali imepiga marufuku uuzaji wa fataki na kuweka vikwazo vikali vya kudhibiti idadi ya watu wanaokusanyika pamoja.
Katika hotuba yake ya mwaka mpya inayotazamiwa kuwa ya mwisho kwake kama kansela wa Ujerumani, Angela Merkel aliwaangazia watu wanaopotosha umma kuhusiana na janga hilo.
Alisema anashangazwa na jinsi uwongo wa kijinga na wa kikatili unavyotumiwa bila kujali hisia za wale waliyopoteza wapendwa wao kutokana na ugonjwa wa corona
Nchini Italia, amri ya kutotoka nje iliwekwa saa 22:00 huku mabaa, migahawa na maduka mengi kufungwa. Huku hayo yakijiri Papa Francis hakuongoza ibada ya mwaka mpya mjini Rome badala ya kupata maumivu ya nyonga sugu.
Uholanzi pia iko nchini ya amri ya kutotoka nje ambayo itaendelea kudumishwa hadi Januari 19.
Uturuki imeanza kutekeleza amri ya kutotoka nje kwa siku nne
Na Marekani?
Maafisa wameweka vikwazo vya kudhibiti sherehe za mwaka mpya katika majimbo mengi na miji ya nchi hiyo.
Mjini New York, mpira wa mraba wa taa utawashwa wakati wa kuvuka mwaka lakini eneo hilo halitakuwa wazi kwa umma

Chanzo cha picha, Reuters
Kikundi kidogo cha wafanya kazi wa kutoa huduma za afya ambao wanajulikana kama''shujaa wa 2020''. Na familia zao wataruhusiwa kuingia kama wageni maalum katika maeneo yaliyotengwa
Fataki zilipigwa marufuku katika miji tofauti ikiwemo San Francisco na Las Vegas.
Katika hotuba yake ya mwaka mpya iliyowekwa kwenye Twitter, Rais Donald Trump alipongeza kati ya utengenezaji chanjo kama ''miujiza ya kimatibabu'' na kupongeza juhudi za Operation Warp Speed, mpango wa Marekani unaolenga kutengeza na kuwasilisha chanjo
Lakini hakuwataja Wamarekani karibu 350,000 waliofariki kutokana na corona.
Nchi za Asia-Pasifiki zimeathiriwa vipi?
Nchi ya kwanza inayokujia akilini ukitaja mwaka mpya ilikuwa Australia. Maonyesho ya fataki ya Sydney yalifanywa kama kawaida lakini watu hawakuruhusiwa kukusanyika kujionea kama ilivyo ada .
"Hatutaki kuwa na hafla ambayo itasambaza virusi mkesha wa mwaka mpya," Waziri mkuu wa New South Wales Gladys Berejiklian alisema.
Wakazi Wengi wa Sydney walifuatilia onyesho hilo kwenye televisheni zao nyumbani, ambako watu watano tu waliruhusiwa kuwa pamoja.

Chanzo cha picha, EPA
China, tamasha la mwangaza linalofanyika kila mwaka katika mji mkuu wa Beijing lilifutiliwa mbali. Lakini katika mji wa Wuhan, ambao unadhaniwa kuwa chimbuko la janga la corona, maelfu ya watu walikusanyika katikati ya mji huo kusherehekea huku vibofu vikiachiliwa angani.
Japan ilifuta sherehe za jadi za kukaribisha mwaka mpya ambayo Emperor Naruhito na familia yake ilikuwa iwasalimie watu.
Nchini India, Delhi na miji mingine kadhaa, amri ya kutotoka nje usiku na masharti mengine ya kuzuia mikusanyiko mikubwa ya watu wakati wa mwaka mpya iliwekwa
Hata hivyo nchini New Zealand, ambako amri kali ya kutotoka nje na kufungwa kwa mipaka iliwekwa kumesaidia kuangamiza ugonjwa wa corona, sherehe za kuukaribisha mwaka maya ziliandaliwa kama kawaida.












