Watu kote duniani wanasherehekea siku kuu ya krisimasi mojawapo ya siku takatifu duniani katika kalenda ya Wakristo.
Lakini ibada za mwaka huu makanisani na matukio yake yanahudhuriwa na watu wachache kutokana na mlipuko wa virusi vya corona .
Kukaa mbali na kuvaa barakoa kwa sasa ni lazima.
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Nchini Australia mavazi ya Krisimasi ndio yaliotumika katika ufukwe wa bahari wa Bondi
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Papa Francis aliongoza mkesha wa siku kuu ya Krisimasi katika kanisa la St Peter's Basilica mjini Vatican kabla ya waliohudhuria kupunguzwa
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Papa Francis amesema kwamba sikuu ya Krisimasi ulikuwa muda sio wa kuomba msamaha bali kuwapatia faraja wengine
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Ibada ya usiku ambayo ni maarufu ilifanyika mapema kutokana na masharti ya kutotoka nje usiku . Takriban watu 100 walihudhuria hafla hiyo
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Nchini India, watoto waliwasha mishumaa katika lango la kanisa la Sacred Heart Cathedral mjini Delhi
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Wanawake hawa waliomba polepole wakati wa ibada hiyo iliofanyika katika kania la St Andrew mjini Karachi, Pakistan
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Nchini Uingereza , wakaazi wa kijiji cha Woodend, Northamptonshire, walipamba nyumba zao kabla ya siku kuu ya Krisimasi
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Nchini Iraq, watu walikongamana kando ya moto wakati wa Ibada iliofanyika katika kanisa la Virgin Mary Church mjini Baghdad
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Na kulikuwa na shangwe na vigelegele katika kituo hiki cha wazee katika eneo la Santiago nchini Uhispania