Jeshi la Ethiopia 'lawaua washukiwa 40' kufuatia mauaji ya mamia Benishangul-Gumuz

Iliyochapishwa

Jeshi la Ethiopia limewaua zaidi ya watu 40 wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya zaidi ya watu 100 ikiwemo watoto katika eneo la Benishangul-Gumuz , vyombo vya habari vimesema.

Maafisa watano wa serikali ya sasa na wenzao wa zamani pia walikamatwa kufuatia tatizo hilo la kiusalama , ripoti zimeongeza.

Washukiwa hao walichoma nyumba za wanavijiji waliokuwa wamelala kuwapiga risasi na kuwachoma visu wakati wa shambulio hilo la siku ya Jumatano.

Shambulio hilo linajiri siku moja baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed kuzuru eneo hilo.

Haijulikani washambuliaji ni akina nani lakini walionekana kulenga jamii za makabila madogo yaliowasili na kuishi katika eneo hilo , kulingana na Amnesty International.

Ethiopia imeshuhudia ongezeko la ghasia za kisiasa, kikabila na kidini katika miaka ya hivi karibuni.

Ilikuwa na idadi kubwa ya watu waliowacha bila makao barani Afrika 2018 takriban watu milioni 1.8.

Mizozo kwa kiwango kikubwa imechochewa na makundi yanayopigania ardhi zaidi na uwezo wakijaribu kuwafukuza watu wanaodaiw kutoka sehemu nyengine.

Mr Abiy alielezea mauaji hayo kama ya kusitisha na kusema kwamba serikali yake imetuma wanajeshi katika eneo hilo ili kutafuta suluhu ya mzozo huo.

Vyombo vya habari vya serikali havikutoa utambuzi wa watu hao 42 katika operesheni hiyo ya kuwasaka washambuliaji.

Vilisema kwamba silaha ikiwemo mishale ilikamatwa ilisema ripoti ripoti hiyo.

Naibu waziri wa serikali ni miongoni mwa watu watano waliokamatwa vilisema vyombo vya habari vya serikali.

Miongoni mwa watu hao watano waliodaiwa kuhusika na mzozo huo huku wengine walikamatwa kwasababu hawakufanya jukumu lao , ripoti hizo zilisema.

Ni nini kilichotokea wakati wa shambulio hilo?

Msemaji wa tume ya haki za kibinadamu inayoendeshwa na serikali aliambia BBC kwamba wapiganaji walitekeleza shambulio hilo katika eneo la magharibi mwa Benishangul-Gamuz mwendo wa saa kumi siku ya Jumatano.

''Walivamia kijiji kimoja na huku waathiriwa wakiwa wamelala walizichoma nyumba zao na pia waliwapiga risasi raia '', Aaron Maasho alisema.

Je ghasia hizo zinahusishwa na mzozo wa Tigray?

Hapana lakini , lakini chama cha eneo hilo la TPLF kilichoondolewa uongozini kilimuona bwana Abiy kuwa tisho kwa majimbo hayo ya kikabila ambacho kilisaidia kuanza ujenzi wake nchini humo baada ya kuchukua mamlaka baada ya vita vya Gorilla 1991.

Kilikuwa kimeanzisha muungano wa vyama vinne vya eneo hilo kwa jina EPRDF ili kutawala eneo hilo. Lakini bwana Abiy alivunjilia mbali muungano huo mwaka uliopita , na kuubadilisha na chama cha Prosperity PartyPP.,.

Wafuasi wake wanaoona chama hicho kipya kama kinachosaidia kuleta umoja kwa kuunganisha vyama vya kikabila nchini Ethiopia.

Lakini kama mbali na vyama vingine vitatu TPLF kilikataa kujivunja na kuungana na PP.

Hatua hiyo ilisababisha kuharibika kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili na TPLF hakikuwakilishwa katika serikali ya kijimbo kwa mara ya kwanza tangu 1991.Chama hicho badala yake kilelekea katika ngome yake kuu ya Tigray na kufanya uchaguzi wa kijimbo mwezi Septemba kikikiuka uamuzi wa kijimbo wa kuahirisha uchaguzi huo kutokana na mlipuko a virusi vya corona.

Hali hiyo ilizua hali ya wasiwasi hatua iliosababisha kuzuka kwa vita katika jimbo la Tigray mwezi uliopita.