Benishangul-Gumuz: Washambuliaji wawaua mamia ya watu Ethiopia

Jeshi la Ethiopia limewaua zaidi ya wanaume 40 wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya karibu watu 100, miongoni mwao watoto, katika jimbo la Benishangul-Gumuz, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya serikali.
Maafisa watano wa sasa na wazamani wa serikali wamekamatwa kufuatia mauaji hayo, ripoti ziliongeza.
Washambuliaji walichoma moto nyumba za wanavijiji, kuwapiga risasi na kuwachoma visu wahasiriwa katika shambulio hilo la Jumatano.
Shambulio hilo linakuja siku moja baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuzuru eneo.
Haijabainika waliotekeleza shambulio hilo ni kina nani, lakini linaonekana kulenga jamii ya wachache wanaochukuliwa kuwa "walowezi" katika eneo hilo, Shirika la kutetea haki la Amnesty International limesema.
Ethiopia imeshuhudia ongezeko la ghasia za kisiasa, kijamii na kidini katika miaka ya hivi karibuni.
Ilikuwa na idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa ndani barani Afrika mnamo 2018 - karibu milioni 1.8.
Migogoro imekuwa ikichochewa sana na makundi yanayodai ardhi kwa nguvu, na jaribio kutaka kuwafukuza watu wanaochukuliwa kuwa kama watu wa nje.

Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri Mkuu Abiy Ahmes ameelezea mauaji hayo kuwa ya kusikitisha, na kusema kuwa serikali itatuma kikosi katika eneo hilo kusaidia kupata suluhisho la mzozo huo.
Vyombo vya habari vya serikali havikutoa utambulisho wa watu 42 waliouawa katika operesheni ya kijeshi kuwasaka washambuliaji.
Nini kilitokea
Nesi mmoja aliyekuwa akifanya kazi katika kliniki moja aliambia BBC kwamba zaidi ya watu 30 walikua wamelazwa katika kituo hicho cha afya , wengine wakiwa katika hali mahututi.
''Baadhi ya waathiriwa walipigwa, huku wengine wakichomwa visu, muuguzi huyo aliongezea''.
Katika taarifa, Tume ya haki za kibinadamu ya Ethioipia imesema kwamba shambulio hilo lilfanyika katika kijiji cha Bekoji , ambacho kipo katika eneo linaloishi raia kutka makabila mingi.

Chanzo cha picha, Reuters
Zaidi ya watu 100 wameuwa katika moto na ufyatulianaji wa risasi uliotekelezwa na watu waliojihami, wakati wa shambulio hilo la Alfajiri, tume hiyo ilisema.
Beyene Melese, msemaji wa serikali ya jimbo hilo alilaumu kile alichokitaja watu wasiopendelea amani kwa kutekeleza shambulio hilo.
Siku ya Jumanne , waziri mkuu Abiy alisafiri kuelekea katika eneo hilo ili kuzungumzia kuhusu kuzuka mara kwa mara kwa ghasia hizo za kikabila katika miezi ya hivi karibuni.
''Lengo na maadui ni kuigawanya Ethiopia katika misingi ya kikabila na kidini ipo, waziri mkuu aliandika katika ujumbe wa twitter baada ya ziara yake. ''Lengo hili halitakamilika''.
Benishangul-Gumuz limeshuhudia mashambulio manne mabaya tangu mwezi Septemba, ikiwemo shambulio la bunduki dhidi ya basi moja la abiria katika eneo la kaskazazini ma Tigray mwezi uliopita.
Mamia au maelfu ya watu wanadaiwa kuuawa katika mzozo huo huku watu 50,000 wakitorokea Sudan.













