Uchaguzi wa Israel: Uchaguzi mpya kufanyika huku serikali ya umoja ikivunjika

File images of Benjamin Netanyahu and Benny Gantz

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Bw Netanyahu (kushoto) a na hasimu wake wa kisiasa Benny Gantz wamegawana madaraka tangu Aprili
Iliyochapishwa

Israel itafanya uchaguzi wake wa nne katika kipindi cha miaka miwili baada ya vyama vikuu viwili katika serikali ya umoja kushindwa kuheshimu muda wa mwisho wa kutatua mzozo juu ya bajeti ya taifa.

Wapigakura watarejea katika uchaguzi mwezi Machi, miezi 12 tu baada ya awamu ya uchaguzi kufanyika.

Uchaguzi wa awali haukukamilika , na hivyo kusababisha kuundwa kwa serikali nadra ya umoja.

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu, ambaye kesi ya madai ya ufisadi inaendelea dhidi yake, ana matumaini ya kurejea madarakani kwa muhula wa sita.

Alikana mashitaka ya uhalifu, ambayo aliyapuuzilia mbali akiyataka kuwa yenye uchochezi wa kisiasa.

Jumanne usiku, bunge la Israeli-Knesset, lilivunjwa moja kwa moja kulinga na sheria baada ya makataa ya mwisho kupita ya kuidhinishwa kwa bajeti ya mwaka 2020.

Jaribio la saa 11 la kuepuka kuvunjwa kwa bunge lilishindwa baada ya muswada wa kurugusu kuongezwa kwa muda wa majadiliano zaidi kupingwa kwa kura, kinyume na ilivyo tarajiwa.

Natanyahu anasema shutuma za ufisadi dhidi yake ni hila za kisiasa
Maelezo ya picha, Natanyahu anasema shutuma za ufisadi dhidi yake ni hila za kisiasa

Saa kadhaa kabla ya muda wa mwisho kumalizika, Bw Netanyahu, ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la mrengo wa kulia la chama cha Likud , na mpinzani wake wa kisiasa Benny Gantz kutoka vuguvugu la mrengo wa kati la Blu na nyeupe , walilaumiana kila upande ukiutuhumu mwingine kusababisha mzozo huo.

" Sikutaka huu uamuzi ," Aliwaambia waandishi wa habari Bw Netanyahu . "Likud haikutaka huu uchaguzi . Tumechagua tena na tena dhidi ya uchaguzi. Bahati mbaya , Benny Gantz alivunja makubaliano yake na sisi ."

Amesema Likud kitapata "ushindi mkubwa'' katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Machi.

Bw Gantz amesema kuwa kauli za waziri mkuu Netanyahu ni za "uongo zaidi kuliko maneno ". Alisema kuwa Bw Netanyahu alitaka kusababisha uchaguzi kwa lengo la kuepuka kesi yake ya ufisadi.

Wawili hao waligawana madaraka tangu mwezi Aprili katika muungano ambao haukua rahisi , wakikubaliana kupokezana madaraka na waziri mkuu, ambapo Bw Netanyahu angechukua mamlaka kabla ya kipindi cha kukabidhi madaraka kwa Bw Gantz mwezi wa Novemba 2021.

Wachambuzi wanasema mgawanyiko ulikuwa njia ya Bw Netanyahuya kumaliza muungano kutokana na pengop katika mkataba ambao kwa mujibu wake uwaziri mkuu utakabidhiwa kwa kiongozi mwingine kwa kipindi cha miezi mitatu kama chochote kingesababisha uchaguzi, kando na tukio la kushindwa kupitishwa kwa bajeti.

Kura za maoni za hivi karibuni zinaonesha kuwa chama cha Blu na Nyeupe- Blu and White kimesambaratika , na uku uungaji mkono wa Likud ukipungua kitarejea kama chama kikubwa zaidi.

People waiting in line to get the first dose of coronavirus vaccine, in the Heichal Shlomo Sports Arena that turned into a massive vaccination center in Tel Aviv, Israel, 22 December 2020

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Israel kwa sasa imeanza kutoa chanjo ya virusi vya corona ya Pfizer/BioNTech kote nchini

Hatahivyo Bw Netanyahu anakabiliwa na shinikizo kubwa, huku maandamano ya mitaani dhidi ya utawala wake, kesi ya ufisadi ikitarajiwa kufufuliwa tena mwezi Januari, na mapambano yanayoendelea dhidi ya maambukizi ya corona kote nchini.

Baadhi ya wachambuzi wanasema alitaka uchaguzi kabla ya kukabidhi madaraka kwa Bw Gantz, lakini angependelea hilo lifanyike baada ya mwezi Machi. Hilo lingetoa muda zaidi kwa ajili ya kampeni ya utoaji wa chanjo ya corona na wakati ambapo uchumi utakuwa umeanza kufufuka.

Bw Netanyahu pia anakabiliwa na changamoto mpya kutoka chama cha mbunge wa zamani wa Likud , Gideon Saar, ambaye ameunda chama cha mrengo wa kulia ambacho kimeazimia kukipunguzia kura ngome ya kisiasa ya Bw Netanyahu.