Mwanaume aliyekamatwa kwa kukisia nywila ya rais Trump

Iliyochapishwa

Waendesha mashtaka wa Uholanzi wameridhia madai ya mdukuzi aliyefanikiwa kukisia nywila ya akaunti ya Twitter ya rais Donald Trump ambayo ni - "maga2020!"

Lakini hawatamuadhibu Victor Gevers, ambaye alikuwa akifuata maadili.

Bwana Gevers alionesha kile alishirikisha picha ya akaunti ya Trump tarehe 22 Oktoba, wakati wa hatua za mwisho za uchaguzi wa urais wa Marekani.

Lakini wakati huu, Ikulu ya Marekani ilikanusha kuwa walidukuliwa na Twitter ilisema kuwa hawana ushaidi kuhusu hilo.

Msemaji wa Twitter alisema: "Hatuna ushaidi wowote kuhusu madai hayo , pamoja na nakala iliyochapishwa Uholanzi hii leo .

Tuna ulinzi kwa kiwango cha juu kwa makundi ya watu wenye wadhifa wa juu , akaunti za uchaguzi pamoja na serikali."

White House haijajibu lolote.

Bwana Gevers alisema kuwa alifurahia kile alichoweza kufanya.

"Hili sio suala la kazi yangu tu lakini kwa waaojitoa wote katika intaneti," alisema.

Mtafiti mzuri wa masuala ya mtandao amekuwa akifuatilia kwa karibu wagombea wa urais wa Marekani , Oktoba 16 aliweza kukisia nywila ya rais Trump.

Polisi Uholanzi wanasema: Mdukuzi alitoa taarifa mwenyewe.

Walituma walichokipata katika mamlaka ya Marekani.

Bwana Gevers alidai kuwa na ushaidi wa zaidi.

Mbinu alizotumia, angeweza kuona taarifa zote za rais zikiwemo:

  • picha binafsi na ujumbe
  • ujumbe binafsi wa tweet
  • watu wangapi amewafungia

Akaunti ya rais ambayo ina wafuasi 89 sasa iko sawa.