Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi wa Marekani 2020: Mahakama ya juu zaidi yakataa azma ya Trump ya kugeuza matokeo ya uchaguzi
Mahakama ya juu zaidi ya Marekani imekataa jaribio la kubatilisha matokeo ya uchaguzi katika majimbo manne yenye ushindani mkubwa ambayo yalimuunga mkono Rais Donald Trump.
Mashitaka, yaliyowasilishwa wiki hii na jimbo la Texas, yalilenga kubatilisha matokeo ya uchaguzi katika majimbo ya Georgia, Michigan, Pennsylvania na Wisconsin.
Rais mteule Joe Biden alipata ushindi katika majimbo yote manne.
Mashitaka hayo yaliungwa mkono na Wanasheria wakuu wa majimbo 18 nchini Marekani na wanunge wa Congress 106 kutoka chama cha Republican.
Lakini katika maelezo mafupi ya kukataa azama hiyo, Mahakama kuu iliamua kuwa Texas haina haki ya kisheria ya kuleta kesi mbele ya mahakama hiyo.
Hukumu hiyo ni pigo kwa Bw Trump , ambaye awali alisema bila ushahidi Tkwamba matokeo ya uchaguzi wa urais wa Mwezi Novemba yatatatuliwa na Mahakama ya ngazi ya juu .
Mahakama pia ilikataa mashitaka mengine ya kisheria dhidi ya ushindi wa Bw Biden katika jimbo la Pennslvania mapema wiki hii, na kuyatupilia mbali madai hayo katika hukumu moja.
Bw Trump amekuwa akirudia mara kwa mara madai yasiyo na ushahidi kwamba "kura zisizo halali "zilimfanya asipate muhula wa pili wa urais.
Tangu uchaguzi ulipofanyika, Bw Trump na wafuasi wake wamefungua mashitaka makumi kadhaa wakihoji matokeo ya uchaguzi . Hakuna hata shitaka moja lililoweza kugeuza ushindi wa Bw Biden.
Biden ambaye alikuwa mgombea wa Democratic alimshinda Trump kwa kura za wajumbe 306 kwa 232 , ambao humchagua rais wa marekani . Bw Biden pia alipata ushindi wa kura milioni zaidi ya saba kuliko rais Trump zilizopigwa na raia wa nchi hiyo kote nchini Marekani.
Wajumbe wa uchaguzi wanatarajiwa kukutana Jumatatu kumchagua rasmi Bw Biden kama rais wa 46 wa Marekani
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa , wataalamu wa sheria walikuwa na wasiwasi kuhusu nafasi yake ya kufanikiwa kufikia lengo lake.
Lakini saa kadhaa tu baada ya hukumu hiyo kutolewa, Bw Trump alionekana mwenye matumaini , akiitaka Mhakama ya juu zaidi kuonesha "Gusara kubwa na ujasiri" wakati itakapotoa uamuazi juu ya mashikata yake.
Je hukumu imepokelewa vipi ?
"Hakuna njia ya kuelezea huku hii kuliko kutumia neneo kukwepa " aisema msemaji wa White House Bi Kayleigh McEnany, akimaanisha majaji . "Walikwepa, walijificha nyuma ya taratibu , na wakakataa kutumia mamlaka yao kutekeleza katiba ."
Msemaji wa Bw Biden alisema kuwa "hakuna la kushangaza " Mahakama ya juu ilikataa "majaribio yasiyo na msingi " kukkana kuwa Trump alishindwa katika uchaguzi.
"Mahakama yetu ya taifa ya juu zaidi iliona hata hivyo ukiukaji huu wa mchakato wa uchaguzi ," alisema Mwanasheria mkuu wa Pennsylvania Josh Shapiro, Mdemocrat.
Dana Nessel, Mwanasheria mkuu wa Michigan Mdemocrat alisema uamuzi ulikuwa " muhimu kukumbusha kwamba tuna taifa lenye sheria , ingawa baadhi hata hivyo wanaweza kumpendelea mtu mmoja binafsi, mahakama haiwezi ".