Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
David Beckham: Nyota aonekana amezeeka haraka - kunani?
David Beckham ndio sura ya kampeni mpya ya kukabiliana na ugonjwa wa Malaria , ugonjwa hatari unaosambazwa na mbu unaoathiri mamilioni ya watu kila mwaka.
Zaidi ya watu 400,000 walifariki kutokana na ugonjwa huo 2019 kulingana na shirika la Afya Duniani WHO.
Katika kanda hiyo ya video, Beckham anaonekana kuwa mzee akizungumza katika siku za usoni ambapo ugonjwa huo umeangamizwa.
Tangazo hilo lililofanywa na Charity of Malaria No More Uk limetengenezwa hali ya kwamba linawashinikiza watu kote duniani kuendelea na juhudi za kuangamiza ugonjwa huo kabisa.
Beckham amehusika na shirika hilo la hisani tangu 2009 na anasema ni ugonjwa ambao angependelea kuangamizwa kwasababu unawauwa watoto wengi duniani.."
Anasema kwamba Watoto wake mwenyewe walimuuliza iwapo ugonjwa huo unaweza kuangamizwa wakati wa kizazi chao na aliwajibu ndio utaangamizwa iwapo kutakuwa na ushirikiano mkubwa, uongozi bora pamoja na kutia bidii."
Je kuna hatua gani kubwa zilizopigwa katika vita dhidi ya Malaria?
Kwa sasa kuna chanjo dhidi ya ugonjwa huo ambao inapunguza idadi ya wagonjwa kwa asilimia 40.
Mpango wa miaka mitatu wa kusambaza dawa hiyo ulianza barani Afrika katika mataifa ya Malawi, Kenya na Ghana 2019.
Mnamo mwezi Mei 2020 wanasayansi waligundua kinga ya kuwalinda mbu dhidi ya Malaria.
Timu ya Kenya na ile ya Uingereza zilisema kwamba ugunduzi huo una uwezo mkubwa wa kudhibiti ugonjwa huo.
Hiyo ni kwasababu iwapo mbu hawatoambukizwa ugonjwa huo hawataweza kusambaza ugonjwa huo kwa wanadamu.
Vifo kutokana na ugonjwa huo vimepungua kwa asilimia 60 hatua iliowaokoa zaidi ya watu milioni 7 tangu 2000 kulingana na WHO lakini shirika hilo linasisitiza kwamba kunahitajika uwekezaji mkubwa katika vita dhidi ya Malaria iwapo ugonjwa huo utaangamizwa kufikia 2050.
Je serikali tofauti zimekuwa zikichukua hatua gani?
Mwaka 2016 serikali ya Uingereza ilitia saini hadi £500 million kwa mwaka kukabiliana na Malaria zitakazotumika hadi Marchi 2021.
Viongozi walikubaliana kufanya juhudi za pamoja kutumia mabilioni ya fedha miongoni mwa nchi zilizopo katika jumuia ya madola kufikia.