Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
‘Nyumba iliochini ya ardhi ilikuwa makazi ya Yesu’, Wasema wanaakiolojia
Wanaakiolojia "wanaamini" kuwa nyumba iliyojengwa chini ya ardhi huko Nazareth, Israel, ilikuwa makazi ya utotoni ya Yesu, kulingana na wachimbuzi wa vitu vya kale.
Profesa Ken Dark, kutoka chuo kikuu cha Reading, ametumia miaka 14 akisomea mabaki ya karne ya kwanza chini ya eneo la kidini la sasa.
Profesa huyo anasema kuwa mabaki yaliyofanyiwa utafiti, mwanzo yalionesha eneo hilo lilikuwa makazi kwa Yesu, Mary na Joseph karne ya 19.
Hata hivyo, hilo lilitupiliwa mbali na wanaakiolojia miaka 1930.
Eneo hilo likasahaulika kabisa tangu wakati huo hadi Profesa Dark alipoanza mradi wake wa kuhuisha tena mji huo mwaka 2006.
Alisema: "Sikwenda Nazareth kutafuta yaliyokuwa makazi ya Yesu, badala yake nilikuwa ninasomea historia ya hija ya Kikiristo ya Byzantium.
"Hakuna aliyepatwa na butwaa kama mimi."
'Utafiti ambao tunaweza kuufikia'
Alisema eneo hilo la kale lilikuwa chini ya kanisa enzi ya Byzantium.
Aidha, Profesa Dark anaelezea: "Tunachojua kutoka kwa ushahidi ulioandikwa, kanisa hili linaaminika kuwepo wakati wa Byzantium na lilijengwa katika eneo la makazi ya Yesu chini ya ardhi lililochimbwa na kuhifadhiwa mfano wa kaburi.
"Ni eneo lililokuwa Kanisa la Nutrition, lililotajwa katika hija ya karne ya 7."
Profesa Dark anasema kazi yake imetambua nyumba hiyo kama iliyokuwepo karne ya kwanza na kugundua kuwa jengo hilo lilikuwa mfano wa pango kwenye vilima vyenye miamba.
Alisema yule aliyejenga nyumba hiyo, alikuwa na ufahamu mzuri wa kazi inayotumia jiwe ambaye wakati huo alijulikana kama tekton, jina la kale la fundi stadi lililotumika kumtambua Joseph katika bibilia.
Hata hivyo, wanaakiolojia hao walisema ingawa yote hayo huenda yasidhihirishe kwamba ilikuwa nyumba ya Yesu, "huo ndio utafiti unaoweza kufikia katika kusema hiyo ilikuwa nyumba ya Yesu".