Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: Biden anasema Trump anatuma ujumbe mbaya sana duniani

Joe Biden

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, "Watu wote wanaamini kuwa uchaguzi ulikuwa wa halali"
Iliyochapishwa

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amelaani kitendo cha Donald Trump kukubali kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa rais, amesema kuwa 'anatuma ujumbe mbaya sana kuhusu Marekani'.

Bwana Biden amesema, alikuwa na uhakika kuwa bwana Trump alikuwa anajua kuwa hasingeshinda na kila kitu kilionekana wazi , kwa kuwa alikuwa hajitumi kabisa katika majukumu yake.

Kulikuwa na marudio ya kuhesabu kura za uchaguzi wa rais katika jimbo la Georgia, na bwana Biden alipata ushindi katika jimbo hilo.

Bwana Trump alifungua kesi ya madai ya wizi wa kura.

Madai yake yote ya kisheria yaligonga mwamba na kushindwa kufanya mabadiliko yoyote.

Bwana Biden amepata ushindi wa kura za umma kwa zaidi ya milioni 5.9 .

Ushindi wake katika kura za wajumbe ambazo zinaweza kuthibitisha nani anakuwa rais aliweza kukadiriwa kupata kura 306 mpaka 232.

Biden amesema nini?

Alikuwa akiongea katika mkutano wa simu na magavana , wakiwemo wa Democrats na Republicans, kuhusu janga la corona.

Alihojiwa kuhusu suala la Trump kutokubali ushindi wake, Biden alisema rais anatuma ujumbe wa kutisha... kwa dunia nzima kuhusu jinsi demokrasia inavyofanya kazi, na hilo anapaswa kulikumbuka kwa kuwa amekuwa rais ambaye hawajibiki katika historia ya Marekani."

President-elect Joe Biden attends a virtual meeting with frontline healthcare workers in Wilmington, Delaware on November 18, 2020

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Joe Biden anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa 46 wa Marekani tarehe 20 Januari

"Ni suala gumu kufahamu jinsi mtu anavyofikiri ," aliongeza: "Jambo ambalo analifanya linaleta hasira."

Matokeo ya uchaguzi wa rais, rais mteule huyo kutoka Democratic anaapishwa kuingia madarakani mwezi Januari.

Nini kilitokea Georgia?

Alhamisi, Katibu wa jimbo la Georgia, Brad Raffensperger, alisema kuwa kura urudiwaji wa kura haujabadilisha ushindi wa Biden katika jimbo hilo.

Awali, Republicans walishindwa kesi yao baada ya mahakama kukataa kusitisha kutoa cheti cha kukubali uchaguzi, na kinatarajiwa kutolewa Ijumaa.

Marudio ya kuhesabu kura walipata makosa ya kiwango cha juu kwa 0.73% kati ya Biden na Trump na kiwango cha chini kilisalia kuwa chini ya 0.5%.

Vote counting in Michigan

Chanzo cha picha, Reuters

Wakati wa harakati hizo wiki hii, maelfu ya kura ambazo zilipatikana na makosa, yalikuwa makosa ya kibinadamu na sio wizi wa kura, alisema meneja wa mfumo wa kura ,Gabriel Sterling.

Maofisa katika eneo la Floyd, Georgia, wamemfukuza meneja kutokana na suala hili , vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Trump atachukua hatua gani baada ya hapo?

Jambo moja ambalo vyombo vya habari vya Marekani vinadhani anaweza kujaribu kulifanya ni kushawishi majimbo rafiki ya Republican-kupuuzia kura zilizopigwa badala yake kuchagua wajumbe ambao watakuwa upande wa rais.

Bwana rump amemkaribisha mbunge wa Michigan katika Ikulu ya White House siku ya Ijumaa, kumjulisha mabadiliko yanayoweza kutokea.

Marekani ni jamuhuri ya kidemokrasia, na baada ya kupata ushindi wa kura nyingi za umma, rais uhesabu kura za moja kwa moja za umaarufu kulingana na wawakilishi wake katika kila jimbo.

Majimbo mengi huwa yanaangalia nani amepata kura nyingi za umaarufu.

Lakini sheria ya shirikisho inasema sheria ina mamlaka ya kufanya uchaguzi huo kama watashindwa kufanya maamuzi.

Wakala wa habari Reuters wamenukuu chanzo cha habari kilicho karibu na mipango ya Trump kikisema kuwa sasa kuna mikakati mingi ili kuifanya sheria ihusike katika hatua hizo.