Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Ethiopia: Vikosi vya Ethiopia vinasonga mbele, Tigray yaapa kuendelea na mapigano
Vikosi vya Ethiopia vimeteka miji miwili katika eneo la kaskazini mwa Tigray ambako wanajeshi watiifu kwa chama cha kisiasa cha kisiasa wanapigana na seikali kuu.
Viongozi wa Tigray wamethibitisha kushindwa lakini wamesema ni changamoto ya muda na kuapa kuishinda serikali.
Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema majeshi yake yanaelekea mji mkuu wa Tigray, Mekele.
Mamia ya watu wameripotiwa kufariki katika kipindi cha ghasia za wiki mbili.
Kuthibitisha hali ilivyo katika eneo la Tigray ni vigumu baada huduma za mawasiliano kukatizwa.
Mzozo huo umetokana na taharuki ya muda mrefu kati ya chama kikuyu cha kisiasa katika eneo hilo,Tigray People's Liberation Front (TPLF) na serikali kuu ya Ethiopia.
Wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuahirisha uchaguzi kutokana na janga la corona, hali ya taharuki ilipanda kati ya pande hilo mbili. TPLF inachukulia serikali kuu ni batili ikadai kuwa Bwana Abiy hana mamlaka ya kuendelea kuongoza nchi.
Serikali inalaumu TPLF kwa kushambulia kabi ya majeshi kwa lengo la kuiba silaha, madai ambayo TPLF imepinga. Bwana Abiy alijibu madai hayo akisema kitendo cha TPLF ni uhaini.
Ni yapi yanayojiri kwa sasa?
Vikosi vya serikali vimeteka miji ya Shire na Axum baada ya muda wa siku tatu ya makataa uliotolewa na Waziri Mkuu Abiy kwa vikosi vya Tigray kujisalimisha kuisha siku ya Jumanne.
Kiongozi wa TPLF Debretsion Gebremichael amethibitisha katika Televisheni ya eneo hilo Jumatano kwamba wanajeshi wake wamepoteza udhibiti wa Kusini na Magharibi mwa Tigray, lakini akaongeza kuwa ni changamoto ya muda na kushinda vikosi vya Bwana Abiy.
"Naomba tuimarishe uwezo wetu pamoja," alisema, akitoa wito kwa watu wote wa Tigrayan wakiwemo watoto kujiunga na "harakati" hizo.
"Tigray sasa ni Kiama kwa maadui wake. Watu wa Tigray haweatawahi kupiga magoti," chama cha TPLF kilisema katika taarifa, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Maafisa wa Ethiopia wanalaumu TLPF kwa kuharibu madaraja manne karibu na mii mkuu waJimbo la Tigray, Mekelle, lakini kind hilo limping made hayo.
Siku ya Jumanne Waziri mkuu aliashiria kwamba mapigano yanakaribia kumalizika, akingezea "hatua ya mwisho ya utekelezaji wa kisheria utafanyika siku zijazo".
Karibu watu 27,000 wamekimbilia mpaka wa kaskazini na kuingia Sudan huku Umoja wa Mataifa ukionya kutokea kwa "mzozo kamili wa kibinadamu" .
Mshauri wa TPLF Fesseha Tessema, ambaye ni mwanadiplomasia wazamani wa Ethiopia, ameambia BBC kuwa makazi ya raia mjini Mekelle yalishambuliwa kwa makombora na vikosi vya serikali.
"[Watu wa Tigray] hawajafanya makes yoyote, wake majumbani mwao, kanisani," Bwana Fesseha alisema.
Serikali kuu imekana kuwalenga raia na kusema kwamba mashambulizi ya angani yalilenga wanajeshi wa Tigray.
Hali ni mbaya kiasi gani?
Shirika la kutetea haki la Amnesty International limesema kuwa ''limethibitisha vifo vya watu karibu 100 ambao wameuawa kwa kuchomwa kisu au kukatwa mapanga'' katika mji wa Mai-Kadra (May Cadera) Jumatatu wiki iliyopita.
Bwana Abbiy amelaumu vikosi tiifu kwa viongozi wa Tigray kwa kutekeleza mauji ya watu wengi. TPLF kwa upande wake imekanusha madai hayo na kusema iko tayari kufanyiwa uchunguzi huru wa kimataifa.
Tume ya haki za binadamu ya Ethiopia imesema itapeleka wachunguzi wake katika eneo hilo.
Kwa nini Ethiopia na TPLF Wanapigana?
TPLF ilitawala jeshi la Ethiopia na maisha ya kisiasa kwa miongo kadhaa kabla ya Bw Abiy kuingia mamlakani mwaka 2018 na kupitisha mageuzi mkubwa.
Mwaka jana Bw Abiy alivunja muungano tawala , unaojumuisha vyama vilivyoundwa kwa misingi ya kikabila , na kuviunganisha katika chama kimoja, national party, the Prosperity Party, ambacho TPLF walikataa kujiunga.
Utawala wa Tigray unayaona mageuzi ya Bw Abiy kama jaribio la kujenga mfumo serikali moja na kuharibu mfumo uliopo sasa wa shirikisho.
Pia hukasirishwa na kile inachokiita urafiki wa waziri mkuu na rais wa Eritrea Isaias Afwerki "usiokuwa na kanuni "
Bw Abiy alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019 kwa juhudi zake za kuleta amani kwa kumaliza mzozo wa muda mrefu wa nchi yake na Eritrea.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu anaamini kuwa maafisa wa TPLF wanadharau mamlaka yake.
Bw Abiy alimuru mashambulio ya kijeshi dhidi ya TPLF baada ya kusema kuwa wapiganaji wake walikuwa wamevuka "mstari wa mwisho mwekundu".
Aliwashutumu kwa kushambulia kambi ya kijeshi ya vikosi vya shirikisho tarehe 4 Novemba. TPLF walikanusha kuishambulia kambi ya majeshi.