Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trump 'kurejesha nyumbani' wanajeshi zaidi wa Marekani kutoka Afghanistan na Iraq
Jeshi la Marekani linatarajia Rais Donald Trump ataamuru majeshi zaidi kuondoka nchini Afghanistan na Iraq, kwa mujibu wa maafisa wa idara ya ulinzi walionukuliwa na vyombo vya habari vya Marekani.
Wale walio Afghanistan watapunguzwa kutoka 5,000 mpaka 25,000 ifikapo katikati ya mwezi Januari, maafisa wameeleza. nchini Iraq watapunguzwa kutoka 3,000 mpaka 2,500.
Rais Trump awali alisema kuwa anataka wanajeshi "wote" watarejea nyumbani msimu wa Krisimasi.
Amekataa kukubali kushindwa na Joe Biden katika uchaguzi wa tarehe 3 mwezi Novemba.
Mchakato wa kuwaondosha wanajeshi utamalizika tarehe 15 mwezi Januari, vyombo vya habari vya Markeani vimeripoti, siku kadhaa kabla Biden kuapishwa kuwa Rais.
Lakini Trump aliripoti mpango huo kuwa unakosolewa na Warepublican wenzake- Kiongozi wa Seneti Mitch McConnel, aliyeonya kuwa wanamgambo ''wataupenda" mpango huo.
Akizungumza siku ya Jumatatu kwenye bunge la juu, seneta wa Kentucky alisema: " Tumekuwa tukipunguza idadi ya wanajeshi- lakini kazi muhimu ya kulinda usalama wa taifa la Marekani na maslahi ya Marekani dhidi ya magaidi ambao hawatataka cha ziada kwa taifa lenye nguvu kama kutuona tukinyayuka na kurudi nyumbani. "watalipenda hilo".
Rais Trump kwa muda mrefu ameyataka majeshi kurejea nyumbani na amekuwa akikosoa operesheni za majeshi ya Marekani kuwa yamekuwa yakigharimu na kukosa ufanisi.
Viongozi wa kijeshi waliambiwa mwishoni mwa juma lililopita kuhusu mpango wa kuondoa majeshi, kwa mujibu wa maafisa walionukuliwa na shirika la habari la AP. Lakini amri hiyo haijatolewa kwa makamanda, waliongeza.
Mwezi Septemba, Idara ya ulinzi ilitangaza kuwaondoa wanajeshi zaidi ya theluthi kutoka Iraq ndani ya wiki kadhaa- kutoka 5,200 mpaka 3,000.
Wakati huo, Kamanda wa Mashariki ya Kati Jenerali Kenneth McKenzie amesema wale watakaobaki wataendelea kushauri na kusaidia vikosi vya usalama nchini Iraqi ''kuondoa wanamgambo wa Islamic State waliosalia.
Vikosi vinavoongozwa na Marekani vilivamia Iraq mwaka 2003 kuangusha utawala wa Rais Saddam Hussein, na kutafuta silaha za maangamizi ambazo hata hivyo ikabainika kuwa hazipo.
Vikosi vya Marekani vimekuwa nchini Afghanistan tangu mwaka 2001. Muungano wa majeshi ukiongozwa na Marekani waliondosha wanamgambo wa Taliban baada ya mashambulizi ya al-Qaeda tarehe 11 mwezi Septemba 2001 nchini Marekani , wanamgambo ambao wakati huo makazu yao yalikuwa Afghanistan.
Marekani ilianza kuondoa majeshi yake kutoka Afghanistan mwanzoni mwa mwaka huu kama sehemu ya makubaliano ya amani na Taliban.
Taliban waliungana tena na kurejea tena kwenye operesheni zao mwaka 2018 katika zaidi ya theluthi mbili ya nchi.
Hatahivyo, wakuu wa jeshi, pamoja na Jenerali McKenzie, walionya hapo awali kwamba mazungumzo ya amani kati ya Taliban na mamlaka ya Afghanistan yanaweza kudhoofisha uondoaji wa haraka wa majeshi ya Marekani.