Biden:'Watu wanaweza kufa' wakati Trump anaondoka madarakani

Joe Biden

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Joe Biden ametoa angalizo kuwa "watu wanaweza kufa" kama rais aliye madarakani ataendelea kuwa kuzuizi.

Akizungumza na Delaware, rais mteule alisema ushirikiano aliokuwa anauhitaji ni kukabiliana na mlipuko wa janga la corona.

Kitendo cha Rais Trump kukubali kuwa ameshindwa uchaguzi licha ya jitihada zake kugonga mwamba.

"Huu si mchezo," mke wa rais wa zamani Michelle Obama aliandika katika mitandao ya kijamii.

Rais mteule alipata kura 306 kutoka kwa wajumbe wa uchaguzi , na kuzidi hata kiwango kilichowekwa cha ushindi cha kura 270.

Ingawa Trump, wa Republican, aliandika kwenye tweeter Jumatatu asubuhi : "Nimeshinda uchaguzi!"

Kampeni za Trump zilipeleka madai ya kura za uchaguzi wa Novemba 3, kuibiwa katika hatua za kisheria.

Gwinnett county workers begin their recount of the ballots on November 13, 2020 in Lawrenceville, Georgia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maofisa wa uchaguzi

Utawala Mkuu wa Huduma (GSA), ambao ndio wakala wa serikali uliopewa jukumu la kuanza mchakato wa mpito kwa rais mpya,bado hawajamtambua Bwana Biden na Kamala Harris kama washindi, na kuwaacha bila ya kuwapa taarifa fupi za serikali ambazo kawaida hutolewa kwa utawala unaoingia.

Hivyo hali hiyo ya kutokutambuliwa inazua hofu kwa Biden, kwa sasa hakutakuwa na utaratibu maalumu kutoka serikalini katika kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya Corona hivyo huenda kukaendelea kuwa na vifo vingi zaidi.

Katika hotuba yake Jumatatu Biden alisema : "Hivi kuna yeyote anayeelewa hiki ?Ni kuhusu kuokoa maisha ya wa watu , kiukweli hii si sawa."

"Watu wengi wanaweza kufa kama hatutashirikiana ," aliongeza.

Pia Biden amesema suala la chanjo ya kitaifa ni kazi kubwa, kubwa na ikiwa yye na timu yake watasubiri mpaka kuapishwa kwake hapo Januari 20 mpango wa usambazaji wa chanjo hiyo utakuwa nyuma sana.

Kampuni ya dawa ya nchini Marekani iitwayo Moderna hajo jana ilitangaza kupata chanjo inayoendelea kufanyiwa utafiti ambayo inaweza kuzuia ugonjwa wa COVID-19 kwa asilimia 94.5.

Michelle Obama amesema nini?

Obama
Presentational white space

Mke wa rais wa zamani Michelle Obama ameonya suala la Trump kwenye Instagram.

Alieleza suala la ugumu wa Trump kuondoka katika Ikulu ya Marekani White House, kwa miaka minne iliyopita alisambaza uongo wa kibaguzi kuhusu mume wake na kuiweka familia yake hatarini - alitoa madai ya kipuuzi kuhusiana na eneo ambalo Obama alizaliwa.

Hata hivyo , "Mapenzi kwa taifa letu linatutaka tuheshimu matokeo ya uchaguzi hata kama hatupendi au kama tungependa mambo yawe tofauti -Urais haumilikiwi na yeyote au chama chochote", Bi. Obama aliandika.

Huu sio mchezo , wala sio suala binafsi au la kisiasa-maigizo ya masiahala ya namna hii yanaweza kuhatarisha maisha ya watu kiafya na usalama wao.

Bi. Obama amewataka Wamarekani, haswa viongozi kutoka chama chochote kuheshimu mchakato wa uchaguzi na kuhamasisha makabidhiano ya utawala yaende vizuri kwa amani.

"Wamarekani wamezungumza.Na jukumu kubwa la rais ni kusikiliza ,"aliandika.