Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanamke mwenye HIV anayelishutumu taifa la Chile kwa kumfunga kizazi bila idhini yake
Wakati waliponipeleka katika chumba cha kujifungulia, nesi aliniambia kuwa watu kama mimi wenye HIV hawapaswi kuwa na watoto na kwamba ningetakiwa kuwa nilikwisha toa mimba.
Aliniambia: "Umepoteza fahamu kwasababu, mtoto wako wa kiume atakayezaliwa atakuwa na maisha gani ya usoni kama utakufa."
Nilikuwa nimetambua kuwa nilikuwa na virusi vya Ukimwi(HIV), lakini sikua na la kufanya. Na kile nilichotaka tu ni kuwa mama, ilikuwa ni ndoto yangu.
Nisingefuta kile nilichokitaka.
Lakini wakati huo wa kujifungua ,nilihisi vibaya sana, sikujua kama nilifanya vema kwa kuwa mimba au kama nilifanya makosa. Nilijiuliza maswali mengi.
Lilikuwa ni tukio la kuvunja moyo sana, roho yangu inauma. Nilikuwa na uchungu wa na kujifungua na uchunguwa mtu ambaye alikuwa ananiambia kuwa nitakufa na labda hautaweza kumuona mtoto wako na kwa ujinga wote ambao nilikuwa nao wakati ule, ilinifanya nihisi mwenye hasira na mfadhaiko mkubwa.
Na siku ya pili kana kwamba maneno waliyoniambia hayatoshi waliniambia kuwa : "Umefungwa kizazi, hautakuwa na uwezo tena wa kupata watoto zaidi ."
Mwanzoni mwa mwaka ule, wakati Francisca alipobaini kuwa ana HIV, aliendelea kupata matibabu ya vidonge vya kupunguza makali ya virusi -antiretroviralsili mtoto wake aliyekuwa amembeba tumboni asiathirike, na akapanga kufanyiwa upasuaji wa uzazi- cesarean section ili kujifungua mtoto wake katika hospitali ya Curicó Hospital, iliyopo kusini mwa Chile.
Alijifungua salama kwa upasuaji , lakini baada ya kujifunbgua alifungwa kizazi kwa kufunga mirija ya inayokutanisha mayai ya uzazi na mbegu -fallopian tubes bila idhini yake, anasema Francisca, ambayer anapenda utambulisho wake ufichwe.
Kesi yake
Tume ya America Kusini ya haki za binadamu IACHR (Inter-American Commission on Human Rights) shugulikia kesi yake kwa njia ya kirafiki kkufuatia mashhitaka ambayo Francisca aliyawasilisha kwake dhidi ya taifa la Chile.
BBC ilijaribu kuzungumza na Hospitali ya Curicó , lakini ikaambiwa wauliza Huduma za kikanda za afya katika jimbo la na wakasema kwasababu kesi bado inaendelea hawawezi kuizungumzai.
Wizara ya makazi na miji ya Chlie iliiambia BBC kuwa "Taifa la Chile litasaini akubaliano ya kirafiki na Francisca" na kwamba "Katika hatua za kumlipa fidia ataweza kupewa nyumba yenye thamani ya dola 737,000 za kimarekani".
"Walinifanyia ukatili mkubwa "
Sikufahamu kabisa kwamba wanakwenda kunifunga kizazi. Baadaye nilifikiri kila mtu mwenye HIV alifungwa kizazi.
Nilifikiria zaidi kuhusu ugonjwa wangu, nilifahamu tu utaratibu huo wakati nilipokuwa nikifuatilia taratibu za kuhakikisha kuwa mwanangu anazaliwa mwenye afya.
Kipaumbele change cha kwanza kilikuwa ni kumlinda mwanangu, kwahiyo niliamua kutumia daw azote, kufanya vipimo vyote kwasababu nilitakiwa kumlinda mwanangu.
Mwanzoni sikufikiria zaidi ya haki zangu au lolote.
Baadaye nilipokwenda katika uchunguzi wa kawaida , nikaanza kuwasiliana , kuzungumza zaidi na watu kuhusu yaliyonisibu ambao walikuwa na hali kama yangu na pale wakanifahamisha kuwa kunifunga kizazi ni kinyume cha sheria na kwamba haki zangu zimekiukwa, kwamba hawangepaswa kunifunga uzazi.
unaweza pia kusoma:
Mwanangu wa kiume alikuwa na umri wa mwaka mmoja nilipoanza kuona mtizamo mwingine.
Mwaka uliofuata nilitarajia kupata mimba kila mwezi, nilitumaini kuwa sitaona hedhi ya mwezi na nilipoipata, niliumia sana kwasababu nilijaribu sana lakini sikupata.
Unapohisi kwamba unataka kupata mtoto mwingine, halafu upate hedhi , lakini huwezi kupata ujauzito, inauma sana.
Unaweza pia kutazama:
Hadi nilipomuona daktari nikamueleza kwamba sijapata ujauzito. Daktari aliniambia: " Lakini inaonekana uliiondoa kwasababu mirija yako [the fallopian tubes] ilikatwa kwa hali iliyo ya kawaida".
Hapo ndipo nilipojua kuwa sina tena bahati ya kupata mtoto mwingine.
Likikabiliwa na tuhuma hizo , katika mwaka 2017 taifa la Chile ilikubali kusaini makubaliano ya kirafiki na Francisca na akakubali.
Lakini hadi sasa, Francisca na mawakili wake wanasubiri serikali itie saini katika mkataba huo.
Kuna kesi zaidi nchini Chile
Kulingana na uchunguzi uliofanywa na makampuni ya CDR na Vivo Positivo, visa kama cha Francisca vimekuwa vikirudiwa nchini Chile miaka iliyofuatia baada ya Kisa cha Francisca.
Mwaka 2009 na mwaka 2010 utafiti kuwahusu wanawake 27 wanaoishi na virusi vya HIV nchini Chile, uliofanywa na CDR na Vivo Positivo ulibaini kuwa wanawake 16 walifungwa vizazi vyao na kati yao, "ni wane tu waliosema kuwa walipewa taarifa na kuamua binafsi kufungwa vizazi. "
"Wanawake wengine waliripoti kuwa walifanyiwa mkakati wa kupewa ushauri wa kuwashawishi , walipewa taarifa za upotoshaji au taarifa ambazo hazikukamilika, na kuamua baadaye kufunga vizazi bila kuwa na ujuzi au kutoa idhini ," kulingana na ripoti ya mashirika hayomawili iliyochapishwa mwaka 2011.