Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: Mfahamu Jill Biden mke wa Rais mteule Joe Biden

Jill Biden: Joe Biden atatimiza ahadi alizotoa kwa Wamarekani
Maelezo ya picha, Jill Biden: Joe Biden atatimiza ahadi alizotoa kwa Wamarekani
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Akiwa amesimama nje ya darasa lisilo na wanafunzi ambapo alikuwa akifunza lugha ya Kiingereza miaka ya 90 , Jill Biden alitoa hotuba katika mkutano mkuu wa chama cha Democrat baada ya mume wake kutangazwa kuwa mgombea wa urais wa Democrat.

Baada ya kutoa hotuba hiyo ili kumsaidia mumewe kuteuliwa , alikumbatiwa na mumewe ambaye alimpongeza kwamba ana kila kitu kuwa mke wa kwanza wa taifa.

''Kwa wote waliopo nchini humu , fikirieni walimu wenu waliowapatia elimu na kuwa mulivyo sasa ili kujiamini …huyo ndio aina ya mke wa kwanza …Jill Biden atakavyokuwa'', alisema.

Lakini tunajua nini kuhusu mwanamke huyu ambaye hivi karibuni atakuwa anajiunga na mume wake katika Ikulu ya Whitehouse?

Jill Jacobs alizaliwa mwezi Juni 1951 katika jimbo la New Jersey nchini Marekani.

Akiwa ndiye mwana mkubwa kati ya dada watano, alikulia katika makaazi ya Philadelphia ya Willow Grove.

Kabla ya kufunga ndoa na Joe alikuwa ameolewa na mchezaji wa soka akiwa chuoni kwa jina Bill Stevenson.

Joe Biden alipoteza mke wake wa kwanza na mwanawe wa kike katika ajali ya barabarani 1972. Watoto wake Beau na Hunter wote walinusurika katika ajali hiyo. Jill anasema kwamba alimjua Joe kupitia ndugu zake miaka mitatu baadaye.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Wakati huo , alikuwa seneta huku yeye akiwa chuoni.

''Nilikuwa nikichumbiana na watu waliokuwa wakivalia nguo aina ya jins na Tishati, alikuja mlangoni akiwa amevalia koti moja la michezo na viatu aina ya lofas, na nikafikiria Mungu wangu hii haiwezekani , hata miaka milioni moja ijayo''

"Alikuwa na umri wa miaka tisa zaidi yangu . lakini tulikwenda nje kumuona mwanamume na mwanamke katika ukumbi wa kutazama filamu katika mji wa Philladelphia na tulivutia watu wengi'', aliambia jarida la Vogue kuhusu siku yao ya kwanza walipokutana.

Anasema kwamba Joe alimchumbia mara tano kabla ya yeye kukubali.

''Sikutaka watoto wa Joe wapoteze mama mwengine . Hivyobasi nilitaka kujihakikishia asilimia 100'' , alielezea.

Wanandoa hao walifunga ndoa mjini New York 1977. Mtoto wao Ashley alizaliwa 1981. Bi Biden alizungumzia kuhusu familia yake na changamoto walizokumbana nazo wakati alipompendekeza mume wake katika mkutano huo mkuu.

Mwanawe mkubwa Beau Biden alifariki kutokana na saratani ya ubongo mwezi Mei 2015 akiwa na umri wa miaka 46.

''Najua kwamba iwapo tutaliacha taifa hili chini ya mikono ya Joe , atazifanyia familia zenu kile ambacho ametufanyia - kutuunganisha , na kutuongoza wakati ambapo tutakuwa na changamoto na kufuata na kutimiza ahadi zote alizowapatia raia wa Marekani'', alisema.

Kazi yake ya kuwa mwalimu.

Bi Biden , mwenye umri wa miaka 69 ametumia kipindi cha miongo kadhaa akifanya kazi kama mwalimu. Mbali na kuwa na shahada moja na mbili za uzamifu pia alikuwa na ile ya elimu kutoka chuo kikuu cha Delaware 2007.

Kabla ya kuelekea Washington DC , alifunza katika chuo cha jamii , katika shule ya upili ya umma na katika hospitali ya wagonjwa wa Saikolojia ya watu wazima.

Jill na Joe Biden

Chanzo cha picha, Twitter/Joe Biden

Alitoa hotuba yake katika mkutano wa Democrat mwaka huu kutoka katika darasa lake la zamani katika shule ya upili ya Delaware Brandywine ambapo alifunza lugha ya Kiingereza kutoka 1991 hadi 1993.

Huku Mume wake akiwa makamu wa rais , bi Biden alihudumu kama profesa wa somo la kiingereza katika chuo cha jamii cha Northern Virginia. 'Kufunza sio kitu ninachofanya bali ndio mimi'', alituma ujumbe wa twitter mwezi Agosti.

Siasa

Bi Biden awali alishikilia taji la mke wa pili huku mumewe akihudumu kama makamu wa rais kutoka 2009 hadi 2017. Wakati wa kipindi hiki kazi yake ilishirikisha kukuza vyuo vya jamii , akipigania familia za wanajeshi na kutoa hamasa kuhusu saratani ya matiti.

Pia alizindua shirika la kuungana na kusaidia wanajeshi wakongwe na familia zao kupata mipango ya elimu na ajira akishirikiana na Michelle.

Mwaka 2012, alichapisha kitabu cha watoto kwa jina Don't Forget , God Bless our troops kutokana na uzoefu wa mjukuu wake wa kuwa katika familia ya kijeshi.

Amekuwa akimuunga mkono mumewe wakati wa kampeni , akionekana naye huku wakifanya hafla na kuchangisha fedha.