Matokeo ya Uchaguzi Marekani 2020: Je ni nani anayeongoza katika majimbo ambayo hayajahesabiwa?

Iliyochapishwa

Kinyanganyiro cha Ikulu ya Whitehouse kinakaribia awamu ya nani atakayeshinda majimbo machache yaliosalia .

Huu hapa mwelekezi wako.

Uchambuzi wa ripota wa Marekani kaskazini Anthony.

Lini tunaweza kupata mshindi?

GEORGIA - Wajumbe 16

Mambo yalivyo kufikia sasa: Trump anaongoza lakini Biden anapunguza pengo lililopo - tofauti iliopo sasa ni chini ya kura 2000.

Je ni kura ngapi ambazo hazijahesabiwa: Maafisa wanasema kwamba takriban kura 15,000.

Ramani ya Georgia

Je kura hizo zinatoka maeneo gani?

Hizi ni kura zilizopigwa kwa njia ya posta ambazo zinatoka Atlanta na Savannah ambazo zinaelekea katika kapu la Biden.

Anthony anaangazia kinachotarajiwa: Ni kinyanganyiro kikali - Kwanza Biden anakaribia kumfikia Trump la sivyo Kura zinazohesabiwa zitaisha.

Ni Lini tutapata matokeo? Maafisa wanasema wanakaribia kumaliza na huenda wakapata matokeo Alhamisi Jioni au Ijumaa alfajiri.

…………………………….

PENNSYLVANIA - Wajumbe 20

Hali ilipofikia: Trump anaongoza lakini Biden anapunguza tofauti ya kura iliopo - Kile ambacho kilionekana kama uongozi wa zaidi ya kura nusu milioni sasa kimepungua hadi kura 23,000.

Je ni kura ngapi ambazo hazijahesabiwa?

Kuna takriban kura 550,000 ambazo hazijahesabiwa huku nusu yake zikiwa hazijaguswa.

Je kura hizo ziko wapi? Katika kaunti ambazo Hillary Clinton aliibuka mshindi katika uchaguzi wa 2016 hivyobasi huenda zinaelekea katika kapu la Biden.

Ramani ya Pennsylvania

Anthony anaangazia kinachotarajiwa : Kura nyingi zilizosalia ni zile zilizopigwa kwa njia ya Posta kutoka katika eneo la Philadelphia , na hio ndio sababu Biden anaendelea kupunguza tofauti ya idadi ya kura kati yao katika jimbo hilo.

Ni lini tutapata matokeo?

Maafisa wa kijimbo wanasema kwamba wanatumai kwamba idadi kubwa ya kura zitahesabiwa kufikia mwisho wa Alhamisi.

…………………………………………….

ARIZONA - Wajumbe 11

Kufikia sasa: Biden anaongoza kwa kura 47,000 lakini Trump amekuwa akipunguza tofauti

Je ni kura ngapi ambazo hazijahesabiwa? Maafisa wanasema siku ya Alhamisi walikuwa na kura 470,000 ambazo zilikuwa hazijahesabiwa - haijulikani ni kura ngapi

Ramani ya Arizona

Je kura hizi zinatoka wapi?

Zote zinatoka katika majimbo hayo, lakini nyingi zinatoka katika eneo la Phoenix.

Anthony anaangazia kinachotarajiwa :

Biden alikuwa na uongozi wa kura nyingi mapema kura zilizpoanza kuhesabiwa , lakini ni Trump ambaye amekuwa akipunguza tofauti hiyo ya kura .

Huku kura zilizosalia zikitarajiwa kutoka kaunti ya Maricopa kounti, ambayo Biden alishinda , muhimu ni iwapo walipiga kura moja kwa moja ambapo Trump amefanya vyema ama hata kushindwa katika kura za kupitia njia ya posta ambazo zinaelekea kumpendelea Biden.

Je ni lini tutapata matokeo?

Tunatarajia matokeo mengi siku ya Ijumaa.Hatujui ni ngapi na iwapo yatakuwa na athari yoyote.

NEVADA - Wajumbe 6

Pale tulipofikia: Biden anaongoza kwa takriban kura 12,000, uogozi ambao aliuimarisha kidogo siku ya Alhamisi. .Je ni kura ngapi ambazo zinasubiri kuhesabiwa: Maafisa wanasema kuna takriban masanduku 190,000 ambayo hajajahesabiwa.

Ramani ya Nevada

Je kura hizi zinatoka wapi ?

Takriban asilimia 90 ya kura hizo zinatoka katika kaunti ya Clark ambayo inashirikisha Las Vegas na kura nyingi zilipigwa kupitia njia ya posta.

Anthony anasemaje?: Uongozi mwembamba huenda ukaongezeka huku kura zaidi zilizopigwa kwa njia ya posta na masanduku ya kura kutoka maeneo mbalimbali mengi kutoka kaunti inayounga mkono chama cha Democratic huko Las Vegas

Je ni lini tutapata matokeo zaidi?

Ongezeko la masanduku 51, 000 ya kura yataripotiwa kesho , kulingana na Joe Gloria afisa wa kaunti ya Clark.

Matokeo yote hatahivyo yatatolewa siku ya Jumapili.