Uchaguzi wa Marekani 2020: Je wajua kuna wagombea wengine 1,214 wa urais Marekani?

Iliyochapishwa

Marekani imekuwa na marais kwa zaidi ya miaka 230, lakini - George Washington - ndiye wa kwanza kuchaguliwa kama mgombea binafsi.

Siasa za vyama vya Republican na Democratic zimeangaziwa zaidi na vyombo vya habari kiasi cha kuwa ni vigumu mtu yeyote kutoka nje ya vyama hivyo kushinda uchaguzi.

Kufikia Octoba 9, wagombea 1,216 wa urais waliwasilisha maombi ya kutaka kuwania kiti cha urais wa Marekani kwa Tume ya Uchaguzi.

BBC alizungumza na watatu kati yao - mpiga piano na mashauri nasaha, mzaliwa wa Marekani na fundi wa mitambo mawasiliano ya kiteknolojia na bilionea wa sarafu ya dijitali - wanasimamia nini, na kwanini wanastahili kura za Wamarekani.

'Wamarekani wataona wagombea wawili wakuu hawafai'

Jade Simmons ni mwanamke ambaye kwa lugha ya majazi anavalia kofia kadhaa. Malikia huyo wa zamani wa urembo pia ni mpiga piano wa tamasha la kitaalam, mshauri nasaha, rapa, mama, na mchungaji aliyeteuliwa.

Kama anavyosema, yeye ni mgombea asiyekuwa wa kawaida, "lakini kuna nyakati ambazo sio za kawaida ".

"Kwangu mimi huu ni wakati ambao hatuwezi kufanya mambo kama kawaidal," anasema "Mimi ni binti wa mwanaharakati wa kupigania haki katika jamii, pia naomba mjue kuwa baba yangu alinifunza kutonyamaza nisiporidhika na mambo yalivyo, ukiona haki inakiukwa unahitaji kujiuliza laiti ni mimi ningelifanyaje."

Anasemalengo lake ni kubuni nafasi sawa kupitia uchumi, elimu na mageuzi ya mfumo wa haki. Na kutokana na malengo hayo "anapania kuendesha kampeni isiyo na gharama katika historia ya nchi yetu".

Kwa hivyo yeye ni mlibarali au mhafidhina?

"Inategemea swali hilo umemuuliza nani!" anasema. "Kila kitu kutoka kwa wanaolalamika kinyonge hadi wahafidhina makanisani wanapenda sera zetu."

Anasema malezi yake ya kihafidhina na mpenda dini hayajamnya yeye kuwa mhafidhina moja kwa moja , anasema.

Janga la corona limevuruga kwa kiwango kikubwa kinyang'anyiro ch akuingia Ikulu ya White kwa kuzuia mikusanyiko ya watu, hali iliyolazimu vyama vya kisiasa kunadi sera katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Lakini kwa Jade, changamoto kubwa iliyokumba kampeni yake ni kujitambulisha kwa watu wajue naye yuko katika kinyang'anyiro hiki.

"Hata wakati wa ambapo ulimwengu uliangazia suala la maisha ya watu weusi yana umuhimu watu walikuja pamoja kuzungumzia suala hilo kupitia vyombo vya habari na mashirika ya kijamii - lakini vyombo hivyo vy ahabari vilikataa kusema nika hapa.

"Huenda umemsikia msanii maarufu kama Kanye West ambaye hata hakuwasilisha makaratasi yake lakini Julai tarehe nne alipotangaza kuwa tagombea urais ndani ya dakika 30 taarifa yake iliangaziwa katika vyombo vyote vikuu vya habari. Kwa hivyo tulishangaa sana kuona suala la demokrasia halipo kama wanavyodhania wapiga kura wa Marekani hasa ukilichunguza kwa undani."

Wakati wagombea walioteuliwa na Republican na Democratic watakuw akatika karatasi ya kupiga kura katika majimbo yote, wagombea binafsi lazima wafikia masharti kadhaa kabla ya kupewa idhini ya kugombea.

Jina la Bi Simmons lilichapishwa katika makaratasi ya kupiga kura katika majimbo ya Oklahoma na Louisiana, lakini katika majimbo mengine 31 alisajiliwa kama mgombea atakaye andikwa jina - kumaanisha ikiwa wapiga kura wataandika jina lake katika karatasi ya kupiga kura basi kura yake itahesabiwa. Anakubali kuwa hali ilivyo hana uwezo wa kufikia ndoto yake kwa sasa, lakini anaamini siku moja ataingia ikulu.

'Nimeamua kuishi maisha yangu kwa kuwahudumia watu milele'

Brock Pierce ni mwigizaji wa zamani wa watoto ambaye alionekana kwenye densi ya Mighty Ducks na aliigiza kama mtoto wa rais katika filamu ya ucheshi ya First Kid mwaka 1996. Lakini pia ni mfanyabiashara wa teknolojia na bilionea wa sarafu ya dijitali

Kwanini anagombea urais? Moojawapo ya sababu kuu ni kwamba hapendelei hali ya mambo yalivyo nchini.

"Nadhani tunakosa maono ya siku zijazo - Namaaniasha ulimwengu tunaotaka kuishi kufikia mwaka 2030? Tuna mpango gani? Tunajaribu kwenda wapi, unanielewa? Lazima uwe na azma ya kufikia lengo lako. Lakini kile tunachoona ni watu wanaotoa mapendekezo ambayo hayana tija. Inasikitisha sana. Na mimi nina wazo la jinsi tunavyoweza kujikwamua katika janga hilo."

Kwa miaka mmine iliyopita, Bw. Pierce amekuwa akijihusisha na shughuli za kutoa misaada huko Puerto Rico, ambapo wakfu wake umekusanya mamilioni ya dola kuwasaidia wahudumu wa afya kupata vifaa vya kinga binafsi PPE.

Alipoulizwa Wamarekani wanahitaji kupatia masuala gani umuhimu katika miaka minne ijayo, aalipendekeza nchi ikome kufuatialia "ukuaji kwa maslahi ya ukuaji tu", na kupima mafanikio yake kwa jinsi maisha, uhuru, na jinsi ukuaji huo unavyobadilisha hali ya watu.

BBC ilipombana kwa maswali ya kisiasa Bw. Pierce anaye fahamika na Rolling Stone kama "Mfalme wa sarafu ya jiditali" anataka kuhalalishwa kwa bangi na pia anaamini sana uhuru wa mtu binafsi. Amewafadhili wagombea kadhaa wa chama cha Republican kuwania vitikadhaa vya kisiasa.

'Lazima tubadilishe mambo kadhaa ambayo ni msingi wa taifa hili'

Kitu kimoja kinachowaunganisha wagombea binanfsi ni kwamba hawahitaji kuridhisha wafuasi wengi wa chama kupa jukwaa la kujieleza- kwa hivyo wanajiendesha wenyewe na kuangazia masuala yanayowagusa wao binafsi.

Mark Charles ni mfuno mzuri wa kauli hii.

Kitaalamu alifanya kazi ka mtaalamu wa programu za kompyuta na huduma za kiufundi, lakini pia ni mpiganiaji mkuu wa haki ya kijamii juu ya maswala yanayoathiri Waamerika wa asili na watu wa rangi.

Lengo lake ni kuwa mgombea mbadala kwa watu ambao hawajavutiwa na Trump au Biden.