Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: Mshindi atajulikana lini?
Huenda kufikia sasa ulitarajia kuwa fununu kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Marekani kufikia sasa.
Naam, sasa ni nani atakuwa rais ajaye wa Marekani?
Kufikia sasa haijulikani, kwasababu shughuli ya kuhesabu kura bado inaendelea- kumaanisha wagombea wote wawili Donald Trump na Joe Biden wanasubiri matokeo, kwa sasa hakuna aliyepata ushindi.
Ukweli ni kwamba kutokana na muda unaohitajika kuhesabu kiwango kikubwa cha kura zilizopigwa kupitia posta katika uchaguzi huu uliofanyika wakati wa janga la corona, matokeo huenda yakachukua siku kadhaa.
Majimbo kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na Arizona, Georgia na Michigan, zinatarajia kukamilisha shughuli ya kuhesabu kura wakati wowote siku ya Alhamisi. Baada ya kura katika majimbo hayo - kujumuishwa na kura za maeneo mengine ambazo matokeo yalitangazwa usiku wa Jumanne - taswira ya ni nani huenda akaibuka mshindi itapatikana.
Lakini sio hayo tu. Ikiwa matokeo yatapingwa kisheria - kama alivyotishia kufanya Bw. Trump - huenda ikachukua wiki kadhaa kabla mgombea aliyepata ushindi kutangazwa rasmi. Hatua hiyo huenda ikawa ngumu.
Majimbo kuamua mshindi
Kumbuka - ili kuwa mshindi katika uchaguzi wa urais wa Marekani mgombea hahitaji kushinda kwa wingi wa kura. Badala yake mgombea anahitaji kushinda wingi wa wajumbe katika mfumo unaojulikana kama ''electoral college'' jopo la wajumbe maalum walioteuliwa kulingana na kiwango cha wapiga kura katika jimbo husika na idadi ya watu. Mgombea akipata ushindi katika jimbo husika, anashinda kura ya wajumbe waliotengewa jimbo hilo (isipokuwa Nebraska na Maine, lakini huo ni mjadala wa siku nyingine).
Kuna jumla ya wajumbe 538 wanaowakilisha kura zinazopigwa katika majimbo yote kwa jumla - mgombea atakayepata wajumbe 270 atakuwa rais. Kwa hivyo safari ya wagombea wote wawili, kuelekea White House inaamuliwa na ushindi katika majimbo yatakayo wawezesha kupata nambari hiyo muhimu.
Na kama ilivyo kawaida, makabiliano makali yamesalia katika majimbo machache muhimu.
Bwana Biden anapigiwa upatu kupata ushindi kati jimbo Michigan. Pia anaongoza katika majimbo ya Nevada na Arizona, kulingana CNN, CBS, Fox na shirika la Associated Press anatabiriwa kushinda jimbo la Wisconsin.
Ikiwa atafanikiwa kuzoa kura zitakazohesabiwa katika majimbo hayo yote, kwa pamoja atapata jumla ya kura 43 za wajumbe ambazo zitamwezesha kupata kura 270 zinazohitajika kuwa mshindi. Ushindi wa ziada katika jimbo la Pennsylvania au Georgia utawapa kinga Democrats, utakaowahakikishia ushindi hata dosari ikijitokeza.
Kwa bwana Trump, nafasi ya kushinda muhula wa pili wa urais huenda ikatokana na ushindi wake Pennsylvania, ambayo ina kura 20 ya wajumbe. Ikifanikiwa kushinda jimbo hilo na kupata ushindi mwingine katika majimbo yaliyosaliwa yanayoaminiwa kuwa- Georgia, North Carolina, Nevada au Arizona - anaweza kurejea tena White House.
Lakini anakabiliwa na kibarua kikubwa ikizingatiwa idadi ya kura zilizosalia kuhesabiwa.
Kwa nini ushindani uko karibu sana?
Kwanza kabisa kinachojitokeza ni kwamba data za uchaguzi wiki hii hazikuto atawira ambayo haikukamilika.
Robert Cuffe, mkuu wa kitengo cha takwimu wa BBC, anasema ni mapema sana kusema uchaguzi huu umekuwa jinamizi kwa makapuni ya utafiti. Lakini tunachofahamu ni kwamba makadirio ya kura ya maoni ya kitaifa hayakuonyesha ushindani huu mkali tunaoshuhudia.
Kura za maoni za kitaifa zilizofanywa mwisho kabla ya uchaguzi zilimuonesha Joe Biden akiwa mbele ya Bw,Trump kwa karibu pointi nane. Katika majimbo yenye ushindani mkali Bw. Biden pia alitabiriwa kuongoza, lakini kwa kiasi kidogo.
Vipa umbele vya wapiga kura huenda havikueleweka. Licha ya kwamba janga la corona liligonga vichwa vya habari kwa kipindi kirefu cha mwaka, utafiti uliyofanywa Edison ulibaini kuwa ni mmoja kati ya wapiga kura watano waliochukulia virusi vya corona kama suala kuu litakaloamua jinsi watakavyopiga kura. Wengine kadhaa - zaidi ya thuluthi moja ya wapiga kura wote - walisema uchumi ulikuwa suala muhimu.
Mtazamo huu huenda ulimpendelea Bwana Trump - wale ambao walitanguliza uchumi na kazi kwanza walimtegemea sana rais.
Taarifa kwa ufupi ni?
Donald Trumpanaendelea kufanya vyema kuliko alivyotarajiwa na Joe Biden ameshindwa katika majimbo yenye ushindani mkali ambayo yanahesabu haraka kura, hali ambayo inamaanisha kutokuwa na uhakika zaidi tunapongojea majimbo kadhaa muhimu.
Kwa kauli zao wenyewe...
Katika hootuba yake kwa wafuasi wake Joe Biden, alisema: "Tutashinda uchaguzi huu" na kutoa wito wawe na subira.
Donald Trump alisema Republican wameshinda na kudai kura kura zimeibwa lakini huo sio ukweli wa mambo - kama tunavyojua, kura bado zinaendelea kuhesabiwa na hakuna uthibitisho wa wizi wa kura.