Vita vya Syria: 'Mashambulio ya ndege yawaua makumi kadhaa ' Idlib

Waliouawa ni wa kundi la Faylaq al-Sham

Chanzo cha picha, AFP

Iliyochapishwa

Mashambulio ya ndege ya Urusi Kaskazini mwa Syria yamewaua wapiganaji waasi zaidi ya 50 wanaoungwa mkono na Utruruki katika jimbo linalodhibitiwa kwa kiasi kikubwa na waasi la Idlib, zinasema ripoti.

Wengine wengi walijeruhiwa katika shambulio , linaloonesha kuongezeka kwa ghasia katika jimbo hilo.

Ngome ya mazoezi ya kijeshi ya kundi la kiisamu linalojuliikana kama Faylaq al-Sham ilipijgwa.

Shambulio hilo linaweka hatarini mpango wa usitishaji mapigano katika Idlib uliofikiwa na kusimamiwa na Urusi na Uturuki , ambazo kwa pamoja zinaunga mkono pande zinazohasimiana.

Kundi la waangalizi wa Syria lenye makao yake nchini Uingereza -Syrian Observatory for Human Rights limesema kuwa idadi ya waliouawa ni watu 78.

Baadhi ya majeruhi walikua katika hali mbaya, na idadi ya vifo huenda ikaongezeka, waangalizi wanasema .

Kundi hilo limeelezea shambulio hilo lililotokea katika jimbo la Herem Kaskazini -Magharibi mwa mji wa Idlib kama shambulio baya zaidi la mauaji kutokea tangu ulipoanza utekelezwaji wa mkataba usitishaji mapijgano mwezi Machi.

Mkataba huo ulimaliza mashambulio ya serikali katika jimbo hilo ambako watu takriban milioni moja wamesambaratishwa na mapigano na ambalo limedhibitiwa tangu wakati huo.

Wakati usitishwaji wa mapigano ulipotangazwa, Uturuki ilisema kuwa ina haki ya "kujibu mashambulio kwa nguvu zake zote" dhidi ya shambulio lolote la vikosi washirika wa Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Idlib ni jimbo la mwisho linaloshikiliwa na waasi na wapiganaji wa jihadi, ambao wamekuwa wakipijgwa katika vita vya miaka tisa vya wenyewe kwa wenyewe.