Trump na Afrika: Jinsi Ethiopia "ilivyosalitiwa" juu ya bwawa la Nile

Donald Trump amemuunga mkono rais wa Misri kuhusu bawa la Nile

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Kwa wakosoaji wake hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump, kuongeza mvutano kati ya washirika wawili wa Marekani wa muda mrefu, Misri na Ethiopia, kuhusu bwawa kubwa la mto Nile ni ishara ya kufeli kwa diplomasia ya utawala wake barani Afrika.

Wiki iliyopita Bw. Trump alisema kwamba Misri huenda "ikalipua" bwawa lililojengwa na Ethiopia, licha ya kujidai mwezi Januari kwamba anastahili kupewa Tuzo ya Amani ya Nobel kwasababu ya "machango wake" katika utatuzi wa mzozo wa mto Nile.

"Nimezuia kutokea kwa vita. Nimezuia vita mara kadhaa," alisema, muda mfupi baada ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kupewa tuzo hiyo.

Matamshi ya Bw. Trump yalikuwa ya kutatanisha, lakini yalionekana kuashiria jitihada zake - za kuingilia kati mzozo huo kupitia ombi la Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ambaye wakati mmoja aliripotiwa kumuita ''Dekteta wake mpendwa''- kusuluhisha mzozo kuhushu bwawa la Grand Renaissance linalojengwa na Ethiopia.

Misri inaona bwawa hilo kama "tishio kubwa" kwa uhai wake hata kuliko Sudan. Ethiopia, kwa upenda mwingine inachukulia bwawa hilo kuwa na umuhimu mkubwa katika mahitaji yake ya kawa.

Trump ni 'kiungo cha chuki kwa Waethiopia'

Mchambuzi wa masala ya Upembe wa Afrika mwenye makao yake nchini Kenya Rashid Abdi amesema usuluhishi wa Marekani wa mzozo unaozunguka bwawa hilo umeongeza mvutano zaidi kati ya Misri na Ethiopia.

"Ethiopia inaimarisha usalama Katika eneo linalozunguka bwawa hili," Bw. Abiy alisema.

"Hatua yake ya ulinzi inajumuisha kutangaza eneo la Benishangul-Gumuz, ambalo bwawa hili lipo kuwa eneo ambalo anga zake zinadhibitiwa, huku kukiwa na ripoti kwamba Ethiopia imeweka ulinzi mkali. Huenda inahofia shambulio la ndege kutoka Misri."

litakapokamilika bwawa hilo litakuwa kubwa zaidi linalozalisha umeme barani Afrika

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, litakapokamilika bwawa hilo litakuwa kubwa zaidi linalozalisha umeme barani Afrika

Alisema hii inamaanisha Bw. Trump alifeli kung'amua jinsi diplomasia inavyofanya kazi duniani.

"Ana dhana potofu kwamba anaweza kufikia mkataba kama hali inavyofanyika katika ulimwengu wa kibiashara. Kwa hivyo aliachia Hazina ya Marekani jukumu la majadiliano, wakati sera ya kigeni inatakiwa kuendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje. Matokeo yake yamezidisha hali kuwa mbaya zaidi," aliongeza Bw. Abdi.

Marekani ililaumu Ethiopia kwa kutokuwa na fikra njema baada ya nchi hiyo kuendelea mbele na mpango wa kujaza maji bwawa hilo kabla ya hoja iliyoibuliwa na Misri na Sudan kuhusu mtiririko wa maji katika nchi zao kupata ufumbuzi, na kuamua kuipunguzia msaada wa thamani ya dola milioni 100- Licha ya kwamba Ethiopia ni mshirika muhimu kwa Marekani katika juhudu za kupambana na wanamgambo wa Kiislam katika eneo la Upembe wa Afrika.

"Ethiopia inahisi kusalitiwa na Marekani na sasa Trump anaonekana kuwa na kiwango cha chuki na Waethopia wengi," Bw. Abdi alisema, akiongeza kuwa wanatumai Joe Biden atashinda uchaguzi wa urais wa Novemba tarehe 3.

W Gyude Moore, mwanazuoni wa ngazi ya juu wa masuala ya sera katika Kituo cha Maendeleo ya Kimataifa chenye makao yake nchini Marekani amesema hatua ya utawala wa Trump kupendelea Misri si wa kushangaza kwa sababu lengo lake kuu la kimataifa lilikuwa kuunganisha Israel na mataifa ya Kiarabu.

Mapinduzi ya kidiplomasia ya Trump

Licha ya kwamba Misri imekuwa na mgogoro wa kidiplomasia kwa muda mrefu na Israel, utawala wa Trump hauna mpango wa kuvuruga mambo zaidi wakati inamhitaji Bw. Sisi kuisaidia kushawishi nchi zingine za Kiarabu kutambua Israel, Bw. Moore alisema.

"Kwa hivyo, utawala huo umekuwa sehemu ya mezzo wa bawl la Nile kwa kuegemea upande wa Misri," aliongeza.

Lengo lake la kufanikisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Israel na nchi za Kiarabu pia ilichangia kuamua sera yake kwa Sudan, ambayo iliipatia Bw. Trump mapinduzi makubwa ya kidiplomasia kwa kukubali kuregesha uhusiano wake na Israel wiki mbili kabla ya uchaguzi wa Marekani.

Endapo Bw. Trump,atashinda mutual wa pili, anatarajiwa kuendelea kuishinikiza Ethiopia kutatua suala la Misri na Sudan kuhusu bwawa la Nile, na wakati duo huo kuhakikisha Sudan inaondolewa katika orodha ya Marekani nchi "zinazofadhili ugaidi", kufungua njia kwa kupata msaada wa kiuchumi inayohitaji kwa dharura.

Bw Moore amesema japo utawala wa Trump utahitaji kupongezwa ikiwa bunge la Marekani litaidhinisha kuondolewa kwa Sudan katika orodha ya ugaidi, uamuzi wake wa kuhusisha hatua hiyo na kutambuliwa kwa Israel itakuwa na Atari kwa serial ya Waziri Mkuu Abdalla Hamdok, ambayo iliingia madarakani mwaka jana baada ya kufurushwa kwa kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir.

"Suala la kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Israel limeleta mgawanyiko mkubwa katika jamii ya Wasudan. Huenda ikawa hoja itakayotikisa umoja wa nchi wakati serikali tayari inakabiliwa na changamoto za kiusalama na amani ambayo bado ni dhaifu," Bw. Moore aliongeza.

Raia wa Sudan wameendelea kutaka haki kwa waathiriwa wa utawala uliopita

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa Bw. Abdi, hofu yake zaidi kuhusu athari za sera za Trump kwa Afrika ilikuwa ni "vita vipya baridi" kati ya Marekani na China.

Mfano mmoja mzuri ni ukweli kwamba China imewekakambi yake ya kwanza ya kijeshi nchini Djibouti, karibu na kambi ya Marekani inayotumiwa kwa mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambowa Kislamu nchini Somalia, ngome kuu katika oparesheni yake dhid ya ugaidi Afrika na Yemen.....

Mvutano na China Kwa Bw. Abdi, hofu yake zaidi kuhusu athari za sera za Trump kwa Afrika ilikuwa ni "vita vipya baridi" kati ya Marekani na China.

Mfano mmoja mzuri ni ukweli kwamba China imewekakambi yake ya kwanza ya kijeshi nchini Djibouti, karibu na kambi ya Marekani inayotumiwa kwa mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambo wa Kislamu nchini Somalia, ngome kuu katika oparesheni yake dhid ya ugaidi Afrika na Yemen.

"Hii karibuni ndege za kivita za Marekani, zilikuwa zinakuja kutua. Wachina walifanyia majaribio kifaa ambacho kiliwafanya marubani wa Marekani kushindwa kuona pakutua. Ilikuwa na scheme katika sinema ya James Bond," Bw Abdi alisema.

"Chini ya utawala wa Trump, Marekani imekuwa mpinzani mkuu wa sera za China lakini China imeendelea kuonesha nguvu yake. Hali ambayo ni hatari katika eneo la Upembe wa Afrika," Bw. Abdi aliongeza.

Kama sehemu ya juhudi za kabiliana na ushawishi wa ukuaji wa kiuchumi wa China katika bara hilo, utawala wa Trump ulibuni mpango, wa ustawi wa Afrika mwaka 2018 Kama kitovu cha sera zake barani humo.

China ilijenga kambi yake ya kwanza ya kikjeshi ugenini Djibout

Chanzo cha picha, AFP

Aliongeza kuwa uwekezaji wa Marekani barani Afrika awali ilikuwa katika sekta ya mafuta na gesi lakini uwekezaji huo umeshuka vibaya kutokana na kukua kwa mfumo wa kuzalisha mafuta kutoka kwa miamba nchini Marekani.

Utawala wa Trump ulitenga fedha za kufadhili makampuni yake mwaka 2019 ili zijiimarishe barani Afrika.

"Wanataka kuzipatia uwezo wa kifedha mashirika ya Marekani. Yamekuwa yakilalamika kwamba hayawezi kushindana na makampuni ya china yaliyo na fedha. Ukiangalia katika sekta ya Teknolojia ya Mawassiliano, karibu asilimia 70 ya uti wa mgongo wa teknolojia ya mawasiliano ya Afrika inahusishwa na China," Bw. Moore alisema.

'Kuhujumu' Muungano wa Afrika

Utawala wa Trump pia umeamua kuondoa kipengee cha sheria ya Nafasi ya Ukuaji wa Afrika itakapomalizika mwaka 2025. Ilikuwa sera ya Marekani Barani Afrika iliyowekwa utawala wa Rais Bill Clinton, ambayo inazipatia nchi za Afrika nafasi ya kufikia soko la Marekani.

Bw. Moore anasema utawala huo umejikita zaidi katika masuala ya kibiashara na tayari imeanza kufanya mazungumzo na Kenya - ambayo ni kitovu cha biashara katika kanda ya Afrika Mashariki ambako China imejenga miundo mbinu ya bararbara ambayo Marekani inaamini ina lengo la kuunganisha njia za biashara zitakazoiwezesha nchi hiyo ya mara Asia kujiimarisha barani humo na pia kuwa na ushawishi mkubwa duniani.

China imejenga barabara, reli na viwanja vya mpira Afrika

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, China imejenga barabara, reli na viwanja vya mpira Afrika

''Utawala wa Trump unawake kufanya kazi na Kenya , ili baadaye itumie vigezo iliyotumia Kenya kufanya kazi na mataifa mengine ya Afrika," Bw. Moore alisema.

"Kenya imekubaliana na Marekani kwasababu ilitumia mkataba wa Agoa kwa manufaa yake na haitaki kupoteza nafasi ya kufanya biashara na nchi hiyo a," Bw. Moore alisema.

Hii ni licha ya kuwa Kamishena wa Muungano wa Afrika wa kitengo cha biashara Albert Muchanga kupendekeza haja ya majadiliano ya pamoja kwa "sauti moja" kufikia ''makubaliano kati ya Afrika na Marekani.

Bw. Moore aid anasema uamuzi wa Marekani huenda ukahujumu jitihada za Muungano wa Afrika kuimarisha kwa pamoja chumi za mataifa ya bara Afrka kwa lengo la kuifanya Afrika kuwa soko moja huru.