Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Daktari wa India anayewatunza maelfu wa tembo
Kushal Konwar Sarma anafahamika na wengi kama ''daktari wa tembo'' katika ulimwengu wa uhifadhi wa wanyamapori nchini India. Ameishi miaka 35 ya maisha yake kuwatunza tembo, kuokoa maisha ya maelfu yao katika misitu ya India na Indonesia, alimsimulia mwandishi wa BBC Hindi Dilip Kumar Sharma.
"Najihisi mwenye furaha nikiwa karibuna tembo," anasema Dk Sarma. "Ule muda nimeishi na tembo ni mwingi kuliko ule muda nimeishi na familia yangu."
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 60 alikulia katika kijiji cha Barma kilichopoJimbo la Assam kaskazini mashariki mwa India ambako ni nyumbani kwa karibu tembo 5,000 kati ya tembo 27,000, nchini humo kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2017.
Anasema ana uwezo wa kuelewa ''lugha'' ya tembo. "Mbali na kuwalisha, Nawasiliana nao kupitia lugha ya ishara," akiongeza kuwa "baadhi ya tembo wanamtambua".
Dk Sarma alipewa tuzo ya Padma Shri, mbayo ni heshima ya juu inayopewa raia,kutokana na kazi yake mapema mwaka huu. Kulingana na takwimu lake mwenyewe amewatibu zaidi ya tembo 10,000 kufikia sasa.
Alianza shughuli hiyo mwaka 1984, alipomtibu tembo mgonjwa chini ya uangalizi wa mwalimu wake, Profesa Subhash Chandra Pathak.
"Nakumbuka mara ya kwanza nilipoandamana naekwenda katika mbuga ya kiraifa ya Manas kuwatibu tembo. Nilifurahi sana siku hiyo," Dk Sarma anasema.
Uhusiano wake na tembo unaweza kufuatwa tangu utoto wake , wakati familia yake ilipomtunza tembo wa kike anayeitwa Laxmi nyumbani kwao.
"Nilipotimiza umri wa karibu miaka saba, Nilikuwa nikimkalia mgongoni Laxmi na kuzunguka naye kijijini - nakumbuka sana zama hizo na hivyo ndiyo namna nilianza kuwapenda tembo."
Upendo wake kwa wanyama hao uliimarisha taaluma yake kama daktari wa kuaminika hasa msimu wa masika. Assam hukumbwa sana na mafuriko, hali ambayo inawaweka wanyama katika hatari.
Mbuga ya Kitaifa ya Kaziranga, ambayo imetambuliwa na Unesco kama turathi ya kimataifa, ni moja ya maeneo yanayoathiriwa na mafuriko. Hivyo karibuni Jimbo hilo lilikumbwa na mafuriko mwezi Julai na maafisa walisema karibu wanyama 51 katika mbuga hiyo walikufa.
"Wanyama huathirika sana wakati wa msimu wa mafuriko. Wanyama wengi hufa maji hata tembo wanasombwa na maji," Dk Sarma, ambaye mara kwa mara husaidia katika jitihada za kuwaokoa wanyama, anasema.
"Ni mambo la kwaida kwa watoto wa tembo kutenganishwa na mama zao. Katika hali kama hizo, wanahitaji kupewa matunzo. Hiyo ndio sababu nasaidia wakati wa mafuriko."
Hajapokea ombi rasmi la kwenda kuwasaidia wanyama wakati wa mafuriko. "Lakini najitolea kufika kufanya hivyo kwasababu nataka kujaribu kadri ya uwezo wangu kuwaokoa wanyama wengi iwezekanavyo."
Anasema amehatarisha maisha yake mara akitekeleza wajibu wake. " Kati mwingine najiuliza nilinusurika vipi?" anaelezea.
"Siku moja nilikesha juu ya mti katika juhudi za kujaribu kumtuliza tembo mkali ambaye mimi na wenzangu tulitaka kushika na kupatia matibabu."
Lakini licha ya hatari hiyo, anasema kazi yake imekuwa ya kurudhisha.
Anatarajia kumhamasisha bunt yake, ambaye amekamilisha shahada ya sayansi ya udaktari wa mifugo kuendeleza kazi yake.
"Nataka binti yangu afuate nyayo zangu kwa kuendeleze kazi ya kuwatibu tembo nitakapostaafu."