Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Marekani yaidhinisha rasmi dawa ya remdesivir
Mamlaka ya Marekani yameiidhinisha dawa aina ya remdesivir kuwatibu wagonjwa wa Covid-19 hospitalini.
Mamlaka ya chakula na dawa nchini Marekani (FDA) imesema Veklury, ambalo ni jina la dawa sokoni, imeweza kuwasaidia wagonjwa katika wastani wa siku tano wakati wa majaribio.
"Veklury ni dawa ya kwanza kuidhinishwa na mamlaka ya chakula na dawa kutibu ugonjwa wa corona," FDA ilieleza kwenye taarifa yake.
Wiki iliyopita Shirika la afya duniani (WHO) lilisema kuna ushahidi mdogo kuhusu ufanisi wa dawa ya remdesivir kumponya mgonjwa wa Covid 19.
WHO lilisema hii ni kutokana na utafiti wake, lakini mtengenezaji wa dawa hiyo kampun ya Gilead alikataa matokeo ya jaribio lililofanywa.
Remdesivir ilikuwa inaruhusiwa kutumika wakati wa dharura pekee nchini Marekani tangu mwezi Mei.
Hivi karibuni Rais Donald Trump alipatiwa dawa hiyo baada ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.
Mamlaka ya dawa na chakula ilisema nini?
Katika taarifa iliyotolewa na FDA , imesema dawa hiyo iliidhinishwa Alhamisi kwa ajili ya matumizi ya watu wazima na wenye umri wa miaka 12 na zaidi ambao wana kilo takribani 40, na wale ambao watakuwa wamelazwa kwa ajili ya kutibiwa corona.
"Leo hii kuidhinishwa kwa dawa hiyo imeambatanishwa na takwimu za matokeo ya majaribio kadhaa yaliofanyika kuthibitisha na kuona kuwa ni hatua kubwa muhimu ya kisayansi imefikiwa katika kukabiliana na janga la virusi vya corona," alisema msimamizi wa FDA Stephen Hahn.
Mamlaka hiyo imesema uamuzi huo uliungwa mkono na uchambuzi wa data kutoka kwa majaribio matatu ambayo yilijumuisha wagonjwa waliolazwa kutokana na Covid 19 na wale ambao hawakuathirika sana na Covid-19.
Utafiti mmojawapo umeonesha kuwa ''wastani wa muda wa kupona Covid-19 kwa kutumia dawa ya Veklury ilikuwa siku 10 tofauti na nyingine za placebo kuwa siku 15".
Vipi kuhusu utafiti wa WHO?
WHO , ilijaribu kuona matokeo ya tiba nne muhimu watu wanne remdesivir ilikuwa moja wapo,lakini pia walichunguza dawa ya malaria ya hydroxychloroquine, interferon, pamoja na dawa dhidi ya makali ya virusi vya Ukimwi lopinavir na ritonavir.
Dawa nyingine ya Dexamethasone, ambayo inapatikana kwa bei nafuu imeonekana kutumika zaidi kwa wagonjwa wa Covid-19 kwa wagonjwa walioko katika chumba cha wagonjwa mahututi nchini Uingereza, ilikuwa haijajumuishwa katika utafiti huo.
Dawa nne zilifanyiwa majaribio kwa jumla ya wagonjwa watu wazima 11,266 katika hospitali 500 kutoka nchi 30.
Na matokeo yameonesha kuwa hakuna dawa yoyote kati ya hizo ambayo inafanya kazi kwa ufanisi katika kutibu corona , kupunguza vifo au muda wa kukaa hospitalini, WHO imesema.